Sijui nichague wapi

Huyo new brand anakupa kiasi gani cha pesa ?
 

Habari Cornath, kwanza kabisa pole na "experience" uliyokutana nayo katika mahusiano, ni vyema ukatambua ya kwamba si kila baya linatokea kwa ubaya, kuna mabaya yantokea ili kutujenga kifikra na kimtazamo. Ningependa kukushauri ya kwamba usiingie kwenye mahusiano kisa unatafuta mtu wa kukufariji nikiwa na sababu kuu mbili. Kwanza itajidhihirisha kwamba wewe ni mchoyo, nasema mchoyo kwa misingi ya kwamba mtazamo wako kwenye mahusiano utakua tu ya kwamba "MIMI" nifarijike, Je! vipi kuhusu mwenzako? Pili utakuwa "dissappointed" zaidi pale ambapo utakutana na mtu hasiyejali mfano mzuri ni huyo aliyekufokea kwa shilingi 5,000 tu.

Ufanye nini basi?

Kwanza jaribu kusahau YALIYOPITA penda na tamani sana ujipende wewe kama Cornath. Tafuta kuwa karibu sana na Mungu wako, penda kuwa mtu wa kusali maana bila msaada wa Mungu ni vigumu kupata ufumbuzi wa changamto za maisha. Vilevile chukua muda wa kutosha kumdadisi mtu na tabia yake nikimaanisha pelekeni urafiki wenu taratibu.
Nakutakia kila la kheri katika mahusiano yako na Mungu akutangulie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…