Sikubaliani kabisa na Kampeni ya Black Lives Matter inayoendelea especially kwenye league ya Uingereza its Better iwe All Lives Mater

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
2,994
2,000
Binafsi hainingii akili... yaani ni kama vile unafamya kampeni ya Kutoweka kwa Tembo au Sokwe watu, so mnapiga kampeni kuwa tuwalinde wasipote.

Why not
ALL LIVES MATTER.. ALL RACE MATTERS ...KULIKO BLACK LIVES MATTER ..

Sijui kuna mtu ananielewa kwenye hili?
 

S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
650
500
Ndugu yangu, Hivi wewe unatambua yanaoendela kweli? All Lives Matter kama weupe watawatendea haki sawa Weusi ndio msemo wako utapokuwa na maana- All lives matter...

kwa wazungu- wakitunga sheria na kutaka kujua inafanya kazi kiasi gani basi majaribu kwa sheria mpya hujaribiwa weusi. Ukipelekwa mahakani na kukutwa na hatia, kosa la mweusi atafungwa miaka kibao, sasa linanganisha na mweupe kwa kosa hilo hilo.

Mtu Mweusi hana thamani si tu kwa watu weupe lakini pia kwa weusi wenyewe kwa wenyewe- angalia polisi huko nyumbani wanavyowauwa majambazi , angalia watu wenye hasira kali wanavyo- wachoma vibaka, angalia watu wasio julikana wavyoteka ndugu zetu kwa kiu ya madaraka.

hata wazungu wanatuangalia tunavyotendeana na kujisemea- ikiwa wao kwa wao wanatendea hivi, hata sisi (weupe) tukiwatendea vibaya , who cares?

hapo ndio pa kuanzia- tujijali sisi kwanza na ndo tujue all lives matter
 

Chang’oe

Senior Member
Jun 16, 2013
140
500
Ishu iko hivi

Kuna A,B,C,D mpaka Z

Assume hizo herufi ndio asili za watu

Herufi zote zinaheshimiwa na kila mojawapo ya nyenzie kwakuwa wanaamini asili yao ni bora zaidi na kwamba wana haki ya msingi lakini hii B haieshimiwi. Popote ilipo nje ya taifa lake inatengwa na kudharauliwa ikiwa pamoja na kusitishwa maisha yake bila kujali (kupotezewa haki ya msingi anayotakiwa kuipata pindi anapozaliwa).

Je "B" anapotaka kudai haki yake kwa hizo herufi nyingine atasema maisha ya herufi zote ni muhimu au atasema Maisha yangu pia ni muhimu?

Ikumbukwe, hadai haki za watu wengine kwakuwa tayari wao wanapeana haki hizo, ila anadai haki yake ambayo herufi nyingine zote hazimpi.

Kiufupi tu ni kwamba, huwezi kuandamana ukisema wote tunahitaji chakula wakati umelala njaa pekeyako wenzio wamekula.

#Anza upya kujielewesha juu ya hiyo movement mzee ili kuelewa maana halisi.

#Black Lives Matter
 

BinSalum7

JF-Expert Member
Jan 26, 2019
246
500
Binafsi hainingii akili ... yaani ni kama vile unafamya kampeni ya Kutoweka kwa Tembo au Sokwe watu, so mnapiga kampeni kuwa tuwalinde wasipote.

Why not ..
ALL LIVES MATTER.. ALL RACE MATTERS ...KULIKO BLACK LIVES MATTER ..

Sijui kuna mtu ananielewa kwenye hili. ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mie nimekuelewa mkuu
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
6,128
2,000
Ishu iko hivi

Kuna A,B,C,D mpaka Z

Assume hizo herufi ndio asili za watu

Herufi zote zinaheshimiwa na kila mojawapo ya nyenzie kwakuwa wanaamini asili yao ni bora zaidi na kwamba wana haki ya msingi lakini hii B haieshimiwi.Popote ilipo nje ya taifa lake inatengwa na kudharauliwa ikiwa pamoja na kusitishwa maisha yake bila kujali (kupotezewa haki ya msingi anayotakiwa kuipata pindi anapozaliwa).

