Siku ya leo 14/10/2015 ni mwiba kwa Lowassa

Siku ya leo 14/10/2015 ni mwiba kwa Lowassa

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
8,381
Reaction score
11,827
Siku kama ya Leo ni siku inayokumbukwa na watanzania kwa kupotelewa na mzalendo wa kweli..Baba wa Taifa JKN.
Siku hii pia inatumika katika propganda za kisiasa.

Mimi niseme kidogo tu, kwa mtu bepari kama Lowassa hataki hata kusikia jina hili masikioni mwake. Anajua alichokwa anakisema Nyerere kuhusu utajili wake.
Alijitwalia mali na kuwaacha watanzania walio wengi wakiwa masikini bila huruma wakiwemo na watu wa Monduli

Ila uzuri tu nikwamba hizo pesa amezileta kwenye kampeni tunazila na Kura hapati, ili watawala wengine wa namna hii wasiwe wanachukua hela za serikali
Nawaomba watanzania wenye uzalendo wa kweli na nchi hii wasithubutu hata kidogo kumpatia kura huyu jamaa.

Tusijifanye tumepoteza kumbukumbu kuhusu huyu jamaa kisa kajificha kwenye kichaka cha UKIWA, Asije akawa kama katuloga ili tupoteze kumbukumbuku.
Wanao Muunga mkono wengi wao ni masilahi binafsi tu
Magufuli is for Public Interest ndo maana hakuna cha Timu Magufuli.
Asanteni
 
Ngumu kutofautisha it masaki na ccm kindakindaki wote mna mabandiko ya kipuuzi, eti lowassa hataki kusikia jina la nyerere. Ungejiongeza kidogo tu ungejua toka atoke ccm hadi sasa lowassa anatumia misemo ya nyerere. Pole yako gamba usiyejielewa
 
uvccm unategemea kuna mtu anaye weza kukuelewa!
 
Munaweweseka tu . ila yeye ukweli anaujua. Nyerere alimkataa huyu jamaa tangu alipoona ni Bepari
 
Munaweweseka tu . ila yeye ukweli anaujua. Nyerere alimkataa huyu jamaa tangu alipoona ni Bepari

Kwa kumuogopa kumfunga lowasa jela awamu zote NNE, kwa kusubiri nyerere afe ndio mmpe uwaziri mkuu...aya ndio yananifanya nimpe lowasa kura yangu!!
 
Munaweweseka tu . ila yeye ukweli anaujua. Nyerere alimkataa huyu jamaa tangu alipoona ni Bepari

Lowasa bepari tangu enzi za Mwalimu na je hao mabepari wenu wa juzi?? miaka 10 ya Kikwete imemufanya mwanae Bilionea mbona husemi, akina Chenge na vicent huwaoni???
 
Ni kinyume chake, hii ndiyo siku hasa ambayo Lowassa na sisi wana UKAWA wote, tunapozidi kukumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere,"WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO, WASIPOYAPATA CCM, WATAYATAFUTA NJE YA CCM". Imeshindikana kupata mabadiliko ndani ya CCM, na ndiyo maana tuko na Lowassa nje ya CCM. Tumechoka na ahadi za CCM, miaka 54, bado tu wanatoa ahadi!!!!!!! HATUDANGANYIKI, Rais wetu ni Lowassaaaaaaaaaaaa!!!!!!!
 
Lowasa bepari tangu enzi za Mwalimu na je hao mabepari wenu wa juzi?? miaka 10 ya Kikwete imemufanya mwanae Bilionea mbona husemi, akina Chenge na vicent huwaoni???

Mkuu tofautisha kati ya Raia, Mbunge na Rais. Rais ndo Dila ya taifa. Wala usitumie gia ya Chenge kumtakasa Lowasa.Kila mtu anahukumiwa kivyake
 
Siku hii ni mwiba kwa watanzania aliowachia dhamana ya kuongoza nchi.
Dhambi kubwa waliyofanya ni kupoteza maana halisi ya uhuru wa mwafrika.
Kumbuka wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais wahindi walienda na mapesa kuhonga wajumbe kule Dodoma.
Nyerere angekuwepo, upuuzi huo ungevumiliwa? Mbaya zaidi hakuna hatua dhahiri zilizochukuliwa kwa uzito unaostahili ili iwe fundisho kwa sasa na vizazi vijavyo.
Utu na uhuru aliopigania unalindwa?
Masuala ya utaifa hayatakiwi kujadiliwa kwa ushabiki wa kipumbavu!
 
Ni kinyume chake, hii ndiyo siku hasa ambayo Lowassa na sisi wana UKAWA wote, tunapozidi kukumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere,"WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO, WASIPOYAPATA CCM, WATAYATAFUTA NJE YA CCM". Imeshindikana kupata mabadiliko ndani ya CCM, na ndiyo maana tuko na Lowassa nje ya CCM. Tumechoka na ahadi za CCM, miaka 54, bado tu wanatoa ahadi!!!!!!! HATUDANGANYIKI, Rais wetu ni Lowassaaaaaaaaaaaa!!!!!!!

