Sijui dunia inaenda wapi!

Wilson Gamba

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
812
Reaction score
888
Sijui tu viumbe au binadamu wa sasa shida nini, dunia imekuwa ya matukio ya ovyo Kila siku, maadili ni shida kwa Kila upande, siyo Rika au umri au cheo, tuombe tu Mungu maana familia zimejaa shida za malumbano, ubabe na majigambo.

Mungu atupe tu upendo na tuiombee dunia irudi kwenye maadili ambapo binadamu waliishi kwa upendo na kueshimiana, hata haya matukio ya urusi ni matokeo ya Aya Aya tu kwani binadamu wa sasa Hana huruma kwa mwenzake. Tuiombee dunia.
 
Kipato kimekuwa cha shida sana siku hizi tofauti na zamani kila mtu anatoka kutafuta hela watoto wanabaki wenyewe ni mungu tu ndo atakiokoa kizazi hiki ila kimeshapotea tayari.
Ndugu umewaza vema tatizo ni kubwa dad sijui watoto wetu watakiwa ktk Hali gani
 
Acha lomolomo sema kimekukuta nini wewe..
 
Hivi wale kina Bushman walikuwa wanavaa kwa kujisitiri..?
Ukisema uchimbe Sana haya maswala ya uvaaji utakuja kujua huko zamani walikuwa wanakaa utako njenje!
Kwahiyo unataka kusema miaka ile level ya kistaarabika na sasa ni sawa.
 
Mbona ndio kwanza kumekucha..na mbaya zaidi hakuna kurudi nyuma tena.

Mwaka wa shetani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwahiyo unataka kusema miaka ile level ya kistaarabika na sasa ni sawa.
Nataka kusema kukaa uchi ni asili yetu hivyo asishangae sana haya mambo yanaunyama wake na unyama wenyewe ndo kina sisi na sisi ndo wakuyaenzi.
 
tatizo ni wale watoto wa masingle mother wamekuwa wakubwa
 
Tatizo ni sisi wazazi unakuta mtu anajifanya yuko busy sana yy anaona sifa kurudi saa nne saa tano usiku nyumbani kwake na asubuhi anaondoka saa kumi na moja ukiuliza yuko busy hana mda wa kujua watoto wake wanaishi vip yy anajua wakila na kuenda shule ndo katimiza waj8bu wake huu upuuzi usipokemewa tunazaa kizazi kibovu sana kwa nn mda wa kwenda bar ama kwa michepuko tunao ila mda wa kukaa na watoto hatuna ...wakuambie changamoto zao uwasikilize na ujenge uhuru wa wao kukuambia jambo lolote linalowatatiza na hakikisha unawasimamia kwenye maswala ya dini ...
 
Mkuu, najaribu kuwaza, unalinganisha binadamu wa sasa na wa kipindi gani hasa. Wa miaka ya 90s 70s 60s au kabla ya Uhuru? Au wa kwenye vita za dunia, enzi za biashara ya utumwa, zama za chuma au zama wa za mawe?

Amini usiamini, binadamu na dunia ni salama zaidi leo kuliko ilivyokuwa hapo zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…