Sikio kuziba

Sikio kuziba

Aizeck12

New Member
Joined
Aug 23, 2025
Posts
2
Reaction score
2
Jaman naombeni msaada juzi nimeamka nimekuta masikio yamezipa tu yemyewe hata sielewi shida nini nimetumia dawa ile ya boric acid na labda kufuta na pamba lakini haisaidii kitu. Na nina mafua wiki ya pili saizi hayaishi eti
 
unatumua earphone, matumizi ya simu kuongea ni myda gani, umeoga maji yakaingia, kuna baridi kali ulipo?
 
Earwax imezidi nenda hospital waondoe uchafu na kuyaosha, mi tatizo Hilo pia linanisumbua.
 
Nenda hospitali mkuu, macho, masikio, pua, mdomo na sehemu za siri sio maeneo ya kuchekea ukiona kitu huelewi.

Na sio vizuri kutumia dawa mfululu bila kujua tatizo, ni kheri usitumie mwili ukapambana wenyewe.
 
kuna dawa ya macho ya 2000 tsh ambayo hutibu sikio ama kitunguu swaumu mafuta yake kama halijaziba kwa uchafu twanga paka maji yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom