SIKIA SAUTI YA MUNGU

SIKIA SAUTI YA MUNGU

Principal Focus

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
925
Reaction score
550
SIKIA SAUTI YA MUNGU

Ufunuo wa Yohana 22 : 17 - Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.

Bwana Yesu asifiwe! Ni mara nyingine tena Mungu ameniongoza nishiriki nanyi kuandika ujumbe huu utakao kuwezesha kusikia sauti ya Mungu ama sauti ya neno la Mungu, kwasababu Mungu ametupa neno ili tupate kupona, tuwe huru na vifungo vyetu, magonjwa yapone, vilema watembee, na vipofu waone, vile vile neno lake pia anatwambia haja zetu zijulikane mbele yake kwa maana yeye hujishughulisha na mambo ya kwetu. Ametupa neno alafu anafanya kazi ya kutuhumia sisi, Yesu kaenda mbinguni kutuandalia mahali patakatifu huku akidumu kutuombea si kwasababu tuna mpenda Mungu sana au tumetenda mema mno la hasha ni kwasababu Mungu aliupenda ulimwengu akamtoa mwana wake wa pekee ili tukombolewe. Mungu anasema katika mwanzo kuwa sisi wanadamu mawazo yetu ni mabaya kila siku, yeye hutuwazia mema lakini sisi tunawaza uovu, ikafika mahala ikabidi afupishe siku zetu za kuishi ili neema itukomboe si kwamba anatuchukia sana hapana bali alifupisha ili siku zetu ziwe chache na tutende mema katika Jina la Yesu Kristo, Haleluya! Haleluya! Mwana wa Mungu!

Muongozo wetu unatoka katika kitabu cha ufunuo sura ya 22 na mstari ule wa 17, Biblia inasema hivi; "Ufunuo wa Yohana 22 : 17 - Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure".
Yesu anakuita uje, na ukisikia useme njoo, na kama unakiu uje unywe mji kwa maana ni bure. Mungu hutuita na tukisikia tuende na kuita wengine pale ulipo na kiu ya neno lake ni bure halilipishwi kiasi chochote kwa maana gharama zake amekwisha kuzilipia pale msalabani, kwa damu ya Yesu Kristo ile inenayo mema maishani mwetu. Wokovu wa Mungu ungekuwa unalipiwa kama uganga leo hii watu wangekuwa wengi humu kila mmoja amejijazia neno la kwake ili mamlaka tulizopewa zifanye kazi kila anapobonyeza button (kitufe). Lakini sasa Mungu ametulipia hizo gharama lakini kumwamini katika maisha yetu imekua issue nyingine, hakuna anaemwamini tena, watu wanaenda kanisani lakini magonjwa yao, shida zao, fedhea zao, mawazo yao, furaha yao, amani yao, hadi kuamini kwao hakupo kwa Mungu. Hawaamini kama Mungu ananguvu na uweza mkubwa mno, maisha ya sasa mtu anaenda kutafuta baraka kwa waganga, lakini kanisani unamuona lakini rohoni kaziba sikio asisikie wokovu wa Mungu. Biashara zake zimetawala maagano na mikataba ya nguvu za giva lakini sura amevaa ya Jumamosi kwenda kuadhimisha sabato na jumapili kuwahi siku mahali pa mbele abisa kuketi but moyoni siri yake anaijua yeye mwenyewe. Watu hawataki kusikia sauti ya Mungu ibadilishe maisha yao but wanataka kusikia kile wakipendacho kukisikia.

