Habari za siku nyingi wana wa JF.
Niko na furaha nyingi. Nimetulia hapa nami nashangilia siku ya kuzaliwa kwa Tanganyika huru. Huru kutoka kwa weupe wa Kiiingereza. Leo hata job wala sijatokea.
Nimeamka kujitupa viwanja vya huku kitaani kwetu. Si vikali sana i'la ndo hivyo bia mbili tatu angalau.
Nisiwachoshe marafiki.
Leo katika mkao huu wa kupunga upepo bwana, Kuna wazo la kumbukumbu mbaya nisiyoipenda limenijia. Jambo hili kwa miaka 22 nimechelea kutolisema angalau niwe huru kiakili. Lakini je ninaweza. Laah nimeshindwa. Nitalisema. Imebidi. Mbona hata nisiposema ukweli huu nafsi inanisuta?
Jambo hili bwana huwezi kuamini nimegundua si mimi na mama tu tulijualo bali hata waume wa mama zangu wadogo na wakubwa wanalijua. Na tena naongeza pengine na wanao wanalijua. Ni gumu! Gumu haswa.
Mwishoni mwa mwaka 2000 hivi nilikuwa nimemaliza kidato cha nne. Basi nikatoka shuleni kule Tabora Boys nikarudi kwetu Marangu mkoani Kilimanjaro japo kiasili mimi si mtu wa hapo. Hapo homu nikaanza kuishi maisha mapya yasiohusiana na shule kabisa.
Nikalima na nikafanya vibarua vingine Kama kubeba mikungu ya ndizi za watu kupeleka hapa na pale. Lakini pamoja na yote haifanyi nisahau nilikuwa mtu wa kulala sana kipindi hiki cha kusubiri matokeo.
Hapo nyumbani rafiki yangu akawa mama yangu tU, coz baba ye alikuwa akifanya kazi mbali na akibaki huko hadi mwisho wa wiki anaporudi kututembelea. Nisiseme uwongo mama na babaangu ni watu walionipenda na wananipenda sana hata leo. Japo baba si mtu wa stori lakini upendo wake ulijidhihirisha kwenye huduma za kiskuli nilizopata kabla na baada ya kumaliza kidato cha nne, sita mpaka chuo. Hapa niligundua upendo huu mkubwa ada yote alilipa yeye na vingine. Itoshe kusema he is the best father ever.
Lakini sasa, Nianzie hapa katika miaka hii ya 2000 ndipo zilipokuwa zimeibuka simu za mkononi kipindi kile kulikuwa na simu maarufu zenye majina kama Motorola na Siemens. Mama na baba walikuwa na Motorola. Simu flani hivi kama ina mnara. Si unajua tena familia yetu ilikuwa na kipato cha Kati kwa hiyo simu kama zile haikuwa cha ajabu.
Maza bwana alikuwa kutwa akizungumza na maza mdogo aliyeishi Singida enzi hizo stori za hapa na pale mara kwa mara.
Sasa bwana katika siku za mastori yao, siku fulani wakaanza kupiga stori ya kutisha sana, stori kuhusu Mimi na baba yangu mzee Soni ( si jina lake halisi). Stori hii ndio iliyobadilisha kabisa fikra zangu kuhusu baba yangu mzee Soni . Nikawa namuogopa , simsogelei tena kama zamani, na sometime nikimuona namkimbia asiponiona.
Hili likatia stress katika moyo wa mzee wangu siku moja akaniita barazani. Akaniambia mwanangu una shida gani? Umekuwa ukinikimbia kila ukiniona. Huna uhuru tena hata wakati wa kula. Unaniogopa. Mimi ndie baba yako wa kipekee. Nikiendelea kuwepo ulimwenguni natamani uwe na furaha tele milele. Basi nikamjibu Hakuna shida baba sema tu nimekuwa na mawazo juu ya matokeo ya mitihani yangu. Akanijibu nitahakikisha unasoma mpaka uwezo wa kiakili utakapofika mwisho. Nitauza vyote hata ardhi na nyumba tatu ninazomiliki mjini ili usome!
Hili la kusema hivi lilinitisha zaidi. Nikazidi kuogopa zaidi. Kikao cha kupunguza kumuogopa mzee kikasababisha hofu zaidi.
Je akijua ninayoyajua kuhusu yeye na Mimi itakuwaje? Je ataniua? Ataniacha niishi? Je, atamuua mama? Je mama atajinyonga kwa fedheha?
Ninapojiuliza Mambo hayo ndipo nilipojiapiza itakuwa siri tu dhidi ya kumwambia ukweli mchungu babaangu mzee Soni. Labda aambiwe na wengine.
Ni siri gani hii? ITAENDELEA. Natania
Oh Hili neno itaendelea WanaJF hawalipendi sana. Hata Mimi silipendi pia.
Siku moja nilikuwa nimekaa nyuma ya nyumba yetu. Basi nikiwa nimejituliza hapo nikaskia mama akiongea na simu. Alikuwa akiongea kwa sauti ya kati lakini nikiisikia vyema. Ghafla simu ikiwa hewani akaanza kuniita Sela, Sela ,Sela. Nikanyamaza kimya. Nikasikia anamjibu wa upande wa pili kwenye simu "atakuwa kaenda kwa madem zake huyo tuendelee"
Mama akaendelea kusema " eh mdogo wangu moyoni naumia sana huyu mwanangu Sela anapendana na baba yake huyu utadhani babake kweli. Ile mbaya yani. Angejuua... Angekaa nae mbali kama nyuki. Mtoto anajipendekeza kama nini? Babake halisi nae anasumbuuaa ataka nimuoneshe mwanae. Hana nia mbaya lakini ataka tu kuona athari ya mkojo wake. Kama watoto anao wengi shida hiyo tu"
Kusikia hivyo nikatoka mbio mama asinione na kugundua nimesikia siri yake na mamdogo. Baadae nikarudi maisha yakaendelea. Baada ya miaka 22 ukweli nimeutoa huku mitandaoni but si baba, mamdogo wala mama wajuao kwamba ninaijua siri yao. Hata hivyo huyo babangu halisi simjui na Wala sitaki kumfahamu.
Mwisho.