Siku kuu ya dini, ujumbe wa siasa

JABEZ

Member
Apr 20, 2011
51
10
Ni sikukuu ya pasaka. Kila Askofu aliyepata nafasi ya kuzungumza, alizungumzia siasa: katiba mpya, amani na mustakabali wa taifa. Kwanini tafakari za siku muhimu kama hii zisilenge kuwajenga waumini na wananchi wengine kiroho zaidi? kwanini siasa zinachukua sehemu kubwa ya maisha ya wa TZ kama vile ndiyo maisha yenyewe? Tuna muda mrefu wa kujadili siasa, mwaka mzima. Siku hizi chache za sikukuku kwanini tusiimarishe imani? Bila imani (kila mtu ana yake) kuna siasa safi?
 
Una pointi mzee wa kijiji lakini siasa ikiwa chafu ikapelekea mapigano hata kanisani hutaenda so for the mean time inabidi siasa ipewe kipaumbele katiba mpya
 
siasa inaplay part kubwa sana ktk maisha ya mtanzania hasa kwa wakati huu kila kitu kimekuwa siasalized afu pia kwa upande mwingine viongozi wa dini hawana ujasiri wa kukataza dhambi coz na wao wanazifanya kwa saana tu, so wanadeal na kutaka kuboresha na kutengeneza maisha ya kimwili( ulimwengu huu) ya waumini wao kuliko yale ya kiroho yaani ya ulimwengu unaokuja. Tena kuna lingine la muhimu since wanatakiwa na Vitabu vya dini wale kutoka madhabahuni wanaona ni muhimu kudai maisha bora kwa waumini wao ili nao waweze kuishi kama waumini wanazidi kuwa maskini hata sadaka zinapungua so ni lazima waongelee siasa ambayo kwa sasa Tz ndo kila kitu ili maisha ya waumini wao yawe safi na wao waishi
 
Ni sikukuu ya pasaka. Kila Askofu aliyepata nafasi ya kuzungumza, alizungumzia siasa: katiba mpya, amani na mustakabali wa taifa. Kwanini tafakari za siku muhimu kama hii zisilenge kuwajenga waumini na wananchi wengine kiroho zaidi? kwanini siasa zinachukua sehemu kubwa ya maisha ya wa TZ kama vile ndiyo maisha yenyewe? Tuna muda mrefu wa kujadili siasa, mwaka mzima. Siku hizi chache za sikukuku kwanini tusiimarishe imani? Bila imani (kila mtu ana yake) kuna siasa safi?

Kwani roho inakaa nje ya mwili? kama ikitokea katiba mpya ikakataza uhuru wa kuabudu hizo imani unazotaka ziimarishwe zitaimarishiwa wapi? Samahani ndugu yangu nisije kuwa nimekukwaza, kwani tatizo langu ni kwamba sijui kama nina roho au kama nimewahi kuwa nayo.
 
Kama unaweza kutenganisha roho na mwili then jaribu kutenganisha siasa na dini....
Hii kauli ya "tusichanganye sias na dini...." zinatoewaga na watu wanaojua nguvu ya dini kwenye siasa sababu kimaandiko huu utawala wa kidunia na mamlaka zake vyote vipo chini ya Mungu, na watumishi wa Mungu(watu wa dini, ila kwa sasa hasa hapa kwetu sio wote) ndio wanakuwa wanawakilisha matakwa ya Mungu juu ya Taifa husika, hebu pitia hizi harakati za hawa watu

Osama na wanaharakati wengine wa JIHAD
Bishop Desmond Tutu
Martin Lutherking Jr
Malcom X
Na wengine kibao tu wanajamvi watanisaidia!
Tena sisi bado sana tuna watu wa dini waoga ndio maana mambo ya kijingajinga bado ni mengi.
Kwenye Biblia kuna stori ya Yohana, alikuwa anawasema watoza ushuru wasitoze zaidi ya viwango na watosheke na mishahara yao, pia akawachana maaskari kutokusingizia watu kesi.... hii yote ukileta kwenye mazingira ya sasa ni siasa.
Ni upuuzi na ni kitu kisicho cha ukweli kuwa eti utaihubiria "habari njema" nafsi iliyodhurumiwa na kukandamizwa katika mfumo wa ufisadi unaosimamiwa na hao hao watu ambao ndio waumini wa hizo dini, yaani huyo mtu huku ni mwanasiasa na kule ni muumini, so hapo utaona kwa kuingia kwenye siasa watu wa dini ni kama wanaenda upande wa pili wa shilingi ambapo watakutana na waumini wao walewale.
Tatizo ni kwamba viongozi wetu wa dini wengi ni wanafiki na waoga, wanaishia kujipendekeza kwa wanasiasa tu na kutoa matamko mepesi. Pia tatizo la waumini wanaoamini utenganisho wa dini na siasa.
 
Mbona ushangai Kikwete kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la pasaka badala ya Askofu? huna hoja tambaa, kwanza unatumia ID ya jina hilo ili kuwachanganya watu kati yako na Mzee Mwanakijiji. lakini kwa pumba zako siku si nyingi utajuwa tofauti kubwa kati yako na mzee mwanakijiji.
 
