Hakuna kipindi kizuri ambapo Simba na Yanga zinakutana kama sasa ambapo macho na masikio ya wapenzi wa soka la Tanzania, Afrika Mashariki na Kati yataelekezwa katika dimba la Taifa kuanzia majira ya saa 10 jioni kushuhudia timu hizi kongwe nchini zikiwania uongozi wa ligi na vilevile kujiweka vizuri katia safari ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi hapa Tanzania Bara.
Ynaga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifurusha Simba 2-0 katika mchezo uliochezwa Septemba 2015 na hivyo itataka kuionesha jamii ya wapenda soka kuwa haikubahatisha ushindi ule, huku Simba nayo ikitaka kujifuta machozi ya kipingo kile kwa kurudi 'njia kuu' ya ushindi dhidi ya Yanga kama ambavyo imekuwa ktk miaka ya karibuni.
Hata hivyo kama tulivyosema hapo juu, kipindi hiki timu zinakutana zikiwa katika fomu nzuri na ndio maana zinaongoza ligi, kufunga magoli mengi na pia kucheza 'mpira mwingi'.
Katika mchezo ule wa mkondo wa kwanza, timu zote zilikuwa zimeshinda mechi tatu za mwanzo wa ligi kabla ya kukutana lakini Yanga ilionekana kuwa vizuri zaidi, ikiwa na wachezaji bora na wazoefu, kikosi kipana na kocha makini na mwenye mzoefu mkubwa hivyo wachambuzi wengi waliipa nafasi kubwa zaidi ya kuibuka na ushindi dhidi ya Simba ambayo ilikuwa na wachezaji wengi wageni, vijana na kocha mpya huku wachezaji wake wakidaiwa kuwa wanagenzi kulinganisha na wapinzani wao.
Katika mchezo wa Jumamosi hii, Yanga bado inaendelea kuonekana kuwa bado ina ubora uleule au zaidi kidogo na kwa hivyo wengi wanasubiri kuona ni namna gani itaendelea kuuthibisha ubora huo uwanjani dhidi ya mnyama. Hata hivyo Simba inaonekana kuwa imepiga hatua kubwa zaidi kulinganisha na ilivyokuwa Septemba mwaka jana.
Wakati Yanga ikitumainia ubora na uzoefu wao, Simba inajipigia chapuo na ufundi mwingi ulionyeshwa na kikosi hiki hadi sasa katika mechi za karibuni huku ikicheza 'mpira mwingi' kwa kasi na kufunga magoli ya videoni... wenyewe wanauita mpira wenye udambwiudambwi.
Kabla ya kutoa tathmini ya mechi hii inayokuja Jumamosi hii ni vizuri kuangalia mazingira na hali ya mchezo uliotangulia. Katika mechi ya Septemba 2015, Simba kama kawaida waliunza mchezo vizuri huku wakikamata kiungo na kulitia kashkashi kadhaa goli la Yanga kwa sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza hadi kulazimika kocha wa Yanga van Pluim kumtoa winga hatari Simon Msuva na kumwingiza Malimi Busungu. Ni mabadiliko haya yanayotajwa kuwa moja ya mabadiliko bora zaidi ktk kipindi cha hivi karibuni yaliyoleta mapinduzi ya mchezo huu ambapo eneo la ulinzi la Simba lilianza kupata majaribu makubwa na kujikuta wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili. Aidha pamoja na kumiliki mpira katika kipindi cha kwanza fowadi ya Simba haikuwa na uelewano mzuri ambapo Kiiza na Mgosi walijikuta chini ya ulinzi mkali wa Yondani na Cannavaro kiasi cha kutumia muda mwingi wakiwa wanatembea uwanjani kutokana na kushindwa kupewa pasi za maana au wao wenyewe kujitengezea nafasi za maana.
