Nakumbuka enzi ya Aussems, ilikuwa Simba akifungwa mechi moja au ku draw basi next game kocha atabadilisha mfumo, anaweza mpanga mchezaji mmoja juu ya mabeki ili kuongeza ulinzi, na Kennedy Juma alikuwa anatumika zaidi kwenye hili.
Lakini huyu kocha wetu wa sasa hajui kuiona hatari na kuifanyia kazi mapema, hizi counter wanazopiga hawa jamaa ni wazi anatakiwa mtu wa kusimama juu ya mabeki asipande, kazi yake iwe kuzima haya mashambulizi ya kushtukiza ya hawa jamaa, lakini naona kocha yupo tu, akili yake yote kushambulia, then tukifungwa aanze ku panic .