Sikia hii....!

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Uwepo wa mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume ni kitu cha heri,lakini kwa vile huwa inatokea kutoelewana katika mahusiano hupelekea KUACHANA na kila mmoja anaanza maisha mapya.Kinachonifanya niandike hapa ni yale maisha baada ya wawili waliokuwa katika mahusiano wanavyoishi,utakuta WANACHUKIANA,DHARAU na kikubwa zaidi utakuta mmoja wao ana MTUKANA mwenzie,sasa yote haya ya nini kwanini msiachane kwa amani na ikibidi muendelee kuwa marafiki wa kawaida ili hata siku unapohitaji msaada mkasaidiana.

Mfano,imewahi kunitokea nilikua katika mahusiano na mtu alkini baadaye uhusiano ule ukavunjika kwa vile nilikua bado napenda kuwa na urafiki wa kawaida na mwenzangu nikawa namtumia sms hata kumpigia simu ili kumjulia hali,tofauti na mawazo yangu mwenzangu akawa anani jbu kwa kunitukana na kunitaka nisimpigie simu tena,nilipoona yamezidi nikaacha kumtumia sms na kumpigia.Ikaja siku nikashangaa ananipigia nilipokea vizuri tu katika kuongea naye akasema anashida anataka nimsaidie kwani amekwama,nilijiuliza sana si ndiye yeye huyu aliyekuwa ananitukana na kunitka nisimpigie tena leo hii anarudi anataka nimsaidie.

So ndugu zangu nawashauri mahusiano yetu yanapovunjika tusigeuke kuwa maadui bali tuendelee kushirikiana kama watu waliowahi kuwa wapenzi kwani hujui ni lini utahitaji msaada wake.
 
Sitaki nataka
 
ah huyo hana msimamo tuu. ila ni kweli kwamba hamtakiwi kudharahuliana na kutakanana. cha msingi keep communication to the minimum. mie simtumii text mpaka atakapo nianza ndio nitajibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…