Simba imempeleka kwa mkopo (miezi 6) mshambuliaji wake wa kimataifa, Blagnon katika klabu ya Muscat

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,949
1,940
Tunasajili hili kufurahisha wanachama sau tunasijili ili kukidhi mahitaji ya timu?
========

MSHAMBULIAJI wa Simba, Frederick Blagnon ameondoka Dar es Salaam leo kwenda Oman kupitia kwao Ivory Coast kwa ajili ya mipango ya kujiunga na Fanja ya nchini humo.

Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu kwamba Blagnon anakwenda kwao, Ivory Coast kushughulikia visa haraka ili aende Oman kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Fanja.

Na Katibu wa Simba, Patrick Kahemele akathibitisha alipoulizwa; “Ni kweli kaondoka kwa ajili ya mipango ya kwenda kujiunga na timu moja ya Oman, bado hatujaijua.
Frederick Blagnon anakwenda Oman kwa ajili ya mipango ya kujiunga na Fanja

Atapitia kwao, baadaye atakwenda Ivory Coast,”amesema.
Blagnon aliyekuwa analipwa zaidi Simba, dola za Kimarekani 3,000 (zaidi ya Sh. Milioni 6) kwa mwezi alijiunga na Simba SC Julai mwaka jana kutoka African Sports ya kwao kwa dau la Sh. Milioni 100, ambazo zilitolewa na mfanyabiashara Mohamed Dewji anayetaka kununua hisa kwenye klabu hiyo.

Hata hivyo, pamoja na kusajiliwa kwa dau kubwa na kulipwa mshahara mkubwa, mchezaji huyo ameshindwa kung’ara kwenye kikosi cha timu hiyo hata Simba imeridhia mpango wa kumuuza Oman.

Na hiyo inafuatia timu kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika dirisha dogo Desemba kwa kumsajili mchezaji Mtanzania, Juma Luizio mwenye uzoefu wa mashindano makubwa kutoka Zesco United ya Zambia.

Pamoja na Luizio aliyekwenda Zambia akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, Simba SC imemsajili kiungo mshambuliaji chipukizi, Pastory Athanas kutoka Stand United ya Shinyanga, ambaye naye ameanza vizuri.

CHANZO: Bin Zubeiry
 
Baada ya usajili wa Mshambulizi galasa kabisa kutoka nchini Ivory Coast ambaye wengi wanasema alisajiliwa kwa ushawishi wa aliyekuwa mlinda mlango wa simba aliyefungashiwa vilago vyake dirisha dogo Vicent Angban...Klabu hiyo imeamua kumpeleka kwa mkopo mchezaji huyo huku ikiendelea kumgharamia gharama zote za misharaha na kila kitu......
 

Attachments

  • 112.PNG
    112.PNG
    72.1 KB · Views: 64
pale pastory athanas/juma luizio anaposajiliwa kuziba pengo la Blagnon.....

haya mambo yanachekesha sana...!

  1. hilini kosa kama ilivyokuwa kumuondoa Kiiza na kurudisha Kiongera.
  2. hili ni kosa ambalo linakamilisha ndoto nyingine ya kuwakosehsa ubingwa wa vpl..sidhani kama luizio na athanas wanaweza perfom kwa kiwango cha kumfikia huyu galasa anayeenda kwa mkopo.
 
Back
Top Bottom