Sijui nifanye nini, naomba ushauri

Chiriku

Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
47
Reaction score
8
Nina mpenzi wangu ambaye tuna mwaka moja nae, juzi nimepigiwa simu na mdada aliyedai kua ni mpenzi wa mpenzi wangu anadai wana miaka minne kwenye mahusiano na huyo mpenzi wangu.

Nilipojaribu kuongea na mpenzi wangu akaniambia na mimi ndio chaguo lake,akasema atanieleza sababu za yeye kuwa na mimi,wakati akiwa na yule mdada,, je nimsubiri anipe sababu au nimteme.
 
Sijaielewa kabisa hii mada
 
Sasa unaogopa nini?si umsubiri akueleze?
 
yani hilo nalo tukushauri? mmh
 

Jina lako lina mashaka!
 

dah!! eti hili nalo la kuomba ushauri..
hiki kizazi asee sijui kinaenda wapi...sasa mkuu, ishu ya kijinga kama hiyo inakushinda kufikiria na kutatua mwenyewe..
 
kwamba bado yupo nae au kamuacha kaja kwako sielewi
 
Wewe subiri uje kupigwa sound na gegedo juu then uone kama unahitaji kushauriwa.
 
Jua hili,na mavuno ya mahindi,vinanifanya nashindwa kuelewa thread,
 
ni kweli kabisa ndio maana nikaja kutafuta ushauri
 
hupendwiiii haa !!!!!
 
Mwanaume malaya huyo...kawapanga foleni...

Subiri kudanganywa tu
 
Kama ulikuwa hujammeza mteme tu, kazi ni kumtapika mwanammme. Unaweza jikuta umetapika utumbo na yeye kabaki kwenye bandama.
 
du nimesoma mara 4, ndio nimekuelewa, aya subiri uongo wake halafu umalizane nae kwa mgegedo wa bardiiiiiiiiiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…