Siku Chief Adam Sapi Mkwawa alipojiunga na TANU mwaka wa 1955

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,802
31,814
MAR
15

1558481_10202564359406945_14461383_n.jpg

Siku Chief Adam Sapi Mkwawa alipopokea fuvu la babu yake Mtwa Mkwawa
Kalenga

1480605_10202564360126963_1384702608_n.jpg

1939595_10202564355446846_1747412651_n.jpg

1239409_10202564351606750_127846408_n.jpg

''Maisha ya Chifu Adam Sapi Mkwawa yalitokea katika Baragumu Aprili 12, 1956. Alisoma Tabora na Makerere alikokwenda kusomea udaktari. Hakumaliza masomo yake na alilazimika kurudi nyumbani kuchukua nafasi ya Uchifu wa Wahehe. Alichaguliwa mjumbe wa Baraza la Kutunga sheria mwaka 1947 akiwa na umri wa miaka 27. Mwaka 1955 Abdulwahid Sykes na Dossa Aziz walialikwa na Chifu Adam Sapi kwenda Kalenga kwenye sherehe za kukabidhiwa fuvu la Chifu Mkwawa aliyejiua katika vita vya Wahehe na Wajerumani. Chifu Adam Sapi Mkwawa aliingizwa kisirisiri ndani ya TANU na Dossa Aziz hivyo kuwa mmoja wa machifu wa wachache sana waliounga mkono TANU.''
(Kwa maelezo ya Machifu waliounga mkono TANU angalia Sauti ya TANU No. 22 ya tarehe 28 Februari, 1958).
Kutoka kitabu ''Maisha na Nyakati za Abdul Sykes...''

1383757_10202564391607750_590406722_n.jpg

1891144_10202564361006985_839776287_n.jpg

''Our tour of Iringa took us to the museum of the Legendary Chief Mtwa (Abdullah) Mkwawa of the Wahehe tribe. He was a Muslim who fought the Germans in the late 19th century and after his defeat they took his skull to Germany as a trophy. He was converted by one Sheikh From Tanga and was taught Arabic and The Holy Qur'aan. The letter in Arabic is purported to have been written by him to the Sheikh in Tanga requesting for reinforcement to help him fight the Germans. His grandson the late Chief Adam Sapi Mkwawa managed to have his skull returned to Tanzania in 1955 and he received it in a parade of honour as some of these pictures show. Allah rhamhum.''
Picha na maelezo hapo juu kwa hisani ya Ummie Mahfoudha Alley.
 
Anayejiita Yericko Nyerere kuna wakati alijidai anaijuwa sana historia ya akina Mkwawa, akaulizwa maswali yakamshinda akaishia kuahidi kuwa akienda Iringa atakuja na majibu, leo takriban miaka mitatu au minne, hajafika tu huko Iringa?
Sema unaniita nije kujadili uzi huu, naijui historia ya Mnyigumba baba wa Mkwavinyika, na mtoto wake Adam Sapi.

Naijua kwakufika kwenye makabiri ya wazee hawa kule Lungemba na Kalenga na kutambika sio kwakusimuliwa kama usimuliwavyo wewe.
 
Haya tunaungana leo mwaka wa tatu, ulikataa kuwa Mkwawa ni Muislam. Ukabisha, ukasema utaends Iringa kuleta ushahidi. Alama Mohamed Said anaendelea kumwaga historia inayoonesha kuwa Mkwawa ni Muislam, vipi wewe yamekushinda na umeingia "mitini"?

Kijana uliyetamba kuwa utaleta ushahidi si ukiri tu ulikuwa hujui na umejifunza kitu kuhusu Mkwawa kwa kumsoma Alama Mohamed Said.
 
Hakuna udhibitisho wa kujitoshereza kuwa Mkwawa alikuwa Muislam, zinaweza kuwa ni story za kutungwa kama nyingine.

Over.................
 
Kyenju,
Historia ya Mkwawa ni ''documented'' na Wajerumani yaani imehifadhiwa
kwa maandishi na inaeleweka vyema.

Hili la kuwa alikuwa Muislam wala si jambo la kubishania hii leo.
Imekuwa ni bahati mbaya sana kuwa leo wengi wanatishwa na Uislam.

Lakini ili kumjua vyema Mkwawa inakubidi ujue hali ya nchi ilikuwaje katika
miaka ile ya katikati 1800 wakati Wajerumani wanaanza kujipenyeza nchini.

Angalia ni nani alipigana na Wajerumani.

Utamkuta Abushiri bin Salim al Harith, Sultan Songea bin Rauf, Sultan
Mataka bin Hamin Massaninga, Abdallah Mkwawa, Hassan bin Ismail

na wengine wengi.

Itakubidi umjue mshirika mkubwa wa Mkwawa, Rumaliza mzaliwa wa Lindi
ambae jina lake halisi ni Muhammad bin Khalfan bin Khamis al Barwani.

Rumaliza ndiye aliyekuwa akimpa silaha Mkwawa apambane na Wajerumani
na silaha hizi alikuwa akizitoa Zanzibar.