Je "B" anapotaka kudai haki yake kwa hizo herufi nyingine atasema maisha ya herufi zote ni muhimu au atasema Maisha yangu pia ni muhimu?...

Hicho ulichotetea kingekuwa hivi; "Black lives matter too" hapo ingalikuwa sawa, lakini unaposema Black lives matter, implication yake ni kwamba kuna; some lives which do not matter.

Watu wamekaa kimya tu kama sympathetic kutokana na kifo cha G, Floyd, isingekuws busara watu watoke na wahoji juu muundo wa slogan; Black lives matter wakati ambapo watu walikuwa na majonzi, huzuni na hata hasira juu ya hilo tukio.

"All lives matter" is the best non racist slogan to be adopted.
 

Pacbig

JF-Expert Member
Oct 15, 2017
552
1,000
Shida kubwa ya kwanza ya mtu mweusi ni inferiority.

Ninaamini kama yule jamaa aliyenyongwa kwa miguu kama angekuwa mzungu na askari akawa mweusi, basi hakuna mzungu ambaye angefikiria ni ubaguzi ila Wangeona ni ujinga wa huyo askari mweusi.

Lakini kwa sababu mweusi ana inferiority complex ndio maana anaandamana as if Wazungu wote ndio wamemuua mweusi mwenzao.

Kampeni ya black lives matter inamudhoofisha mtu mweusi aonekane mtu wa kuonewa huruma hivi ilitakiwa iwe #all lives matter
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
6,128
2,000
Binafsi hainingii akili ... yaani ni kama vile unafamya kampeni ya Kutoweka kwa Tembo au Sokwe watu, so mnapiga kampeni kuwa tuwalinde wasipote.

Why not ..
ALL LIVES MATTER.. ALL RACE MATTERS ...KULIKO BLACK LIVES MATTER ..

Sijui kuna mtu ananielewa kwenye hili. ?

Sent using Jamii Forums mobile app
In this case it should be; all lives matter, whether be it black, yellow, white, blue etc.

By the Slogan; " black lives matter"- it implies the rest lives do not matter and this notion ushers in new form of racism making the black superior over the rest colours.

That is my take.

Naungana mkono nawe.
 

Gwappo Mwakatobe

Senior Member
Nov 22, 2019
142
250
Uko sahihi kabisa, la sivyo unakuwa ubaguzi uleule. Ikumbukwe kuwa si kila mzungu au asiye mwafrika-mweusi ni mbaguzi.

Aidha, si kila mwafrika humjali mwenzake. Ubaguzi au ukatili ni tabia kutokana na malezi au kukosa utu kwa yeyote yule pasina kujali rangi yake. Wapo weusi wanaowabagua au kuwaua weusi/ Waafrika wenzao! Na wapo wazungu wanaowatetea weusi, na kinyume chake.

Kuna weusi waliwauza utumwani weusi wenzao, kuna weusi walipinga utumwa na kutawaliwa na wazungu kama akina Mkwawa, Kinjekitile, nk. Kuna wazungu walipinga biashara ya utumwa na ukoloni uliofanywa na wazungu wenzao, kama akina Abraham Lincoln.

Naunga mkono "ALL LIVES MATTER" AU "ALL PEOPLE MATTER!" TUWAJALI WATU WOTE, TUJALIANE WATU WOTE!!!
 

Gwappo Mwakatobe

Senior Member
Nov 22, 2019
142
250
Umewaza kwa busara na hekima sana!
Hicho ulichotetea kingekuwa hivi; "Black lives matter too" hapo ingalikuwa sawa, lakini unaposema Black lives matter, implication yake ni kwamba kuna; some lives which do not matter.

Watu wamekaa kimya tu kama sympathetic kutokana na kifo cha G, Floyd, isingekuws busara watu watoke na wahoji juu muundo wa slogan; Black lives matter wakati ambapo watu walikuwa na majonzi, huzuni na hata hasira juu ya hilo tukio.

"All lives matter" is the best non racist slogan to be adopted.
 

Gwappo Mwakatobe

Senior Member
Nov 22, 2019
142
250
Naam, umesema ukweli mtupu na wenye uungwana. La sivyo ni ubaguzi uleule na kujidhalilisha!
Shida kubwa ya kwanza ya mtu mweusi ni inferiority.

