Najua umeharibu gari yangu umevunja taa sitaki ununue ila nataka uwe mpenzi wangu,yalinitoka macho nikaropoka we si unajua nina mchumba wangu ambae ni rafiki yako akijua!? Akajibu kwa jeuri "utamwambia wewe" kama hutaki lipa.Nikipiga hesabu na hela saivi ilivyonipiga chenga taa ya mark x na fundi rangi lazima 1 mil vinitoke nikamwambia aniache nikajifikilie akasema kesho yaani leo anataka jibu na saivi kanipigia na kuniambia nimkute hotel flani.Sasa kinachoniuma ni usaliti kwa mpenzi wangu afu niliapa sitamsaliti mbele ya huyo huyo anaetaka nikamsaliti na ki uchumi saivi siko vizuri sana. Au mtego yaani ananivuruga huyu mdada.
Nipeni ushauri
Nawasilisha kwenu wana Jf
Assuming ni kweli: Kosa namba moja ulilofanya ni hilo hapo
(bold, red). Kuanzia hapo ilionekana kuwa tatizo kubwa kwako si kutembea naYe (kumsaliti mchumba wako) bali wasiwasi tu kuwa mchumba wako atajua. Kuanzia hapo ndio maana akakujibu kuwa labda utamwambia wewe, ili "kukutoa wasiwasi".
Inaelekea makuzi yako hayakuwa kipindi kile ambacho kutongoza ilikuwa mtihani mzito. Maana ulitegemea matusi au maneno makali sana ukimtamkia msichana habari za mapenzi enzi hizo especially kijijini. Na vitisho vya kwenda kushitaki nyumbani kwao au hata kwenu ukiendelea, jambo hili lilikuwa linakufanya uogope, na uwezekano wa kumtokea tena ulikuwa mdogo.
Ukiona msichana anadai anaogopa mama yake atajua, au aliambiwa na mama yake au dada yake kuwa ataumia, na vijisababu vingine vya namna hiyo ulikuwa unajua moja kwa moja huyo umempata maana kazi kwako ni kumridhisha kuwa anachokihofia hakitatokea.
Kama kweli story yako, na kama kweli huna mpango kula huo mzigo ambao umeshaanza kuusifia kuwa ni zaidi ya mkeo, lipa gharama.
BY THE WAY, GARI YAKO HAINA INSURANCE, HATA THIRD PARTY?