Simanzi yatawala mazishi ya watoto aliowaua mama

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,113
maziko%281%29.jpg

Majeneza ya watoto watatu Noel, Rose na Anthony Thadeo Kihanda yakionekana katika ibada ya mazishi nyumbani kwao eneo la Kariwa kata ya Longuo B Manispaa Moshi mkoani Kilimanjaro jana.(Picha na Salome Kitomari,Moshi)

Vilio Simazi na majozi vilitawala jana katika mazishi ya watoto watatu waliouwawa na mama yao mzazi, Benedicta Thadei (44) kwa kupigwa shoka kichwani na maeneo mengine ya miili yao.
Katika mazishi hayo ambayo yalivuta hisia na kusababisha majozi kwa kila aliyehudhuria wakati miili ya watoto hao ikiwasili nyumbani kwao majira ya saa 11;30 katika eneo la Kariwa kata ya longuo ‘B’ katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Miili ya watoto hao iliwasili nyumbani baada ya ibada na kufuatiwa na utoaji heshima saa 7:38 ambapo ibada ilianza.
Katika mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa pamoja na wabunge,zaidi ya wananchi 1500 kutoka Manispaa ya Moshi na maeneo mengine ya mkoa huu walihudhuria.
Patashika iliibuka baada ya Padri wa Kanisa la Kristo Mfalume, Jimbo Katoliki la Moshi ambaye aliongoza ibada, Reginald Spend, ambaye alitoa nafasi kwa wananchi kupita kwa mistari mitatu mitatu ili kutoa heshima kwenye miili ya marehemu.
Kila mwananchi alionyesha shauku ya kutaka kuona sura za mwisho za watoto hao, lakini zoezi hilo lilisitishwa baada ya kutaka kutokea vurugu kutokana na kila mwananchi kutaka kuona na kuvuruga utaratibu.
Akisaidiana na Padri Patrick Asanterabi, Padri Spend alisema ni vyema serikali ikafanya uchunguzi wa kina wa jambo hilo na kwamba kuna maswali mengi kwani kwa kawaida vichaa hupenda watoto wao na huwalea hadi wakue bila kuwadhuru.
Alisema maisha ya watoto hao yamekatishwa kikatili na kumshukuru baba wa marehemu kwa alijitahidi kutunza na kuwalea watoto na kwamba tukio hilo limemshtua sana kwani kwa miaka nane aliyokuwa Padri hajawahi kusikia tukio kama hilo.
Spend alisema ni fundisho kwa jamii na serikali kwa ujumla kuwa maadili na huruma ndani ya jamii imepungua na watu wamevaa roho za kikatili kuliko wanyama ambao wanatunza watoto wao.
Watoto waliouwawa ni Rose Thadei (12) ambaye alikuwa mlemavu wa viungo na akili, Noel Thadei (5) na Anthony Thadei aliyekuwa na miaka miwili na miezi minne Aprili 29 mwaka huu.




CHANZO: NIPASHE
 
Too much to take in! It is hurting, hurting binadamu wenzangu. Ila tu, tusiamini vichaa ni vema wapelekwe vituo vya vichaa mpaka wathibitike ni wazima kiakili.
 
Kweli yesu rudi haraka huyu mama alinishangaza sana kuwa na ujasiri mkubwa wa kuua watoto aliozaa mwenyewe ..
 
Dah.....!!!! Please help Us God Almighty, We are getting worse day by day.

RIP Madogo
 
Back
Top Bottom