Simba katika kundi la kifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba katika kundi la kifo

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, May 16, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAKATI Shirikisho la Soka Afrika CAF likiiweka Simba katika Kundi B, kocha Moses Basena amesema anaamini wachezaji wake ni kama kikosi cha askari jeshi hivyo wapo tayari kuwavaa Wydad Casablanca na kuiondosha katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Katika ratiba iliyotolewa jana na CAF, Simba itakuwa kwenye Kundi B kama ikifanikiwa kuwatoa Wydad Casablanca na itakuwa pamoja na Al Ahly (Misri) EST (Tunisia) na Moloudia Club d’Alger (Algeria).

  Simba inacheza na Wydad Casablanca mwishoni mwa wiki hii baada ya kushinda rufaa yake waliyoiwasilisha katika kamati ya mashindano ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kupinga kitendo cha timu ya TP Mazembe kumchezesha mchezaji Janvier Besala Bokungu wakati timu hizo zilipopambana.

  Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya mashindano ya CAF iliyotolewa juzi, Mazembe imepokwa ushindi kwa madai ya kufanya udanganyifu na kukiuka kifungu VIII, kifungu 24, kifungu 26(sifa za mchezaji) na kifungu 29 ambapo sasa nafasi yake imetwaliwa na Simba ambayo itaivaa Wydad ya Morocco katika pambano litakalofanyika sehemu huru wiki moja ijayo.

  Akizungumza na Mwananchi jana Basena alisema licha ya kwamba uamuzi wa CAF umekuja wakati wachezaji wa Simba wakiwa mapumzikoni haimaanishi kwamba uwezo wa wachezaji umepotea kabisa.

  "Kuwa likizo haimaanishi uwezo wa wachezaji umepotea mpaka asilimia sifuri, wapo wanaocheza Harambee Stars (timu ya taifa ya Kenya),Taifa Stars(Tanzania)na The Cranes(Uganda)watakuwa na msaada mkubwa.

  "Sisi ni kama askari wa jeshi ambao muda wowote unaweza kuitwa vitani ukapigane hivyo sioni cha kuhofia naamini tutapambana na kushinda pia,"alisema Basena.

  Basena ambaye pia amewahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu Uganda na timu za KCC, Simba na URA alisema kikosi chake kitaingia kambini leo kujiandaa na mechi hiyo pamoja na michuano ya Kombe la Kagame.

  "Kesho(leo) tunaanza mazoezi, jambo muhimu naomba uongozi uwaite haraka, hii ni fursa ya aina yake tunatakiwa tujipange ili tuweze kupambana na kupata matokeo mazuri,"alisema Basena.

  Alisema anaandaa programu ya muda mfupi ya wachezaji ambapo watakuwa wakifanya mazoezi kutwa mara tatu kwani wana muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda katika mchezo huo.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu alisema,“Simba itawatumia wachezaji wake waliosajiliwa kushiriki mashindano ya klabu bingwa wakiwemo wale waliouzwa TP Mazembe.”Alisema,“Wachezaji hao bado ni mali ya Simba ingawa wameshauzwa, lakini uhalali wa mchezaji kuuzwa ni ITC na mpaka hivi sasa TP Mazembe haijaomba ITC ya wachezaji hao, hivyo bado wanahesabika kama wachezaji halali wa Simba katika mashindano haya”.

  Mbali na kuwatumia wachezaji hao pia Kaburu alisema, “Wachezaji wa Simba waliokuwa likizo na wengine waliokuwa katika mashindano mbalimbali tayari tumeishawandikia barua na watawasili kesho asubuhi (leo).”

  Makundi
  Kundi A
  Hilal (Sudan)
  Coton Sport Garoua (Cameroon)
  Enyimba (Nigeria)
  Raja (Morocco)

  Kundi B
  Ahly (Misri)
  EST (Tunisia)
  Moloudia Club d’Alger (Algeria)
  Simba (Tanzania) au Widad de Casablanca (Morocco)
   
 2. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapa ni kumwomba Mungu atuwezeshe tuvuke hatua hii.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  God doesn't play dice.
   
Loading...