Katika mechi iliyopita Simba iliwakosa nyota wake Jonas Mkude na Abdi Banda waliokuwa majeruhi na hivyo kulifanya eneo la kiungo kukosa mbinu mbadala za kuidhibiti Yanga hususani kushindwa kucheza vizuri mipira mingi ya vichwa katika eneo la katikati na hivyo mipira mingi kuangukia mikononi mwa viungo wa Yanga akina Kamusoko aliyecheza vizuri sana mechi hiyo.
Mechi hii ya Jumamosi inamkuta Jonas Mkude akiwa amerudi kwenye ubora wake lakini pia akiwa amejenga uelewano mkubwa na Justice Majadvi na Mwinyi Kazimoto huku fulbeki zote mbili Kessy na Tshabalala zikiwa tayari kusaidia mashambulizi kila inapowezekana. Isitoshe, eneo la ushambuliaji la Simba limeimarika sana kipindi hiki tofauti na mechi ile kwa sababu kuna maelewano ya kuridhisha kati ya Ajibu na Kiiza huku pia kocha wa muda Jackson Mayanja akiwa na washambuliaji wanaotokea benchi hususani Danny Lyanga, Hijja Ugando, Brian Majwega, Peter Mwalyanzi na wengineo wenye uwezo wa kusaidia na hata kubadilisha matokeo inapobidi.
Eneo la ulinzi la Simba pia limeimarika huku ingizo jipya la kipa Muivory Coast Vincent Angban akiwa na uzoefu wa kutosha na kuonekana kuituliza timu wakati wa pressure tofauti na Peter Manyika aliyecheza mechi ya awali ambae bado anaendelea kupata uzoefu. Hata hivyo tunaweza kusema bado eneo la ulinzi la Simba bado sio bora sana licha ya kufungwa magoli machache ktk VPL kwa kuwa baadhi ya wachezaji wake wa kati wana mapungufu ambayo yakitumiwa vizuri na wapinzani yanaweza kusababisha matatizo zaidi.
Tukirudi kwa upande ya Yanga, ingizo la hivi karibuni la Haruna Niyonzima ambaye ametoka ktk mgogoro na timu yake, limeingozea nguvu baada ya kupumzika kwa muda wa kutosha na kukusanya nguvu mpya kumpunguzia kazi Thabani Kamusoko ambaye amekuwa akibeba kiungo cha Yanga mabegani mwake kwa ubora na ufanisi mkubwa kwa siku za karibuni. Ubora wa eneo la ushambulizi la Yanga linajulikana huku Donald Ngoma na Amissi Tambwe wakiwa na ubora uleule lkn wakiwa wamejenga uelewano mkubwa zaidi. Kitu kizuri ni kuwa Simon Msuva ambaye huonekana kuchemza mechi za watani, anaonekana kupevuka akipiga krosi nzuri maarufu kama 'krosi pasi' lakini pia akiwa anatoa pasi za magoli zaidi na hata kuzitumia kwa utulivu kiasi.
Ingizo jipya Paul Nonga anaongeza upana na makali ya eneo la ushambuliaji la Yanga na uzoefu wake na maelewano aliyojenga na Malimi Busungu yanaweza kuwa na madhara makubwa katika mitaa ya Msimbazi kama hatapata ulinzi wa kutosha. Hata hivyo, kama ilivyo kwa Simba, eneo la ulinzi la Yanga linaonekana kuwa ndipo palipo na 'jipu' hasa baada ya kukosekana kwa Kelvin Yondani aliyefungiwa na hatihati ya kukosekana kwa mlinzi mzoefu Nadir Cannavaro'.
Tumalizie kwa kusema, kama timu zote zitaamua kucheza mpira uwanjani na kuonesha kile walichonacho, tunaweza kushudia mechi bora kabisa maana timu zote ziko katika kiwango kizuri na zina makocha wanaojua kazi zao.
Natabiri matokeo kuwa 2-1 au 2-3!
Naifike siku hiyo ubishi uishe.