Silaha iliyotumika kumuua Mwanasayansi wa Iran inaonekana ilitengenezwa Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Imethibiti Israel na Munafikina (MKO) wamehusika katika mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran

Nov 30, 2020 14:01 UTC

Utawala wa Kizayuni wa Israel na genge la kigaidi la Munafikina (MKO) wamehusika katika mauaji ya mwanasayansi mkubwa wa nyuklia wa Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Iran Press, mauaji ya kigaidi ya shahid Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mkubwa wa nyuklia na masuala ya ulinzi wa Iran yalifanywa kwa kutumia bunduki maalumu iliyokuwa ikongozwa kutokea mbali na ambayo ilikuwa imefungwa kwenye gari ya pikapu aina ya Nissan.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonukuliwa na Iran Press, silaha hiyo ilikuwa imefungwa kifaa maalumu cha mawasiliano ya kuongozea kutoka mbali kilichotengenezwa Israel, ambapo mara baada ya kunasa tawsira ya sura ya shahid Fakhrizadeh ilianza kufyatua risasi kumlenga mwanasayansi huyo wa nyuklia.

[https://media]Maziko ya shahid Mohsen Fakhrizadeh

Vilevile imebainika kuwa, kutumiwa gari ya pikapu kwa ajili ya shambulio la kigaidi dhidi ya shahid Mohsen Fakhrizadeh kulifanywa kwa malengo mawili, ambayo ni kuishambulia timu ya walinzi wa mwanasayansi huyo na pia kuteketeza kifaa hicho cha kuongezea shambulio kutokea mbali ili kupoteza kikamilifu ushahidi wa hujuma hiyo, hata hivyo mabaki ya silaha yaliyopatikana yameonyesha kuwa silaha silaha na kifaa hicho vimetengenezwa Israel.

Ripota wa shirika la habari la Iran Press ameeleza kwamba, nyaraka za kuaminika zilizopatikana kuhusiana na mauaji ya Profesa Mohsen Fakhrizadeh nazo pia zimethibitisha kuwa, shirika la intelijensia la utawala wa Israel na genge la kigaidi la Munafikina (MKO) yamehusika katika mauaji hayo.

[https://media]Jeneza lililobeba mwili wa shahid Mohsen Fakhrizadeh

Mohsen Fakhrizadeh, Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu wa Wizara ya Ulinzi ya Iran aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi lililofanywa Ijumaa ya tarehe 27 Novemba katika eneo la Absard, Damavand katika mji mkuu Tehran.../

4bvf00dd341d021rxo3_800C450.jpeg
4bvfa59c1931d41rxo5_800C450.jpeg
 
Duh naona damu zitamwagika hapa siyo kitoto yan Sera ya kill them all ndo itafuatia
 
Back
Top Bottom