Simba Ina Wakati Mgumu Kwa Yanga

Simba Ina Wakati Mgumu Kwa Yanga

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Simba na Yanga zinakutana kesho katika pambano la watani wa jadi la msimu wa 50 wa ligi ya hadhi ya juu zaidi ya Bara, huku mazingira ya kisoka ndani ya timu hizo mbili yakiwapa mabingwa watetezi nafasi kubwa zaidi ya kuwafunga 'Wekundu wa Msimbazi'.
Mazingira ndani ya Simba na Yanga yanaipa timu ya Jangwani nafasi kubwa ya kuwafunga mabingwa wa mwaka jana kwa sababu, kwanza, Wekundu wa Msimbazi wapo katika kipindi cha mpito kuelekea kutengeneza timu imara kama iliyoipa taji namba 19 mwezi Mei, 2012.
Ingawa baada ya mechi nane za kwanza msimu huu, Simba si tu ndiyo timu iliyo katika kilele cha msimamo wa ligi kuu ya Bara kutokana na wingi wa pointi bali pia ndiyo yenye uwiano mkubwa zaidi wa magoli katika michuano hiyo:
Kinachoipa nafasi kubwa Yanga hata hivyo, tunaona Nipashe, ni ukweli kuwa, kwanza, Simba imecheza mechi chache za ugenini ikikutana na timu dhaifu za Rhino Rangers na JKT Oljoro na, pia, karibu nusu ya tofauti ya mabao 12 hayo inayoringia yalipatikana katika mchezo mmoja dhidi ya timu dhaifu zaidi kwenye ligi kuu msimu huu ya Mgambo JKT, tena kwenye Uwanja wa Taifa.
Iwe ni golini, katika safu ya ulinzi, kiungo na hata ushambuliaji Simba itaingia uwanjani kesho ikiwa haina kombinesheni iliyokamilika ya wachezaji wenye uzoefu wa mapambano ya watani wa jadi wa Bara huku mahasimu wao Yanga wakiwa na timu ile ile ya msimu uliopita ONGEZA Mrisho Ngasa.
Aidha, katika benchi la ufundi, Simba inaweza kuwa na kocha ambaye aliifikisha fainali ya Kombe la CAF la zamani la klabu za Afrika mwaka 1993; hatua ambayo ni rekodi kwa klabu za Bara.
Lakini ni katika Abdallah Kibadeni, tunaona Nipashe, ambapo Simba ina matatizo kulinganisha na wapinzani wao wa kesho Yanga.
Ni katika Kibadeni, tunaona Nipashe, ambapo Simba ina matatizo yanayoipa nafasi kubwa ya kufungwa na Yanga kwa sababu kwanza soka limebadilika sana tangu mwaka 1993 na tabia ya mwalimu huyo ya kuponda wachezaji wake hadharani pindi timu inapokosa ushindi katika michezo ya ligi.
Falsafa ya msingi ya mchezo wowote ambao unahusisha zaidi ya mchezaji mmoja wa upande mmoja uwanjani ni kwamba timu hiyo hushinda pamoja na kufungwa pamoja.
Ni makosa kitaaluma basi, kwa mfano, Kibadeni kumlaumu mbele ya vyombo vya habari mlinda mlango Abel Dhaira kuwa ndiye aliyesababisha sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza dhidi ya Rhino Rangers.
Ni makosa kitaaluma, tunaona Nipashe, kwa sababu bado Simba ingeweza kushinda mchezo ule, kwa mfano, kama washambuliaji wangetumia vizuri zaidi nafasi za kufunga ambazo baada ya dakika 90 zilihesabika kuwa mashuti ambayo hayakulenga lango, ama kama mchezaji wa kiungo asingepoteza mpira ambao ulizaa shambulizi lililozaa nafasi ya wapizani kupata nafasi ya kumtungua Dhaira.
Aidha, sera ya Kibadeni ya kuengua kwenye timu wachezaji ambao ama wameonekana kuwa hawakujituma katika mchezo uliotangulia ama wenye utovu wa nidhamu mazoezini na kambini ni njia nyingine ambayo imeidhoofisha Simba kabla ya mchezo wa kesho.
Wakati kocha wa Yanga Ernie Brandst akiwa na wachezaji 29 katika kambi ya Yanga yenye mshikamano na utulivu kisiwani Pemba, Simba ina upungufu mkubwa katika kukosekana kwa kiungo Henry Joseph ambaye akiwa nahodha wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, uzoefu wake katika kucheza kwenye ligi kuu ya Norway na mipambano ya watani wa jadi pia ulikuwa muhimu mno kesho.
Henry ameachwa katika kambi ya Simba kwa madai ya kukaidi maagizo ya benchi la ufundi mazoezini, lakini katika soka la kileo uwezo wa mchezaji humrejesha kikosini kwa ajili ya mechi inayofuata hata kama alikunjana jezi na kocha mazoezini baada ya hatua za kinidhamu kufuata mkondo wake hata hivyo.
Bahati nzuri kwa Simba kabla ya mchezo wa kesho, hata hivyo, ni kuwa mipambano ya watani wa jadi huwa haiangalii kiwango ambacho timu husika zinavyo kwa wakati huo.
Simba iliyo katika mazingira magumu kulinganisha na Yanga inapaswa kutiwa moyo na timu ya mwanzoni mwa miaka ya 1980, kwa mfano, ambayo ilitakiwa kuifunga Yanga ili isishuke daraja na ikafanya hivyo kweli.

CHANZO: NIPASHE
 
Hiyo ni tahariri au? Kama ni tahariri basi mhariri wake ni dhaifu sana! Mhariri ameungaunga tu maneno yasiyo na logic yoyote labda kwa sababu yeye binafsi ni mpenzi wa Yanga. Uchambuzi wake sio yakinifu; anapaswa kurudi shule ya uandishi wa habari kusoma tena.
 
Back
Top Bottom