Ushimen
Platinum Member
- Oct 24, 2012
- 44,836
- 113,220
Mwana umenipumbaza, nikabaki siamini,
Ubozi umenijaza, nisielewe kichwani,
Upofu umeniweza, ila yako siioni,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Sauti yangu hupaza, sifa zako kuzighani,
Ninaimba kutangaza,hadharani na makani,
Nasifu yanopendeza,hata chuku na utani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Uchao nakutukuza, wengi husema u duni,
Kukupenda najikaza, napuza wao uneni,
Kuchukia sijaweza, nijifanye sikuoni,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Katu sijakupoteza, ungalimo kizimbani,
Naapa sitokutweza, nikutie matesoni,
Mengi nimeyachunguza, kubekua hadharani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Upendo sijapunguza, nikuoneshe hufani,
Mwengine hajatokeza, ajifanye majinuni,
Ajapo taona kiza, dole liwapo kinywani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Makini hunisikiza, ukabaki u moyoni,
Mema unanieleza, yakaselea bongoni,
Kwema takuelekeza, uwe wangu maishani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Ubozi umenijaza, nisielewe kichwani,
Upofu umeniweza, ila yako siioni,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Sauti yangu hupaza, sifa zako kuzighani,
Ninaimba kutangaza,hadharani na makani,
Nasifu yanopendeza,hata chuku na utani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Uchao nakutukuza, wengi husema u duni,
Kukupenda najikaza, napuza wao uneni,
Kuchukia sijaweza, nijifanye sikuoni,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Katu sijakupoteza, ungalimo kizimbani,
Naapa sitokutweza, nikutie matesoni,
Mengi nimeyachunguza, kubekua hadharani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Upendo sijapunguza, nikuoneshe hufani,
Mwengine hajatokeza, ajifanye majinuni,
Ajapo taona kiza, dole liwapo kinywani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!
Makini hunisikiza, ukabaki u moyoni,
Mema unanieleza, yakaselea bongoni,
Kwema takuelekeza, uwe wangu maishani,
Siku zote nakuwaza, sijui umenipani!