Siku hizi imekuwa trend watu kujaa kanisani si kwa ajili ya kusikia sauti ya Mungu bali kusikia wanatabiriwa utajiri, kazi nzuri, mume/mke mwema, afya njema, elimu nzuri hadi kuishi maisha marefu zaidi na zaidi wanasahau Mungu alifupisha siku zetu ili tupate wokovu na kutenda mema ili tuishinde dunia.
Katika Biblia Mwanzo 6 : 3 inasema "Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini".
Mungu alitupunguzia siku kusudi dhambi zetu zipate kutakaswa, Yeye alipokuwa anawaza kutuokoa na utumwa wa mauti sisi tunawaza uasherati, nafsi ya Mungu ili kata tamaa kushughulika na sisi lakini asanteh Mungu kulikuwa na Nuhu wakati huo, alikua mcha Mungu ndio hadi sasa tupo hivyo hapo ulipo ni kwa neema na agano Mungu aliloliweka kwetu. Nafsi yake ingesononeka tena kwa kukosa wamchao hakika sasa dunia na vitu vyote vilivyopo visingekuwepo lakini alitazama wema wa mtu mmoja kwa faida ya wengine. Mungu aliweka agano na Ibrahim kuwa baba wa mataifa, Yesu akija kupita hapa hatazami wazazi wako ni akina nani lakini anatazama kusudi lake na agano la Baba yake juu yetu, mimi sidhani kama umesoma habari za Zakayo katika Luka 19 : 8 - 9 "Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu". Yesu hakushugulika na wazazi walio mzaa Zakayo bali Zakayo aliposikia sauti ya Mungu utii wake ukamfanya Yesu atazame agano Baba yake alilolifanya na Ibrahimu juu yetu na wokovu ukawa ndani ya nyumba ya Zakayo. Wewe unafanya nini mpaka usisikie neno lililotumwa kwako ili usikie sauti ya Mungu upate kupona!? Kusikia unaweza ukasikia lakini biblia inasema watasikia ila hawata elewa, hivyo ukiona hauelewi mahali kuhusu sauti ya neno uliloitiwa usiudhunike moyoni, la hasha omba Mungu usikie sauti yake kwa maana Imani huja kwa neno la Kristo hivyo inabidi uongeze imani ili uweze kusikia. Yesu anasema ili uweze kusikia sauti ya Mungu ni lazima uwe na imani, uwe na hakika ya kile utarajiacho kitendeke. Tuangalie Luka 17 : 6 - "Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii". Kiasi kidogo tu cha imani kinaweza kusikia sauti ya Mungu kwako hata ukafanya mambo makubwa sana kiasi cha kuuambia mti ng'oka ukaote baharini ungetii lakini vipi kuhusu kusikia neno!? Je tusinge weza sikia? Jibu ndio tungesikia mengi kutoka kwa Mungu na kufanyika imani, hivyo tutayarishe utayari wetu kwa kusikia neno, tuvue viatu tuweze kukanyaga mahali patakatifu na kusikia neno maana utayari wetu upo kwenye miguu yetu. Huwezi kusikia neno kama utayari wako umefufungwa, Waefeso inasema silaha moja wapo ni miguu na kwenye miguu upo utayari wa kusikia Injili ya Yesu Kristo, mimi sijui kama unajua utayari wako wa kusikia neno la Mungu upo kwenye miguu yako, mfano: " Unaweza mfahamu mtu ambaye ulijua kabisa anamtumikia Mungu lakini ghafla ule utayari unapotea, ile hali ya kutaka kuomba na kusikia neno a Mungu haupo tena, kila akijaribu kumrudia Mungu anakaa siku ya kwanza, ya pili lakini siku ya tatu unamkuta baa anakunywa na kufanya uasherati, hivyo jua miguu yake imetekwa na ardhi imesemeshwa asiwe tayari
Kusikiliza neno la Mungu hivyo anaweza akaombewa lakini wasip shughulika na miguu yake ataenda siku ya kwanza atakuepo anaweza kukaa miaka au miezi watu wakajua amebadilika kumbe rohoni anajua mwenyewe utayari wake wa kutumika tena haupo, hamu yake ya kusikia tena haipo, katika ulimwengu wa roho ameshapokonywa silaha yake hawezi tena" Musa aliambiwa vua viatu vyako kwa maana hapa ni nchi takatifu. Kutoka 3 : 5 - "Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu". Mungu hakua na shida na viatu vya Musa bali alikuwa anashida na utayari wa Musa ili asikie neno lake, sauti yake, maelekezo yake hata mpango wake ndio maana akamwambia Musa vua viatu vyako hapa ni nchi takatifu, kwa tafsiri nyingine nchi humaanisha ardhi, mimi sijui kama unajua lakini kumbuka Mungu alilaani ardhi isiwe sidhani kama uliewa lakini ardhi hutumika kushika/hubeba/kukanyagakukanyaga miguu yetu hivyo utayaei wetu hutafutwa kupitia ardhi, mtu mwenye nia ovu katika nyumba yako haji kukudhuru tu kienyeji lazima aje kwanza asemeshe ardhi unayokanyaga na kutembea kila siku ndipo dawa zake zifanye kazi kwako,, ndio maana anatafuta jinsi ya kuteka utayari wako kama Waefeso 6 : 15 - "na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;"
Utayari wako wa kusikia neno la Mungu ama sauti ya Mungu unatokana na utayari wako jinsi ulivyo ndio maana biblia inasema miguu ni utayari pia ni silaha ngoja nirudie tena.

