Siku 100 za Utawala wa Dr Shein mwendo mdundo

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Wachina wana msemo "Safari ya maili 1000 inaanzwa na hatua moja". Dr Shein katika safari yake ya miaka mitano ameanza kupiga hatua kuelekea ngamani, lakini amefungwa vikwazo( gavana) miguuni mithili ya vikuku vizito.

Mshindani wake wa kisiasa Maalim Seif ambae anaonekana kumfuata nyuma kwa kasi ya konokono na kumuombea dua la mwewe ateguke miguu ili ateleze na kuweza kumpokonya kijiti na kushika dola!

Ni siku 100 za machungu na uvumilivu kwa Dr. Shein ya kutaka kujaribu kuviunganisha vipande viliovunjika vya kioo vya utengamano bila ya mafanikio.
Ni siku 100 za machungu na uvimilivu kwa Maalim Seif ya kutaka kuidaka bila mafanikio tonge iliokuwa inaelekea kinywani mwake na kuanguka na hata kuomba usaidizi huwa wa kukatisha tamaa

Ni siku 100 za majigambo na tashtiti kwa Dr. Shein kumwelekezea mpinzani wake na kumueleza kuwa uchaguzi umekwisha na sasa ana andaa mikakati ya ushindi wa uchaguzi wa mwaka 2020

Ni siku 100 za majigambo na tashtiti kwa Maalim Seif kumuelekeza mshindani wake kuwa yeye ni Rais halali wa Zanzibar na kamwe Dr. Shein hatamaliza ngwe yake iliobaki!

Ni siku 100 za fitina na na mfarakano kwa wananchi wa Zanzibar ambao wanauona mustakabali wa nchi yao umewekwa rehani na si rahisi kugomboka na kile ambacho wanachokiona kiko mbele yao ni giza nene lisiopambazuka tu.

Ni siku 100 za utawala wa Dr Shein ulioangukia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan,mwezi wa toba na maghufira. Mawaidha mazito yanayohubiri amani kusameheana na kustahamiliana ni kasida zinazovuma kila siku na pembe zote za Zanzibar. Nilitarajia funga zetu zingefyatua mishipa ya fahamu ya viongozi wetu kuirejesha nchi yetu zama za Siti Binti Saad pale alipotuturubisha " Zanzibar ni njema atakae aje lakini asije kufanya fujo"

Tumewaona Nahodha na Rubani wanavyo gombania sukani wakiburuzana Tezi na Omo; Imefika wakati wa kurejea ngamani kwa mustakabali mwema wa mama Zanzibar.
 
Zanzibar hakuna raisi. Kuna mtu anayesadikiwa kuwa raisi na vyombo vya dola tu. Wananchi hawamtambui. Ni ngumu sana zanzibar kuendelea bila serikali kuwepo. Wananchi wa zanzibar wanajiongoza wenyewe kwa sasa.
 
Wachina wana msemo "Safari ya maili 1000 inaanzwa na hatua moja". Dr Shein katika safari yake ya miaka mitano ameanza kupiga hatua kuelekea ngamani, lakini amefungwa vikwazo( gavana) miguuni mithili ya vikuku vizito.

Mshindani wake wa kisiasa Maalim Seif ambae anaonekana kumfuata nyuma kwa kasi ya konokono na kumuombea dua la mwewe ateguke miguu ili ateleze na kuweza kumpokonya kijiti na kushika dola!

Ni siku 100 za machungu na uvumilivu kwa Dr. Shein ya kutaka kujaribu kuviunganisha vipande viliovunjika vya kioo vya utengamano bila ya mafanikio.
Ni siku 100 za machungu na uvimilivu kwa Maalim Seif ya kutaka kuidaka bila mafanikio tonge iliokuwa inaelekea kinywani mwake na kuanguka na hata kuomba usaidizi huwa wa kukatisha tamaa

Ni siku 100 za majigambo na tashtiti kwa Dr. Shein kumwelekezea mpinzani wake na kumueleza kuwa uchaguzi umekwisha na sasa ana andaa mikakati ya ushindi wa uchaguzi wa mwaka 2020

Ni siku 100 za majigambo na tashtiti kwa Maalim Seif kumuelekeza mshindani wake kuwa yeye ni Rais halali wa Zanzibar na kamwe Dr. Shein hatamaliza ngwe yake iliobaki!

Ni siku 100 za fitina na na mfarakano kwa wananchi wa Zanzibar ambao wanauona mustakabali wa nchi yao umewekwa rehani na si rahisi kugomboka na kile ambacho wanachokiona kiko mbele yao ni giza nene lisiopambazuka tu.

Ni siku 100 za utawala wa Dr Shein ulioangukia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan,mwezi wa toba na maghufira. Mawaidha mazito yanayohubiri amani kusameheana na kustahamiliana ni kasida zinazovuma kila siku na pembe zote za Zanzibar. Nilitarajia funga zetu zingefyatua mishipa ya fahamu ya viongozi wetu kuirejesha nchi yetu zama za Siti Binti Saad pale alipotuturubisha " Zanzibar ni njema atakae aje lakini asije kufanya fujo"

Tumewaona Nahodha na Rubani wanavyo gombania sukani wakiburuzana Tezi na Omo; Imefika wakati wa kurejea ngamani kwa mustakabali mwema wa mama Zanzibar.
Umesahau kuandika kwamba pamoja na mambo mengine MWEZI WA RAMADHAN UNAKATAZA MWISLAM KUFANYA DHULUMA , ya wazi ama ya kificho kwa mapanga ama kwa vifaru .
 
Back
Top Bottom