Nikiingia kwenye hoja moja kwa moja bila kumsaili mleta hoja ni kwamba tathmini yake ni yakinifu tatizo kasahau ama kaaacha makusudi kuelewa kua km ilivyo kwa kilimo kua uti wa mgongo (msiniulize mbonaaaaa....sitajibu) wa taifa kwa maana ya chakula na uchumi kwa kiasi chake vivyo hivyo siasa safi ni uti wa mgongo ama tuite ugoko kabisa kwa ustawi wa taifa! Sioni kosa kutoa neno la heri kwenye dini kwa ajili ya siasa kwa kua km siasa ikiingia mdudu si wewe wala wale wanaotaka kuwepo majukwaa maalum ya kuzungumzia siasa watakua na amani...siasa ni kwa ajili ya watu..popote penye mkusanyiko wacha mbegu idondoke!
 
Watu wa dini wana haki ya msingi ya kuelimisha,kufundisha,kutoa maoni na kukosoa mfumo wa maisha ya kila cku wa mwanadamu,waumini wanahaki ya kuelimishwa kuhusu katiba,mienendo mizuri ya maisha kama kuepuka ufisadi,utoaji na upokeaji rushwa nk,na sehemu pekee utakapo wapata waumini wote kwa pmj ni mickitini na makanisani cku za ckukuu na sherehe za dini thus why wanatumia fursa hiyo vizuri kuelimisha uma,ndio maana watu wa siasa ndio watu wa kwanza kuwaomba watu wa dini waiombee nchi so twaweza sema na wao wanachanganya siasa na dini?
 
Ni sikukuu ya pasaka. Kila Askofu aliyepata nafasi ya kuzungumza, alizungumzia siasa: katiba mpya, amani na mustakabali wa taifa. Kwanini tafakari za siku muhimu kama hii zisilenge kuwajenga waumini na wananchi wengine kiroho zaidi? kwanini siasa zinachukua sehemu kubwa ya maisha ya wa TZ kama vile ndiyo maisha yenyewe? Tuna muda mrefu wa kujadili siasa, mwaka mzima. Siku hizi chache za sikukuku kwanini tusiimarishe imani? Bila imani (kila mtu ana yake) kuna siasa safi?

tegemea comments nyingi kutoka misikitini.
 
karibu jamnvini mkuu. nadhani wewe ni mmoja wa wale walioambiwa JF ni threat kwa ccm wakati mlipokuwa dom kujivua gamba.

hahaha.
 
Nikiingia kwenye hoja moja kwa moja bila kumsaili mleta hoja ni kwamba tathmini yake ni yakinifu tatizo kasahau ama kaaacha makusudi kuelewa kua km ilivyo kwa kilimo kua uti wa mgongo (msiniulize mbonaaaaa....sitajibu) wa taifa kwa maana ya chakula na uchumi kwa kiasi chake vivyo hivyo siasa safi ni uti wa mgongo ama tuite ugoko kabisa kwa ustawi wa taifa! Sioni kosa kutoa neno la heri kwenye dini kwa ajili ya siasa kwa kua km siasa ikiingia mdudu si wewe wala wale wanaotaka kuwepo majukwaa maalum ya kuzungumzia siasa watakua na amani...siasa ni kwa ajili ya watu..popote penye mkusanyiko wacha mbegu idondoke!

mkuu ... sina swali hapa ...you are on the right track

viva fikra pevu
 
mleta hoja ana point ya msingi sana....inatia wasiwasi kwa sbb maaskofu wote wanahubiri amani kama vile wametumwa....!
kuna mtu mmoja anaitwa Richard kasesera nilimuona clouds tv anatoa tuzo za injili,alipokabidhiwa mic alimshauri anayempa tuzo kuwa aimbe kuombea amani mwaka mzima!!!!!!!!!!!!hii kitu wanajaribu kutuaminisha kuwa utulivu ndiyo amani! si kweli hata kidogo,hawa watu wanamradi wao behind that......ndo akina shigongo na matamasha yao ya uzalendo wanajaribu kuwahadaa watz kutimiza malengo yao ya kisiasa..

amani ipo ndani ya mioyo baada ya kutimiziwa matakwa/mahtaji ya kimaisha, amani siyo kinyume cha vita hata kidogo!!!
jana nimesoma gazeti moja linasema waislam wamekubaliana kuitenga ijumaa kuwa siku ya kuwajenga wanasiasa misikitini! lakini Kikwete na Bilali wakiwa kwenye misikiti hiyo hawawashauri masheikh kutochanganya siasa na dini....hivi wanafikiri bado watu wanaupofu wa miaka 47????kwa taarifa yao maaskofu wanaoganga njaa ndiyo watakaowahadaa siyo werevu walioenda shule.

Amani amani aman amani............................my --------!
mnatutisha eti ili tuogope na nyie muendelee kututawala kifalme nyie na vizazi vyenu.....hatukubali na hatudanganyiki ng'oooooo!
 
Binadamu ni nwili na roho,kamwe havitengani kwa mtu kubaki mtu kweli. Mtoa hoja aweke wazi,hivi hakusikia ujumbe wowote wa kipasaka? Nahisi mjumbe kama ulikwenda Kanisan au kuangalia TV na kusikiliza redio.sikio lako ulili'tune' ktk siasa.
SIASA inaadhiri maisha ktk ujumla wake,hivyo waumin ktk dini zao wanaathirika,mtu hawezi kuabudu vema akiwa ktk vurugu. Basi nawapa heko maaskofu kwa kukemea siasa chafu, hasa ulaghai ktk rasimu ya musuaea wa
katiba mpya
 
Back
Top Bottom