Itakuwa ngumu sana kukuelimisha mtu kama wewe. Ila subiri 25.10.2015 utaelewa. Mtu aliyetumia pesa nyingi kwa zaidi ya miaka mitatu kutafuta urais eti ndo anataka mabadiliko. Mungu alimuumbua dodoma pamoja na kununua wahusika wote lakini alifeli, atafeli tena na sasa
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana.Kwa comments zako hizi inaelekea wewe ni mwanachama wa CCM.Kinachonishangaza ni kwamba unajua fika mafisadi na wapiga madili kama akina Kinana CCM ndio nyumbani kwao.Sasa kwa nini usianze kutuhumu mafisadi walioko CCM na badala yake unanyooshea kidole walioko nje ya CCM tu.Unajua kwa mfano kwamba ESCROW lilikuwa dili la CCM na madili mengine mengi.Be impartial my friend.Unapomnyoshea mwenzio kidole kumbuka vidole vinne vimekuelekea wewe.
Siku kama ya Leo ni siku inayokumbukwa na watanzania kwa kupotelewa na mzalendo wa kweli..Baba wa Taifa JKN.
Siku hii pia inatumika katika propganda za kisiasa.

Mimi niseme kidogo tu, kwa mtu bepari kama Lowassa hataki hata kusikia jina hili masikioni mwake. Anajua alichokwa anakisema Nyerere kuhusu utajili wake.
Alijitwalia mali na kuwaacha watanzania walio wengi wakiwa masikini bila huruma wakiwemo na watu wa Monduli

Ila uzuri tu nikwamba hizo pesa amezileta kwenye kampeni tunazila na Kura hapati, ili watawala wengine wa namna hii wasiwe wanachukua hela za serikali
Nawaomba watanzania wenye uzalendo wa kweli na nchi hii wasithubutu hata kidogo kumpatia kura huyu jamaa.

Tusijifanye tumepoteza kumbukumbu kuhusu huyu jamaa kisa kajificha kwenye kichaka cha UKIWA, Asije akawa kama katuloga ili tupoteze kumbukumbuku.
Wanao Muunga mkono wengi wao ni masilahi binafsi tu
Magufuli is for Public Interest ndo maana hakuna cha Timu Magufuli.
Asanteni
 
Kuna kiongozi sasa ndani ya serikali asiyekuwa au hata asiyetamani kuwa bepari au kabaila?
 
Mtoa post,unamkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Azimio la Zanzibar ambalo ndio lilizika Azimio la Arusha?
 
Ukimfagilia lowassa utakua unasukumwa na moja kati ya mambo haya (1) chuki dhidi ya mafanikio ya dr magufuli, (2) wewe ni mmkabila(3)utakua unatetea maslahi fulani binafsi,kikundi fulani au eneo fulani kama tulivyo shuhudia mikoa fulani ikineemeka na mingine ikibaki kama ilivyo (4)yawezekana ukawa unatatizo la kupenda bila kufanya uchunguzi,kitu ambacho ni hatari kabisa, tazameni ndugu zangu, watanzania wenzangu magufuli amefanyakazi iliyo washinda wengine ya kusimamia ujenzi wa barabara nchi nzima bila kujali kuwa yeye ni mtu wa chato, kamwe hakujivunia kuwa mtu wa chato bali utanzania, kila alipopelekwa kusimamia jambo matokeo tuliyaona wote, mimi si mwanachama wala mfuasi wa chama ila mimi naamini ktk kazi na uwajibikaji,nidhamu uaminifu na uvumilivu. Hebu tuwatazame hawa wagombea wetu wanafanana na wanayoyaahidi? Mwalimu ambae leo tunamkumbuka alisema, kiongozi wetu akisema atapambana na rushwa tumuangalie na tujiridhishe kama maneno hayo yanatoka moyoni mwake, kwa maana ni kweli atapiga vita rushwa au anatuhadaa?
 
Nyerere alisema ccm sio mama yake, sasa wewe kidampa wa it masaki una nini zaidi ya uchumia tumbo tu ili mkono uende kinywani? Tafuta shughuli halali ya kufanya acha kuishi kwa kuwalamba miguu mafisadi Wa ccm
 
lowasa hawezi kuwa rais hata akifanya maigizo ya kuzimia kwenye mikutano au kudeki bara bara ikulu haipatikani hivyo tare he 26/10 ambapo mauokeo yataanza kutangazwa mtashangaa sana
Hapa Kazi tuuu uzezeta peleka ukawa
 
haa haa labda kura upige peke yako..
 
nyerere tunayemkumbuka leo alipiga vita kwa nguvu zote ujinga na umasikini. leo ccm inatumia ujinga na umasikini kama kinga ya kujipatia kura kutoka kwa masikini wa kitanzania. nyerere alilinda raslimali zetu kama wanyama kwa nguvu zote ili kuvutia watalii leo ccm inaongoza kupandisha twiga kwenye ndege kupeleka ulaya. ccm ya sasa haimuenzi nyerere labda shetani.
 
Back
Top Bottom