Ngoheranga
Member
- Oct 13, 2012
- 29
- 35
Kama mdau wa soka jana nilifuatilia na kufurahia sana sherehe ya wana-simba ambayo kiuhalisia ni tukio waliolianzisha miaka kadhaa iliyopita na linaloendelea kukua mwaka hadi mwaka. Si ajabu pia kuona miaka michache iliyopita watani wao wa jadi, Yanga wakaanzisha nao Wiki ya Yanga yenye maudhui makuu kama yale ya majirani zao. Si jambo baya kuiga kizuri cha mwenzio.
Pamoja na mapungufu machache yaliyojitokeza katika mpangilio mzima wa tamasha lenyewe kuanzia uingiaji uwanjani kwa walioweza kuingia, malalamiko ya tiketi feki, mwenendo wa matukio n.k nachelea kusema kwa ujumla wake tamasha lilifana kwa asilimia kubwa. Kitu ambacho mpaka sasa nashindwa kukielewa ni kuonyeshwa yule ndugu mwenye ulemavu wa ngozi alievaa pampasi.
Lengo hasa ilikuwa kutuambia nini sisi watazamaji, bado sipati picha, inavyoonekana hata mwenyewe pale jukwaani hakuwa ana uhakika wa nini alitakiwa kufanya. Kitendo kile, katika nafsi yangu kimetia doa kubwa maana nzima ya sherehe yenyewe, kwangu ule ni udhalilishaji, mlemavu yule wa ngozi naamini amekubali kufanya alichoambiwa afanye kutokana na njaa tu, pesa imemrubuni na akatii maagizo.
Kama mwana michezo na ninaejua na kufuatilia kwa karibu siasa za timu zetu pendwa za Yanga na Simba naweza kuwa na tafsiri ambayo wengi wetu tumeihisi, lakini je Ina afya kwa maendeleo ya mpira wetu pamoja na utani wetu wa jadi? Tusipokemea sasa hivi tutaanza kuona mpasuko mkubwa huko mbele ya safari. Kama utani wa jadi basi tuufanye kistaarabu bila udhalilishaji wa utu.