Mimi nimebahatika kukutana na kitukuu cha Rumaliza Dubai mwaka wa 1999,
Sheikh Muhammad bin Said na nilipojua kuwa ni kitukuu cha Rumaliza nilitaka
kujua mengi kutoka kwake.

Rumaliza kapigana pamoja na Mkwawa bega kwa bega na mmoja wa majemadari
wa Mkwawa alikuwa ndugu yake akiitwa Yusuf.

Ukitaka kujua zaidi kuhusu historia hii msome Ali Muhsin Barwani: ''Conflict and
Harmony in Zanzibar.''

Nilikuwa Zentrum Moderner Oriente (ZMO) Berlin kama ''Visiting Scholar,'' hii ni taasisi
kubwa sana ya utafiti wa historia na nimeona nyaraka nyingi sana za Tanganyika enzi
za Wajerumani.

Tusitishike na Uislam.
Tufanye utafiti tuijue historia ya kweli ya Tanganyika.
 
Haya tunaungana leo mwaka wa tatu, ulikataa kuwa Mkwawa ni Muislam. Ukabisha, ukasema utaends Iringa kuleta ushahidi. Alama Mohamed Said anaendelea kumwaga historia inayoonesha kuwa Mkwawa ni Muislam, vipi wewe yamekushinda na umeingia "mitini"?

Kijana uliyetamba kuwa utaleta ushahidi si ukiri tu ulikuwa hujui na umejifunza kitu kuhusu Mkwawa kwa kumsoma Alama Mohamed Said.
kujua kiarabu haimaanishi yeye ni muislamu, huenda ndio alikua anatumia kwa mawasiliano,kwani hao ndio watu kwanza kufanya nao biashara na shughuli zingine!!!!!!
 
Kyenju,
Historia ya Mkwawa ni ''documented'' na Wajerumani yaani imehifadhiwa
kwa maandishi na inaeleweka vyema.

Hili la kuwa alikuwa Muislam wala si jambo la kubishania hii leo.
Imekuwa ni bahati mbaya sana kuwa leo wengi wanatishwa na Uislam.

Lakini ili kumjua vyema Mkwawa inakubidi ujue hali ya nchi ilikuwaje katika
miaka ile ya katikati 1800 wakati Wajerumani wanaanza kujipenyeza nchini.

Angalia ni nani alipigana na Wajerumani.

Utamkuta Abushiri bin Salim al Harith, Sultan Songea bin Rauf, Sultan
Mataka bin Hamin Massaninga, Abdallah Mkwawa, Hassan bin Ismail

na wengine wengi.

Itakubidi umjue mshirika mkubwa wa Mkwawa, Rumaliza mzaliwa wa Lindi
ambae jina lake halisi ni Muhammad bin Khalfan bin Khamis al Barwani.

Rumaliza ndiye aliyekuwa akimpa silaha Mkwawa apambane na Wajerumani
na silaha hizi alikuwa akizitoa Zanzibar.

Mimi nimebahatika kukutana na kitukuu cha Rumaliza Dubai mwaka wa 1999,
Sheikh Muhammad bin Said na nilipojua kuwa ni kitukuu cha Rumaliza nilitaka
kujua mengi kutoka kwake.

Rumaliza kapigana pamoja na Mkwawa bega kwa bega na mmoja wa majemadari
wa Mkwawa alikuwa ndugu yake akiitwa Yusuf.

Ukitaka kujua zaidi kuhusu historia hii msome Ali Muhsin Barwani: ''Conflict and
Harmony in Zanzibar.''

Nilikuwa Zentrum Moderner Oriente (ZMO) Berlin kama ''Visiting Scholar,'' hii ni taasisi
kubwa sana ya utafiti wa historia na nimeona nyaraka nyingi sana za Tanganyika enzi
za Wajerumani.

Tusitishike na Uislam.
Tufanye utafiti tuijue historia ya kweli ya Tanganyika.

Great observation. ...this is what we need to learn. Sio propaganda zinazo nia kupotosha malengo
 
Safi sana, shusha material nyingine Muzei.
 
kujua kiarabu haimaanishi yeye ni muislamu, huenda ndio alikua anatumia kwa mawasiliano,kwani hao ndio watu kwanza kufanya nao biashara na shughuli zingine!!!!!!
Lab,
Mkwawa
alikuwa Muislam na jina lake Abdallah.
Kama nilivyosema hapo mwanzo hili si jambo la watu kubishana.

Mkwawa angeweza kuwa hata Mpagani na historia ya maisha yake
ingesomeka kama alivyoishi hayo maisha.

Hakuna popote katika historia ya Tanganyika ambako ipo jamii kwa
namna yoyote ile ilijifunza lugha ya Kiarabu kwa ajili ya biashara tu.

Lakini tunasema alikuwa Muislam kwa kuwa alikuwa Muislam.
Angalia kaburi lake hapo kwenye picha.

Hivyo ndivyo Waislam wanavyozikwa.
 
Nafikiri ukitaka kujua historia ya mkwawa nenda karenga kuna sehemu nilisoma kisegere cha mtwa mkwawa akielezea historia ya mkwawa kwamba imetoka kwa mufwimi aliekuwa ametokea ethiopia na muwindaji hodari..mzee mohamed said anasema tena alikuwa mngazija
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom