Silaha aina ya SMG na risasi 30 vyaokotwa kichakani

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945

Kibaha. Silaha ya kivita aina ya SMG na risasi 30 mali ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani vimekutwa vimefichwa kwenye kichaka jirani na Mto Kitame katika Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Silaha hiyo inadaiwa iliibwa kwenye Geti la Gama saa tisa usiku Desemba 24, mwaka jana wakati askari wa hifadhi hiyo, Jackson Shirima (23) akiwa kazini.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventura Mushongi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya askari huyo kutoka lindo getini hapo na kujipumzisha kwenye moja ya mahema akiwa na silaha hiyo.

“Askari huyu alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana, hivyo alitoka na silaha akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi ndipo ilipoibwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi,” alisema.

"Huyu askari alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana zamu ya ulinzi hivyo alitoka na silaha yake akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi na ndipo ilipoibiwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi hiyo,” alisema.

Mushongi alibainisha kuwa baada ya wizi huo, askari kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) walianza msako na kupitia taarifa ya msamaria mwema walimkamata mtuhumiwa huyo, mkazi wa Tegeta Kibaoni ambaye alikwenda kuonyesha alipokuwa ameificha kichakani ikiwa na risasi 30.

Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk James Wakibara alisema wameshtushwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea na kwamba, zaidi ni baada ya kukuta mtuhumiwa huyo aliwahi kuwa mtumishi wao na aliacha kazi miezi kadhaa iliyopita yeye mwenyewe.

Dk Wakibara alilishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano lilioutoa toka siku ilipoibiwa silaha hiyo hadi ilipopatikana.
 
Ilishawahi tokea kuna jamaa angu alinunuaga smg kongo akaja nayo bongo kipindi flani cha tibaigana. sasa kwenye kupiga bit la afande tibaigana jamaa angu akaitupa. ilikuja kuokotwaga porini kule yalipotupwaga viungo vya binadamu na chuo kikuu cha (jina limenitoka)
 
Ilishawahi tokea kuna jamaa angu alinunuaga smg kongo akaja nayo bongo kipindi flani cha tibaigana. sasa kwenye kupiga bit la afande tibaigana jamaa angu akaitupa. ilikuja kuokotwaga porini kule yalipotupwaga viungo vya binadamu na chuo kikuu cha (jina limenitoka)

daah huyo jamaa atakua amekasirishwa ni kitu gani hasa ,kwanza wadai alikua mtumishi wao na aliacha kazi mwenyewe duuh
 
Back
Top Bottom