Waefeso 6 : 10 -20 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili; ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena".

Shetani anajua utayari wetu uko wapi mdio maana huwai miguu yetu, bila utayari imani haipo, bila utayari neno halipo, bila utayari kuomba hakupo, bila utayari wema na busara kwako hazipo hivyo unahitaji neema ile ya Mungu ikuponye miguu yako kwa maana Mungu anasema akiweza kukupokonyonya miguu yako na sikio basi jua umepona kutoka kwa adui. Tusipokuwa tunaomba utayari wetu tunanyang'anywa na adui maana atakuja atuteke na si tu wewe usimame uombe kwa ajili yako peke yako bali unatakiwa pia uwaombee na wengine utayari wao urudi ili kwenye timu ya maombi mume wengi pia bila kusahau kumuombea yule aliyekuhubiria Injili maana wote ni binadamu kila mmoja akisimama katika zamu yake kwa imani hakika adui mwovu tutamshinda maana vita yetu si ya nyama na damu bali ni falme, na mamlaka ya nguvu za giza na jeshi la mapepo katika ulimwengu wa roho. Hivyo usichoke kuomba pia usiombe huku unalalamika mimi sijui kama umesoma Habakuki. Habakuki alikuoa anaomba huku analalamika lakini ilifika mahali alisitisha kulalamika akaanza kuomba "Habakuki 2 : 1 - Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu." Sura ya tatu anarudi tena kuomba nakusema Habakuki 3 : 2 -" Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema". Hivyo kumbuka pindi unaomba Mungu hujibu ulichoomba kama uliomba kulalamika Mungu hujibu lalamiko lako na kama unaomba upendo kuwa na hakika Mungu atajibu pendo lake hivyo simama katika zamu yako kama Habakuki na umwombe atangaze rehema katikati ya gadhabu yako usichoke kuomba mpaka ile hakika itokee, mpaka mlima uote baharini, mpaka mapepo na magonjwa yakutii, usisahau kuvaa silaha za Mungu katika kuomba kwako, katika kuishi kwako ili usikie sauti ya Mungu na upate kuelewa Mungu anakuelekeza nini mwaka huu, Mungu anakuelekeza nini maishani mwako. Haleluya! Haleluya! Sikia sauti ya Mungu anayekuita utoke huko Misri ijapokuwa safari yako utatembea miaka arobaini ila uwe na hakika lazima Mungu atakufanikisha ufika katika mji mpya aliokuahidi siku ya ufufuo.

