Simba haina mastaa, imekusanya majina ya kihistoria... We subir tu mkuu!kwa kombe la Vodacom/ligi kuu labda waliibe
Okwi tunamjua,Niyonzima tunamjua,hawa wakichapwa mechi mbili mfululizo lazima Kieleweke
Hata madrid kuna kipindi ilikusanya mastaa wote wa dunia ila hakuna walichoambulia
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitarajia ukichambue kikosi kizima na uonesha udhaifu wa kikosi na mapungufu yake ndio utoe hitimisho kumbe ni ngada imejaa kichwaniNinachokiona baada tu ya msimu wa Ligi kuanza, hizi kelele zinazotokana na Imani ya mashabiki wa Simba kuamini kwamba watafanya vizuri saaana msimu ujao, hali itakua tofauti sana..
Yaani kama ni radio, basi betri zitanyofolewa ghafla...
Na ni kama umeme, basi fuse ya taa itaungua...
Ni mtazamo tu, kwani nikiangalia kikosi cha mwaka jana kilikua bora saana, hakukuwa na sababu ya kuingiza makinikia (wahenga) ambao wanajikwaakwaa tu pale mbele.... Mashabiki wanatembea na historia ya wachezaji tu, yaani kama vile Yanga kuwarudisha Mwalala na Ambani....
Ila kwakua wanayo hela, labda waliamua kuonyesha jeuri ya pesa tu, ila kama team, haiendani na akili waloijenga... Tusubir tutarudi kwenye huu uzi baadae muda ukifika........
Mtazamo tu!
Timu za Simba na Yanga zinapokutana hakuna ushindi wa asilimia 90.Mmemsikia Julio alivyosema jana,Yanga sio ya kubeza,wanajua wakifanyacho Simba isibweteke.Kaongea kama kocha.
Sent using Jamii Forums mobile app
KariaTumesajiri majembe ya ukweli Kiria na Wambura Ndala kazi mnayo ha ha ha ha ha wanataka kukimbia wakati hauna breki
Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ni mawazo yako wewe na kama wewe (nikiwamo na mimi). Ila wapenzi wa Simba na wapinzani wengine wa Yanga wanaamini kwamba hicho kikosi ni duni sana; ushindi uliletwa zaidi na 'Double M' (Malinzi na Manji). Wanaendelea kuamini kwamba kukosekana kwa 'wachezaji hao muhimu' msimu huu, Yanga haitakuwa na chake. Tujaalie wako sahihi. Sasa kama majina ya waliosajiliwa ndiyo yanayoamua ubingwa, wanasemaje kuhusu Singida United?Kwa msimu huu timu ya Simba ndiyo yenye kikosi bora zaidi, lakini sio kigezo cha kuchukua ubingwa wa Ligi.
Misimu mitatu iliuliyopita Yanga ilikuwa na kikosi kizuri zaidi, kutokana na ufadhiri wa manji.
Washambuliaji.
Ngoma, Tambwe, Chirwa, Msuva.
Katikati.
Niyonzima, Kamusoko.
Nyuma.
Bossou, Dante, Yondani, Kanavaro.
Ilikuwa halali kwao kuchukua ubingwa wa Ligi.
Msimu huu Simba sc waliahindwa kuchukua ubingwa tatizo litakuwa kwa benchi la ufundi likuongozwa na kocha Amog, na Mayanja kama msaidizi wake.
Ni msimu wa Simba sc. mtake msitake.
Unashangaa hilo? Hushangai Real Madrid kufungwa na Man U ikaja kuifunga Man U?Maneno ya mkosaji...mfungwe na ruvu shooting mje kuifunga simba
What goes around always comes around