Siku Mungu anapokuwa adui yako

Siku Mungu anapokuwa adui yako

Michael Anthon

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2017
Posts
219
Reaction score
110
Niweka mbali na watoto nyakati hizooo
Nyumbani huna chakula hata kidogo
Mfukoni huna hata mia

Mahakamani unakesi uliyoachiwa kwa dhamana
Kitaani unamadeni chungu nzima

Nyumba unayoishi unadaiwa pango la miezi sita
Mkaa uliokuwa unautegemea umetaifishwa na Maafisa wa mali asili na utalii

Shamba kashachukua mwenye nalo kwakushindwa kulilipia
Mama mzazi umemzika wiki iliyopita
Baba ana cancer yupo hoi kitandani

Mkeo anaujauzito wa miezi 8 anategemea huduma zako
Mwanao wa kwanza kafukuzwa ada

Rafiki zako uligombana nao kisa walipokukumbusha madeni ya nyuma
Mbaya zaidi eti na kanisani unadaiwa zaka na fungu la kumi!!!!!!!!!!
Hapo ndo utakapo jiuliza hivi Mungu jina lake nani!?!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom