Siku kama ya leo

Siku kama ya leo

Mariswaga

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2015
Posts
201
Reaction score
2
SIKU KAMA YA LEO:

Inshallah siku kama ya leo itakuwa Oct 25, siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa sana na kila mmoja wetu.

Siku kama ya leo nitamaliza kero ya maji mtaani kwetu

Siku kama ya leo nitapata pembejeo za kilimo kwa bei nafuu haijapatapo tokea

Siku kama ya leo nitaanza kilimo cha umwagiliaji kitakachotimiza ndoto zangu kwenye kilimo

Siku kama ya leo nitamaliza kilio cha ufisadi nchini kwa kua nitajenga mahakama maalum itakayowashughulikia

Siku kama ya leo nitajenga vyuo vikuu vipya viwili, cha kilimo Butiama na cha madini Shinyanga

Siku kama ya leo nitakwenda kuing'oa na kuitupilia mbali mifumo mibovu ya serikali na Chama Tawala kwa kumuweka madarakani mchapakazi na mwana mabadiliko ya kweli.

Siku kama ya leo ntaenda kuchukua milioni 50 za mkopo wa vijana na wanawake wa mtaani kwangu ili niuage umasikini.

Siku ya kama ya leo nitafuta ada na michango yote ya wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Siku kama ya leo nitajenga zahanati pale kijijini kwetu ili bibi asiende umbali mrefu kutafuta huduma za afya.

Siku kama ya leo nitajenga kituo cha afya kwenye kata yangu ili wanawake wapate huduma nzuri za uzazi za karibu na haraka.

Siku kama ya leo nitajenga hospitali ya wilaya na kuijaza vifaa tiba vya kisasa.

Siku kama ya leo ndiyo mwisho wa kununua dawa kwenye duka la madawa pale jirani na hospitali.

Siku kama ya leo ndiyo itakuwa mwisho wa kwenda Muhimbili kupata huduma kwa kuwa hospitali ya rufaa itakuwa kwenye makao makuu ya mkoa wangu.

Siku kama ya leo nitapata ajira niliyoisotea kwa muda mrefu baada ya kufunguliwa kile kiwanda kilichokufa baada ya kubinafsishwa.

Siku kama ya leo nitaondoa kodi zote zinazomsumbua mama angu, mama ntilie na kaka angu bodaboda.

Siku kama ya leo mishahara na maslahi ya watumishi wa umma itaboreshwa na kuwafanya waishi maisha mazuri.

Siku kama ya leo babu na bibi yangu wataanza kupokea posho za kujikimu kila mwisho wa mwezi.

Siku kama ya leo nitaenda kupiga kura.

Siku kama ya leo nitamstaafisha siasa Yule fisadi papa liyelitia hasara taifa letu.

Siku kama ya leo nitaenda kupiga kura.

Siku kama ya leo nitamchagua kiongozi mpya muadilifu na mchapakazi.

Siku kama ya leo nitamchagua John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Siku kama ya leo wiki ijayo utashikwa na butwaa kuiona Tanzania mpya bila ccm ikizaliwa.
 
Siku kama ya leo itazaliwa Tanzania mpya, iliyo chini ya kiongozi mkuu muadilifu na asiye na madoa ya wizi. Tanzania ya Magufuli yenye neema ya viwanda na ajira tele
 
IMG-20151016-WA0087.jpg siku kama ya leo hii ndio itakua ratiba yangu ya kwenda kumstaafisha mtu siasa.
 
Siku kama ya Leo nitaenda kuudhihirishi umma kwamba Magufuli ndio Chaguo letu la kweli Tanzania #HapaKaziTu
 

Attachments

  • 1445184543014.jpg
    1445184543014.jpg
    143.3 KB · Views: 118
IMG-20151018-WA0006.jpg sitafanya makosa, nakumbuka jinsi nilivyokua nashiriki mijadala pale nkuruma alafu namchagua dr magufuli
 
Mh.Magufuli anafaa kwa kuwa Ukawa haina Mgombea Bora.Leo Escrow,Epa,Richmond sio hoja za msingi kutawala mjadala kwa kuwa ukawa inawakilishwa na Mwizi
 
Muda huu week ijayo nitakuwa kituoni nalinda kura.
 
Yaan siku kama ya leo jumapili jioni matokeo ya vituoni itakuwa fully mabadiliko if kituo kina wapiga kura 400 basi lowassa itakuwa above 350 magufuli less than 30. Shngwe nchi nzima zitatawala fully bodaboda na shamra shamra nchi nzima. NOTE MY WORD TODAY
 
Back
Top Bottom