Katika circle yangu, nina atu wengi, ila wa kumpa cheo cha rafiki kiukweli bado, cheo cha urafiki ni kizito mno,
Niliowahi kusoma nao ni wengi sana, kuna kipindi hadi simu ilikuwa kero sasa, ilibidi ni badili laini, shuleni na chuoni nilikuwa mchangamfu, mcheshi, nk hii ilifanya niwe kama rafiki wa wengi, sasa unakuta simu inapiga yan hapo itabidi nitumie zaidi ya dakika kumjua huyo mtu, ninaoendelea kuwasiliana imebidi niwachuje wawe wale ambao walikuwa wanapenda kunisindkiza, kunisaidia, kuninunulia zawadi (hususani mabinti), n.k
Kazini pia nimeenedelea na uchangamf wanfu, hii naifanya iwe wajibu ili kufanya mazingira yawe mepesi, nikikosa kwenda kazini hata siku 1 basi simu zitaiminika, kuna siku sikwenda yani hata dada anliekuwa akileta chai ofisini alinipigia, nlibaki hoi , watu wangu wa karibu kazini ni wawili, wanajua mimi besti yao lakini kiukweli sijawaweka hilo kundi, kwangu nimewaita watu wa karibu na sio marafiki.
Majirani tunafahamiana vizuri tu, misiba nahudhuria, kwenye sherehe pia sikosi, n.k hawa watabaki kuwa majirani tu.