Siku ya wanawake duniani

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,835
Tukiwa tunasheherekea siku ya wanawake duniani tusiigeuze ikawa siku ya starehe kama ilivyo sikukuu zingine bali tupaze sauti zetu zisikike kila sehemu kuna wanawake wananyanyasika ndani ya ndoa, katika familia zao, kazini kwao, mitaani hivyo ifike mahali tuseme IMETOSHA na mwanamke apate uhuru wake.

Mfumo dume unawakandamiza wanawake hivyo tupige marufuku, tusiishie mijini kupiga kelele, matukio ya ajabu yapo vijijini hivyo sauti zetu ziwafikie huko ndani ndani na kwa pamoja tukaipate Tanzania tuitakayo isiyokuwa na ukandamizaji na unyanyasaji wa aina yoyote ile ya mwanamke.

Kampuni ya TAECO inaungana na wanaharakati wote kila kona kutetea haki za wanawake wote.

Happy women's day all

Mtenga Gerald
TAECO LTD
TANZANIA
 
Takwimu zilizotolewa recently zinaonyesha kwa sasa kuna asilimia kubwa ya wanaume wanaonyanyaswa na wanawake wao kuliko wanawake wanaonyanyaswa na wanaume....Wanawake wamekuwa-empowered hadi imepitiliza sasa....
 
Takwimu zilizotolewa recently zinaonyesha kwa sasa kuna asilimia kubwa ya wanaume wanaonyanyaswa na wanawake wao kuliko wanawake wanaonyanyaswa na wanaume....Wanawake wamekuwa-empowered hadi imepitiliza sasa....
Takwimu zipi mkuu?? Tusiongee theory naomba uweke trusted source ya hizo taarifa
 
Tatizo hii haki sawa wanaume wanaichukulia ndivo sivo. Acha nikupeni stori moja inayonihusu kuhusu hii haki sawa. Mama yangu kwao walizaliwa 11 na yeye ndo wa kwanza. wadogo zake wa kiume wote walipelekwa shule ispokuwa yeye kwa sababu ni mwanamke akawa anaenda shambani na mama yake na kuwapikia ndugu zake wakirudi shule wakute chakula tayari. Mjombaake mmoja alikuwa akiishi nje siku alirudi kakuta ile hali pale nyumbani. alichofanya alimchukua Mama tena kwa kulazimisha kaondoka nae kaja kumsomesha. Ivi ninaoongea huyu mama ambaye babaake alikataa kumpeleka shule kisa mwanamke ndo anaewatunza wazazi wake. yeye ndo kila kitu. wale wanaume waliopewa kipaombele cha kwenda shule hakuna hata mmoja anaejishugulisha. Natamani wanaume wotee mnaokashifu wanawake kwa sababu ya haki sawa mngekuwa angalau na akili kama yulee mjomba aliyeitekeleza hiyo na mafanikio yake tunayaona sasa kuliko kuanza kubeza bila hata kujiuliza. Mnaongea tu kwasababu ni wanaume mjifurahishe. Ivi mnajua chanzo wanawake kutafuta haki zao? tafuteni kwanza data ndo mje hapa muanze kuwaponda.
 
Ushuhuda wako ndugu inaonekana ni wa uongo na umejengwa kwa misingi ya chuki, ni kwamba miaka ya nyuma ya 1980 mwamko wa kusoma ulikuwa mdogo sana na kulikuwa na ushindani mkubwa wa kupata fursa.

Na wanawake wengi ari ya kusoma hawakuwa nayo na hii ilifanya kuliko baba amsomeshe mtu badala yake apate hasara bora akamsomeshe mtu mabaye anamwelekeo. Jambo hili limepelekea wanawake wenginwalioshindwa kusoma kujitetea kama unavyodai wewe.

NB; napinga kwa nguvu zote vitendo vyovyote vya kinyanyasaji hasa kwa wanawake
 
Back
Top Bottom