Siku ya kwanza kufungua Biashara ilikuwaje?

KingPower

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
1,099
1,746
Wakuu habari poleni na majukumu!

Twende moja Kwa moja kwenye Mada tajwa hapo juu. Je, siku yako ya Kwanza kwenye biashara ilikuaje? Changamoto gani ulipitia?

Kwa upande wangu jana ilikua siku yangu ya Kwanza. Nilichokiuza lakini bado nina imani napo sana, maana hii ni biashara mpya

Asante.
 
Siku ya Kwanza alikuja Dada mmoja ana biashara kama yangu jirani Kama mita 100(sikua najua nilikuja kujua baadae) hata hakusalimia, alifika na kusema nimekuja kukopa kama haiwezekani naenda zangu jiuzie mwenyewe huyo akajiondokea zake.Nikajisemea kazi ipo nikabaki nashangaa.
 
Ukisikia wanga wa mchana ndio hawa. Alikuja pale kuku-frustrate 🥴🤒😁
 
Nakumbuka pale mwanzoni kwa kufanya biashara jirani yangu mwenye biashara kama yangu alikuwa anauza vitu kwa bei ya jumla badala ya bei ya rejareja.... Ili watu wakija huku waone vitu bei ghali wote wahamie kule kwake... Ilinusumbua sana🤪🥴

Ila uliza sasa hivi.... cha msingi kuwa na focus na usikate tamaa. Ila pia ushirikina una mwisho mbaya sana.
 
Back
Top Bottom