Kuna jamaa tulikuwa tunamtibu hapa alivunjika. Ametibiwa amepaona lakini ndugu walikuwa hawaji kumuona Wala kulipa madeni. Pigiwa simu hawaji.
Deni limeongezeka mpka kulipika ni shida.Jamaa akamuambia daktari, wapigie simu ndugu zangu waambie nimekufa.
Waje wachukue maiti.
Simu ikapigwa
Ndugu wamepokea.
He, amekufa!!? Basi tunakuja baba!!
Baada ya siku 2 wamekuja na jeneza na gari wamekodi.
Kwenda wodini wakapewa faili.
Kalipieni madeni tuwape kibali mkachukue mwili wa marehemu.
Wakaenda uhasibu wakalipa madeni. Wamerudi wodini na risiti wakamkuta jamaa amekaa kwenye benchi anawasubiri.!!
Wakaangua kilio Tena.
Jamaa likawaambia, si mlitaka nifie huku huku. Nimefufuka Sasa.Twendeni nyumbani Sasa tukamalizane huko huko.
Just imagine, mtu katibiwa na kupona ndugu hawaji kumsalimia Wala kulipa gharama.
Walipoambiwa amefariki wakapata pesa za kukodi gari, kununua jeneza na kulipa gharama za hospitali.
Ina maana Hawa watu walikuwa wanaithamini zaidi maiti wanayoenda kuizika kuliko mtu aliye hai.
Hata Kama ndugu yako Ana mapungufu kiasi gani, uhai wake ni muhimu zaidi.
Thamini ndugu yako akiwa hai.
sent as received