kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Kabla ya kuja dini za kigeni kutoka ng'ambo watu, familia, koo na himaya zetu zilikua zinajua kuwa kuna Mungu, zinamjua Mungu wao na ziliwasiliana na Mungu wao kwa matambiko. Kwanjia hii na Mungu wao alikuwa akiwajibu na kuwatimizia matamanio na mahitaji yao kama walivyoomba. Kwanjia ya matambiko walimudu kuvivusha salama vizao miaka karne na karne dhidi ya magonjwa, maadui, na majanga mbalimbali hadi walipokutwa na dini za kuletwa kutoka ng'ambo.
Sifa mahususi za tambiko ni kuwalenga watu maalumu, kufanyikia sehemu na wakati maalumu na kuongozwa na watu maalum wanaofahamu namna tambiko hilo linavyonyika ili kukidhi vigezo vilivyokusudiwa. Utaratibu huo utabaki hivyo milele na milele hata pale viongozi na vizazi vitakapokuwa vinabadilikika.
Ni wazo langu hata kama la kijinga tu
Sehemu za kufanyikia matambiko hayo zilikuwa maalum na kujulikana kwa watu wote. Mara nyingi ilikuwa kwenye mapango, majiti makubwa, msitu mnene, milima mirefu, mawe makubwa, mto, ziwa, chemshem n.k ambako kila mtu alikuwa anapaheshimu na kupapa hadhi yake.
Sikukuu zetu za kitaifa pia zina historia ya mfumo huo wa tambiko, kwani ndipo mahali ambapo watanzania wanabaki kuwa watanzania na Tanzania (Tanganyika/Zanzibar) inabaki kuwa tanzania miongoni mwa mataifa ya dunia. Dunia nzima inafanya hivyo hata kule Uingereza bado wamebaki na matambiko yako hadi leo chini ya Malkia/Mfalme wao. Waingereza hadi leo wanafahamu ni lini, wapi na nani ataongoza sherehe zao.
Hivyo sikukuu hizi za kitaifa ni utambulisho wa taifa letu kwetu na mbele za Mungu na mataifa mengine, hivyo hazifai kubadilishwa, kuahirishwa, kuingizwa maswala ya kisiasa, zama, kidini, kikabila wala ukanda kwa mtu kupenda. Nilazima iwe siku za kulitafakari taifa letu kwa kina na kumuomba Mungu atujalie yale ambayo tunayataka kama taifa na atuondolee yale yote tusiyoyataka kama taifa. Ni sehemu ambayo vizazi vipya vinafahamishwa kuhusu nchi yao ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea.
Hitimisho: Kila kitu kina historia yake, hivyo hata Sherehe za kitaifa hazina budi kuadhimishwa kwa mujibu wa historia yake ilivyo kwa kuzingatia muda, mahali na taratibu za kuziazimisha, hapo ndipo zitakapoleta maana.