Gabraison jr
Member
- Sep 7, 2011
- 21
- 1
Mambo hubadilika kila wakati,2015 inawezekana kabisa.tuache ushabiki CCM itang'ang'ania kiti cha urais mwaka 2015 labda waweke mtu ambaye hawezi kabisa kupigiwa kura na kuiba hiyo ni mlima wa kilimanjaro, la sivyo watashinda kwa nguvu yao ya dola..cha muhimu tujitokeze vijana kugombea hivi viti vya ubunge majimboni mwetu tuwape upinzani viti vya kutosha na kazi yetu ionekane kwa wananchi bungeni. hii italeta ushindi 2020
yah hilo halina tatzo kama CDM wakiwaelimisha na kuwahamasisha watanzania wa mikoa ya pembezon hususan Ruvuma ccm itafika kikomoMambo hubadilika kila wakati,2015 inawezekana kabisa.
CCM itakufa hata kabla ya 2015
Chama cha magamba kimepoteza mvuto wake mbele ya watanzania waliowengi kutokana na sera yake ya kukumbatia mafisad na kutotekeleza waliyoahid wengi wautabiri mwaka 2015 ccm haitakuwa tena chama tawala bali ni chama cha upinzani
Tudai tume huru ya uchaguzi...hizi "stori" nyengine zitajishughulikia zenyewe.
Bila tume huru ya uchaguzi na elimu ya uraia kwa wapiga kura....kiondoa CCM madarakani ni lazima watu wengi watatoka mhanga.
Kikwete kama ni msomaji wa wakati basi angehakikisha kabla ya kumaliza muhula wake kuwa anahakikisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umejadiliwa kwa uwazi...hili litapelekea kuandika katiba ambayo itafaa kupewa jina la Katiba ya Tanzania....pia kuhakikisha Tz inapata Tume huru ya uchaguzi kama anapendelea kuona TZ inabaki kisiwa cha "amani na utulivu".
Haya yasipofanyika uwezekano wa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa wataka uhuru zitaibuliwa na itapelekea kupata NTC hapa TZ na vifo kuongezeka. Hivi vifo vya ajali za barabarani na ukosefu wa huduma za afya vinatutosha..hatustahiki kupata vifo vya ziada kwa kulinda kikundi cha siasa au wanasiasa kuendelea kutawala TZ bila ya tija kwa wananchi.
Ni vyema vyama vya upinzani kupanga mkakati wa pamoja ili kudai tume huru . Time waits for no one..2015 hiyo hapo imefika!!!
Tusitegemee matokeo tofauti ya uchaguzi chini ya tume hii iliyopo. Tusijidanganye!
Tatizo viongozi wa juu waCCM wameshindwa kubainni adui wao.
Kwa mawazo yao wanafikiri adui yao mkubwa ni CDM.
Adui yao mkubwa ni kushindwa kushughurikia matatizo sugu ya wananchi kama vile:
1.Rushwa
2.Ufisadi
3.Kuongezeka kwa ufa kati ya maskini na matajiri na mengine mengi.
"CCM will die on its own success"