Nisingependa hii kitu itokee, maana watani tutawakoma, ila ingependeza kama tukishuka, naona tunafanya mambo kimazoea tu, kuwa sisi ni chama kubwa hatuwezi cheza daraja la kwanza.
Viongozi waamke, kwa kiwango wanachocheza simba, inawezekana kabisa kushuka daraja. Niliangalia mechi na Standa United, sikuamini kiwango wanachocheza simba, ni cha chini ya chini, wachezaji hawana hamasa, yaani kiwango cha mechi nyingi za simba ni chini ya average.
Simba karibu yote inahitaji overhaul, na waganda mie binafsi wala siwafagilii ndani ya Simba. Hawana mchango, mchango wa Coutinho pekee kwa yanga ni mkubwa kuliko wachezaji wote wa nje walio simba.
Ifike wakati uongozi ukubali kuwa kusajili wachezaji wa nje sio fashion, kiwango ni muhimu, kama yawezekana wasajili majembe ya hapa hapa bongo na pia uongozi ujipange.
Wachezaji simba karibu wote wamekuwa laini laini tuu, beki laini, kiungo laini, ushambuliaji ndo kabisaaaa, yaani simba sasa hivi nikiangalia, huwa naona angalau Ndemla ndo anajitahidi, na Singano kidogo (kinachomwangusha lishe) hawa huwa wanakimbia uwanjani kusaka kila mpira, mkude sijui kimemkuta nini. Isihaka anatumia akili sana ila mbavu hana, alitakiwa awe na partner wake mwenye roho mbaya, sasa wote wawili ni akili ila mbavu hamna.
Inasikitisha sana hii Simba!!