Siloam church

dopeboy

Senior Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
121
Reaction score
100
Naomba nieleweshwe mambo yafuatayo nipate kujifunza;

Kalenda yao inatoka wapi? Kwanini wanabadili majina? Yule Nabii wao alitoa wapi mamlaka? Je kubadili cover kwenye bibilia kunabadili nini? Ile picha ya nabii akipaa sijui mbona kama ni photoshop, nisaidieni hata video..
 
Shika neno mliyepewa neema kubwa..

Mbele yenu namleta kuhani Miaka 1000, huyu ndie aliyeteuliwa na Mjumbe wa mapenzi ya Mungu AD2 MUNGU wa majeshi mwezi mmoja kabla ya kutwaliwa, Mjumbe alimsimamisha madhabahuni mbele ya makuhani, wakuu wa njia na wakamilifu na kusema anamkabidhi kazi, amempa moyo wake nafsi yake, na Roho yake, na kuanzia leo huyu sio Elisha tena, bali ni Eliya, baada ya mwezi mmoja ndipo mjumbe akatwaliwa, na ishara zote zilionekana angani siku ya Adari 12, 3 wakati mjumbe wa mapenzi ya MUNGU ELIYA AD2 MUNGU WA MAJESHI akipaa kwenye sherehe maalumu ya kuhifadhi viungo vyake vya ufunuo katika mlima wake wa moto; mlima wa ukamilifu (Mapinga, Bagamoyo)..

Historia fupi ya Kuhani kiongozi Miaka 1000 ni hii; Kabla ya kutoka kwenye ulokole na kuingia Siloam Ministry International "The Pool of Siloam Church" kwenye wokovu wa kweli amewahi kuwa mchungaji katika makanisa ya kilokole na amehudhuria semina nyingi na pia ametembea nchi nyingi sana katika utumishi wake wa awali aliokuwa akitumika kama Sauli. Kuhusu Elimu ni msomi mwenye PHD, na alikuwa anafanya kazi katika ofisi ya Raisi enzi hizo akijulikana kwa jina la Rusumo.

Pamoja na hayo yote alikuwa bado hajapata amani na utoshelevu moyoni kwa kuwa alikuwa halitumikii kusudi la Mungu wa Kweli bali kusudi la mungu wa dunia hii katika makanisa ya kilokole. Siku moja akiwa katika kuhangaika na kumtafuta Mungu wa kweli ndipo alifanikiwa kukutana na AD2 Mjumbe wa Mapenzi ya Mungu ambae katika maongezi yao akagundua kuwa mjumbe ana hiari moja tu. Baada ya kuambatana na mjumbe Kuhani kiongozi Mika 1000 alifanikiwa kuiona ile nguvu na kupokea haja ya moyo wake ya kumtumikia Mungu wa kweli, ndipo alipoamua kuwa na maamuzi ya kuchagua Mungu na kuiacha dunia.

Tendo la kijasiri alilolifanya Kuhani Kiongozi Miaka 1000 ni kuandaa tafrija katika hoteli na kuwaita wafanya kazi wenzake, kisha akawaambia kuwa ameamua kuwa na hiari moja ya kumtumikia Mungu kwa hiyo yeye na kazi tena basi, baada ya maneno hayo akakusanya vyeti vyake vyote alivyohangaika kuvisomea hadi ulaya na kuvichana mbele yao kisha akavichoma moto, hatua hiyo ilitimiza lile andiko la Mtume Paulo analosema mambo yote ya ulimwengu huu aliyahesabu kama mavi, kwa uzuri aliouona ndani ya Kristo. Baada ya hapo Kuhani miaka alichagua kuwa karibu na Eliya AD2 MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU, na kumbe ni Mungu ndio alikuwa amemuandaa kuiendeleza misingi aliyoianzisha Eliya..

Namtakia kila la Kheri katika wajibu alio nao katika jukumu hilo aliloachiwa
 
Call them.
 
JIBU MASWALI. Kuhani mkuu Munuo au Rusumo alikuwa ikulu kama Tisi au Mpenda shina la mabaya yote duniani ?
EFATHA SASA !
 
Naona hakuna tofauti ya Mola wa Babu wa Samunge na kiongozi mkuu wa siloam aliyekufa na kwenda hukumuni(WAEBRANIA 9:27)
 
Je,Siloam sasa linaongozwa na mke wa aliyejiita nabii munuo au nani kiongozi mkuu baada ya kufa munuo ?
 
Hata mimi siwaelewi,wana watu wanajiita sijui kuhani miaka 1000,kuhani amani na upendo,watakatifu,na majina ya ajabu ajabu.juzi waliniletea gazeti lao ndani kuna kalenda ina majina ya miezi yasiyoeleweka.

Anyway ukristo una mambo mengi,hivyo kutoa fursa vikundi vingi vya kidini kuanzishwa wakiwa na tafsiri yao wakiwemo masalia,babu wa loliondo,davidians etc.

Nachoupendea ukristo ni jambo moja tu,unafundisha kwamba Yesu alifuta dhambi zote kwa hiyo hakuna dhambi duniani. Tuko huru kufanya chochote maana hakuna dhambi,Yesu alilipa garama ya tukifanyacho. Thank you Jesus.
 
Kuna wakati walikuwa wanagawa magazeti yao yaliyokuwa na habari ya kiongozi wao wanayesema alipaa. Wameweka picha, lakini lugha wanayotumia na tarehe licha ya kuwa kiswahili sikuweza kuelewa mtiririko wa maelezo yao. Wanatumia lugha kama aliyotumia dopeboy hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Tafadhari, wenye maswali juu ya yote yanayoendelea au kufanyika pale madhabahu kuu Siloam, mimi nawashauri muchukue hatua ya kwenda pale na kujionea wenyewe kwa macho yenu, pia kuuliza pale pale kwa usilolijua pale kuliko kujitafutia laana isiyo na sababu kwa maneno ya dharau juu kinachofanyika katika madhabahu ya MUNGU WA ELIYA. Maana imeandikwa, apandacho mtu ndicho atakacho vuna~ Galatia 6:7-8.
 
Galatia 6:7-8~ Msidanganyike, maana MUNGU adhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakacho vuna!
 

:confused2:
 
Hata Mimi sielewi kuhusu hili dhehebu mwenye taarifa atujuze
 
hapo hujaendana nao, wenzio hawaamini hicho wanasema alishindwa ndio maana alikufa, wanaamini nabii wao Eliya ndio alimuua shetani na kwa hiyo wanaomba kwa jina lake na ndio maana unaskia Mugnu wa Eliya wakati wewe una Mungu wa Bwana wetu Yesu alieyekuokoa...... kifupi sio Ukristo usije ingia ukasema umeomba kwa Mungu wa Yesu Kristo ni mungu wa Eliya. Nafikiri nikimsoma anasema aliyemrithi kwasasa ni Rusumo. Wakuu waumini wa Siloam wekeni wazi imani yenu hapa watu wajifunze nini mnaamini maana hiki ndio wengi tunaelewa kutokana na magazeti yenu.
 
Hiyo laana inatoka wapi..? Unakichaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…