Ninaamini kama yule jamaa aliyenyongwa kwa miguu kama angekuwa mzungu na askari akawa mweusi, basi hakuna mzungu ambaye angefikiria ni ubaguzi ila Wangeona ni ujinga wa huyo askari mweusi.

Lakini kwa sababu mweusi ana inferiority complex ndio maana anaandamana as if wazungu wote ndio wamemuua mweusi mwenzao.

Kampeni ya black lives matter inamudhoofisha mtu mweusi aonekane mtu wa kuonewa huruma hivi ilitakiwa iwe #all lives matter
 

orturoo

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
1,207
2,000
What I can say ni "black lives matter" tutazame kwa muktadha wa kiharakati na msingi wa kimapinduzi ,blm wanapambania haki ya Mwafrika ambae amekua akibaguliwa toka enzi, hivyo hujawahi kusikia mzungu akidai ukombozi huo, yeye anao teari huwezipigania haki ambayo teari umeshaitwaha.
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
6,868
2,000
Kwan wahanga ni wakina nani kati ya hayo makundi mawili?
Mleta thread hajaelewa kabisa, labda mpaka asome historia tangu za utumwa, kunyanyaswa kwa watu weusi huko, kusingiziwa kesi, kusimamishwa na polisi na kusachiwa kukicha tena bila sababu, kunyimwa kazi kisa rangi nyeusi, kuambiwa lazima wakae nyuma ya basi na siyo mbele sababu ni weusi, kunyongwa hasa kule Alabama kisa weusi,

kunyanyaswa madukani, supermarkets, kila sehemu, kupigwa risasi na polisi kukicha, polisi kutumia nguvu sana katika kuwakamata watu weusi, kujaa kwa watu weusi magerezani.

Labda kwa kuweka yote haya na takwimu kuthibitisha yatamfanya mtoa mada afikirie tena...
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,498
2,000
Ndugu yangu, Hivi wewe unatambua yanaoendela kweli? All Lives Matter kama weupe watawatendea haki sawa Weusi ndio msemo wako utapokuwa na maana- All lives matter...

kwa wazungu- wakitunga sheria na kutaka kujua inafanya kazi kiasi gani basi majaribu kwa sheria mpya hujaribiwa weusi. Ukipelekwa mahakani na kukutwa na hatia, kosa la mweusi atafungwa miaka kibao, sasa linanganisha na mweupe kwa kosa hilo hilo...
Tatizo kubwa Waswahili na Waafrika kwa ujumla tunalalamika tupendwe na jamii nyingine.

Tujiulize umeshaona Mmarekani, Mzungu, Mchina , mTuruki, MJapani, mhindi akilia lia ktk mitandao, radio,magazeti au media platform kibao kwa Kuwa hawapendwi au kubaguliwa n.k

Sababu ni kuwa jamii hizo nyingine wanajua ni hulka ya binadamu kupenda, kujali na kukiweka kizazi, jamii na uTaifa wao mbele. Ndiyo watafanya biashara na jamii zingine lakini ukweli wanajua binadamu ndiyo tulivyo hatuwezi kuwaweka mbele jamii zingine, dini zingine, mila zingine zaidi ya za kwao.

Ila sisi watu weusi waAfrika tunalilia tupendwe, tunatukuza dini, mila, desturi , simulizi za wengine tukidhani watatupenda, kututukuza na kutukubali kama wao.

Hilo ndipo tatizo la Waafrika kushindwa kutambua silka na hulka ya jamii za binadamu. Ingia Youtube, Facebook, Twitter, Instagram kama utaona jamii zingine zinalilia kupendwa.

Tuamke tujipende na kukubali hilo la kujipendelea tufanye biashara tuwagonge tupate faida, tujifunze elimu ya kujisaidia hata kama tutachukua elimu inayotufaa toka kwa wengine lakini dhima tuchukue yale yatakayo nufaisha jamii zetu na tusahau kuwa ipo siku tutapendwa maana wenzetu pia wamekubali hawatapendwa hivyo wanajifanyia yao bila kulialia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom