Siku 14 kanda ya Ziwa! Mwanza: hoteli na chakula safi,gharama nafuu,mazingira yanavutia,machinga makoroboi bado wapo....,daladala sumbufu,vituo vya foleni ya kupakia zaidi ya vitatu(kishiri-buhongwa) mamlaka husika fuatilieni;chato stendi yenu aibu,magufuli uko wapi! Muleba stand,choo kichafu kuliko vyote kanda hiyo,mamlaka mko wapi halafu eti ni 300tshs,Bukoba yote; gari ndogo(tax) zimegeuzwa daladala na zinaoverload(mbele wanne nyuma watano badala ya watu wanne tu in total) trafiki mmelala au mnasubiri ajali? Kiwanda x, nyumba za wafanyakazi ni full suti ya bati kama polisi...majanga;Gest za mutukula majanga,mashuka yananuka mikojo zaidi ya toilet; tra kyaka, hamkagui vema mizigo hasa kwenye mabasi mnaikosesha serikali mapato;Watumishi wa uma wa kihaya ni wabaguzi hasa idara ya elimu,usiombe mtu wa kabila lingine ukapangiwa kule kikazi,utajuta,badilikeni!!!! Bariadi,baikeli ndo daladala,mikokoteni ya ng'ombe mpaka mjini,disco linapigwa ovyo kwenye makazi ya watu siku za wkend,mamlaka ya mji mko likizo? Kanda yote ya ziwa wanazungumza lugha zao mpaka maofisini,hamjajui kuwa lugha rasmi ni kiswahili? Au mnahisi sisi sote ni wahaya/wasukuma! Wahudumu mahotelini sehemu kubwa wanajiuza japo hawajitangazi. Hitimisho; Sehemu kubwa ya jamii ya kanda ya ziwa ni wakarimu sana,nitarudi tena Mwanza......