Sikubali

Sikubali

kabiriga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
1,163
Reaction score
1,213
Miaka mitano iliyopita nilikuwa na mahusiano na binti mmoja!katika utafutaji na hali ya maisha niliamua kwenda kujiendeleza kimasomo,sikumuaga ingawa baadae tuliendelea kuwasiliana kwa njia ya simu.Kwa muda wote wa masomo yangu (miaka 3) sikurudi nyumbani baada ya kuhitimu masomo yangu nilienda kutafuta kazi mkoa mwingine yaani mkoa tofauti na ule nilikokuwa nasoma nikapata kibarua na kufanya kazi huko kwa miaka miwili.Baada ya kibarua changu kukoma nikarudi nyumbani ndipo nikakutana na huyo bibie kwa mara nyingine tena,alipo pata habari kuwa nimerudi alinipigia simu akiomba tukutane.tukakutana kwenye mgahawa mmoja katikati ya maongezi yetu aliniuliza kama mapenzi yetu yanaendelea au yalikoma? mimi nili mjibu kuwa ni muda tumekuwa hatupo pamoja kwa hiyo si busara kuendeleza mapenzi yetu na kibaya zaidi nilishakuwa na mtu mwingine.ndipo alipo toa kauli hii tata ya "MIMI SIKUBALI nilisha kupenda wewe na nitafanya lolote liwalo maadamu niwe na wewe" kisha akaondoka.Natafakari sana kauli yake na nimekosa la kufanya ndipo nikawageukieni wanajamvi .ushauri tafadhali
 
la kwako hilo mzee.
Kazi ni kwako.
Tehe tehe tehe
Mkwara tu huo jeba. Hata nyau anao.
Acha uoga
 
hini ni sikubari au Sikubali!!!!!!

nikipiga haraka haraka naona kama ni miaka 5 imepita......

inawezekana alikuwa amekaa anakusubiria miaka yote hiyo ndo maana kapanick........
 
hasira za wanawake tu! kikubwa atakachofanya atamtafuta mpenzio na kumweka mikwara!!!!
 
atakuwa anataka kukuloga...................mweeeh!!!!!!!!
 
Miaka mitano iliyopita nilikuwa na mahusiano na binti mmoja!katika utafutaji na hali ya maisha niliamua kwenda kujiendeleza kimasomo,sikumuaga ingawa baadae tuliendelea kuwasiliana kwanjia ya simu.

Ulipokuwa unawasiliana naye maongezi yenu yalikuwaje?

Ni kama mtu na mpenzi wake au kama kaka na dada yake?

Kuna mahali nahisi umelikoroga ila unajishaua tu hapa jamvini ili uonekane mtu mwema....
 
atakuwa anataka kukuloga...................mweeeh!!!!!!!!

atamuweka kwenye kichupa kisha atamzika kaburini au atakirusha kwenye gari!!Eti mleta mada anaomba ushauri au?
 
kwa nin ukumuacha mapema!wakat mnawasiliana we nawe umeyataka kumpotezea mda dada wa watu,
 
atamuweka kwenye kichupa kisha atamzika kaburini au atakirusha kwenye gari!!Eti mleta mada anaomba ushauri au?

mwenzangu hata mimi sijaelewa. labda anataka kujua maana ya neno "sikubari" ambalo sina uhakika kama lipo katika kamusi ya kiswahili
 
Miaka mitano iliyopita nilikuwa na mahusiano na binti mmoja!katika utafutaji na hali ya maisha niliamua kwenda kujiendeleza kimasomo,sikumuaga ingawa baadae tuliendelea kuwasiliana kwa njia ya simu.Kwa muda wote wa masomo yangu (miaka 3) sikurudi nyumbani baada ya kuhitimu masomo yangu nilienda kutafuta kazi mkoa mwingine yaani mkoa tofauti na ule nilikokuwa nasoma nikapata kibarua na kufanya kazi huko kwa miaka miwili.Baada ya kibarua changu kukoma nikarudi nyumbani ndipo nikakutana na huyo bibie kwa mara nyingine tena,alipo pata habari kuwa nimerudi alinipigia simu akiomba tukutane.tukakutana kwenye mgahawa mmoja katikati ya maongezi yetu aliniuliza kama mapenzi yetu yanaendelea au yalikoma? mimi nili mjibu kuwa ni muda tumekuwa hatupo pamoja kwa hiyo si busara kuendeleza mapenzi yetu na kibaya zaidi nilishakuwa na mtu mwingine.ndipo alipo toa kauli hii tata ya "MIMI SIKUBALI nilisha kupenda wewe na nitafanya lolote liwalo maadamu niwe na wewe" kisha akaondoka.Natafakari sana kauli yake na nimekosa la kufanya ndipo nikawageukieni wanajamvi .ushauri tafadhali

Uliupokuwa unaongea nae kwenye simu ulimwambia kuwa mapenzi yenu basi asonge mbele? hapo kwenye bold kwa nini hukumwaga? acha kuchezea hisia zake wanaume kama nyie mnalishwaga sumu bila kujijua. Na uanaume wote unashindwa kuwa wazi kwa mpenzi wako.
 
sasa kama ulimuahidi hutakua na mwingine mwenzio kakusubiri siku zote huoni umezingua
 
Back
Top Bottom