Bwana na Bibi harusi wanakuita njoo, sikia sauti yao upate kuendea maji yale ya uzima usipate kiu tena, vaa nira za Yesu kwakuwa ni laini na mzigo wake ni mwepesi "Mathayo 11 : 30 - kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi". Sikia sauti yake, nenda msalabani na mizigo yako, dhambi zako, fedheha zako, uchovu wako, kutokufanikiwa kwako, kutokumiliki kwako, njaa yako, kiu yako, ugonjwa wako, hofu yako, majukumu yako, fikra zako, ukatubu kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia. Ukisikia sauti yake lazima uachilie roho ya toba ili mzigo wako upungue, mpe matatizo yako ama mzigo wako yeye ataupokea na kukubadilishia mzigo. Atakupa nira yake na mzigo havitakuwa tena kero kwako maana hofu yako umeiacha pale msalabani kwa maana amekununua kwa damu yake ya thamani usiwe tena mtumwa uwe huru "1 Wakorintho 6 : 20 - maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu".

Mzigo wake ni mwepesi sikia sauti yake na uvue viatu vyako upate utayari utakao badilisha maisha yako katika jina la Yesu Kristo, Eeh Mungu katika jina la Yesu Kristo naomba utayari wa mtu huyu anaesoma ujumbe huu urudi, katikati ya ugonjwa wake ee Mungu mpe uponyaji wake sawa sawa na Kitabu cha nabii Isaya kuwa Yesu amekuja tupate kupona, katikati ya njaa yake ee Mungu umlishe neno lako apate kushiba asiwe na njaa tena, ee Mungu katika jina la Yesu Kristo, msomaji wa ujumbe huu akiwa katikati ya gadhabu kumbuka rehema zako Mungu, akiwa katikati ya kutokukubalika kwake Mungu mkumbuke, akiwa katikati ya kifungo chake mtangazie uhuru wake ee Mungu katika jina la Yesu Kristo, naomba majibu yako sasa ee Bwana Mungu mponyaji ulituma neno lako ili tupone katika jina la Yesu Kristo, badilisha maisha yetu sisi watumishi wako tupate kutenda kazi yako kwa mapenzi yako ee Mungu, wakumbuke kutuombea ili tuzidi kupata ujasiri wa kutangaza Injili yako kwa maana asipoomba ee Mungu utayari wake utanyang'anya ama kutekwa na yule mwovu Ibilisi azungukae kama simba angurumaye ili apate kutushitaki ee Mungu, tuzidishie imani na upendo kwa maana tulitoka kuwa chini ya sheria sasa tupo katika neema yako. Ee Mungu usiruhusu tuendelee kufanya dhambi ili neema iongezeke bali ruhusu mapenzi yako yatimizwe tupate kuvuna katika shamba lako maana tayari ulikwisha panda sasa ni muda wa mavuno tu, ee Mungu katika jina la Yesu Kristo badilisha maisha yetu tuongoze, linda familia ile, linda ndoa ile, kanisa lile na watu wako katika jina la Yesu Kristo mwana wako aliye hai, naomba mapenzi yako yatimizwe usiruhusu shetani akavurua amani yetu iliyopo katika tumaini lako, ee Mungu tuongoze, tutetee, tubariki, tuzidishie upende na imani yupate kutenda kwa upole kiasi, na kukemea katika jina la Yesu Kristo, ee Mungu ujumbe huu ukawe mwisho na mwanzo wa maisha mapya ya kukutumikia wewe kwa mtu huyu anaesoma. Ee Mungu asanteh kwa uaminifu wako katika jina la Yesu Kristo. Amina

Denis Lyamuya
0655925993
denislyamuya@gmail.com
 
Mwafrika haachi kuwa mtumwa wa watu weupe,hizi dini za watu weupe mbona haijakataza utumwa?saa zingine inanifanya niunge mkono kinachoendelea libya na urusi ili mwafrika arudi kuwa na akili timamu,huyo mungu alimsahau mwafrika akasema tuwaamini weupe ndiyo tupate pepo? Utumwa inakuja kwa aina nyingi na hizi dini ni moja wapo.
 
Amina
 
ujumbe wako ni mzuri ila mpangilio uliotumia kuuwasilisha haupo sawa hivyo unachosha kusoma muda mwingine jitahidi kuandika neno/mahubiri haya kwa mpangilio mzuri.. ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom