Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Natumaini mambo yanakwenda vizuri wanaJF wenzangu,
Siku inakatika hiyo, hairudi nyuma. Kuna huu ugonjwa wa tumbo (la kuhara) unapokamataga watu hasa wakiwa safarini, tena safari ndefu za mabasi. Kusimamisha bus porini unashindwa, dereva ndo kwanza anaamsha gari yupo speed 90 km/hr mnatoka lets say Mwanza Dsm, Mbeya Dsm, Tabora Dsm, Tunduma Dsm nk.Yaani acha tu aisee.
Kuna siku nilikuwa natoka Kahama naenda Dsm, gari ndo kwanza inashika njia, tumbo likaanza wajameni. Uzuri lilikuwa linastua, linatulia, linaamsha, linapoa. Hivyohivyo mpaka tukafika Hotelini Manyoni, yaani niliwahi toilet kama mshale.
Je, wewe mwenzangu siku tumbo lilipokukamata ukiwa safarini kwenye public transport uliionaje safari yako?