Sijisikii kumpenda tena, lakini namuonea huruma kumwacha

Bora umwambie mapema, coz itamuuma zaidi ukimuweka wazi na wakati huo umeshampotezea muda wake mwingi tu. ingawa hata sasa ataumia ila at least baada ya muda atarecover.

Ila wewe pia uache tabia ya kukurupuka ndugu!!sasa ukienda huko marekan kama ni kweli ndo ukapagawe zaidi uchezee akili na hisia za wadada uone watakavyokutungua shaba!
 
Watu wamekuwa wabinafsi na wanao jipenda wenyewe haipendezi kwa kweli,ebu fikiria ungekuwa ndio wewe baada tu ya kuambiwa unayotaka kwenda kumwambia huyo bidada ungeuanzishia uzi,kila neno baya ungesema juu ya wanawake
 
Nje anaenda kusoma kiswahil au.??!!!.. mana uo uandish wake unakaa dk 20 nzima unasoma... we bak bongo tu ...
 
kamwe usimwache mwanamke anayekupenda.. hautokuja kumpata kama hyo wa kukupenda hvyo maisha yako yote.. n bora zaid kupendwa kuliko kupenda usipopendwa.. umesema anajiheshmu sana.. ndo kigezo kikubwa cha mwanamke bora.. utakuja kumbuka maneno haya nayokwambia..
 
Mapenzi ni zaidi ya uyajuavyo! mapenzi yanaumiza sana hasa kwa umpendae halafu yeye hakupendi! bora umwambie ukweli kuwa humpendi kabla hajafikisha age 30 huku akiwa na matengemeo kuwa ukirudi zako US mtafanya mipango ya ndoa kumbe unamsababishia msiba mkubwa ndani ya moyo wake! na malipo ni hapahapa duniani
 
Kuacha,kuachwa na kuachana ni kawaida kwenye mahusiano kama hisia zimekata mwambie mapema na usisema hauna sababu hiyo ulioitaja ya kutompenda tena ni sababu tosha muhimu kaa nae mueleze hakuna mapenzi ya upande mmoja,nilishawahi kuachwa kwa kuambiwa kwa utaratibu tu na mpaka leo binti kawa mshikaji wangu iliniuma mwanzoni ila nilimuelewa na kuheshimu maamuzi yake.
 
Ukiendekeza mahusiano ya jinsi hii utaharibikiwa zaidi katika maisha yako, note the following
1. Umekaribia miaka 30, unapoomba ushauri uwe wazi zaidi. Una miaka 20, 25, au 29.9?
2. Uliihisi kupenda, mapenzi ya hisia huwa ni fake. Kwa hiyo hukumpenda
3. Roho inakuumaje wakati moyo imekataa kabisa
4. Hukumpenda toka mwanzo ndio maana hukumshirikisha mipango yako mfano safari ya nje
5. Ulikuwa na kiherehere gani cha kumtambulisha kwa wazazi wako wakati mapenzi yenyewe yalikuwa ya kuhisi
6. Tukushauri nini wakati umeisha fanya tayari maamuzi ya kumuacha? Au ulikuwa ukimaanisha tukufundishe jinsi nzuri ya kumuacha?

Sikiliza kijana hao waliokudanganya utapata uraia marekani kwa kuoa wanigeria amekudanganya. Tafuta naisha hapa bongo ujiandae kwa maisha ya baadaye. Halafu kutongoza sio lazima utumie gia ya kuoa.
 
kamwe usimwache mwanamke anayekupenda.. hautokuja kumpata kama hyo wa kukupenda hvyo maisha yako yote.. n bora zaid kupendwa kuliko kupenda usipopendwa.. umesema anajiheshmu sana.. ndo kigezo kikubwa cha mwanamke bora.. utakuja kumbuka maneno haya nayokwambia..

umenena mkuu...nakuunga mkono kabisa.Na ilishawahi nitokea mpaka leo najutia...
 
sie wanaume ni janga la kitaifa, mtoa maada amethibitisha hilo

Yani bora hata kumuelisha mwanamke kuliko nyie viumbe eti huyo naye msomi anaenda nje kujiendeleza,

1. hajitambui
2. hajithamini
3. hajui kuandika
4. anapeleka majanga huko anakoenda kujiendeleza na madomo nje ya nchi (marekani) - penye red nimenukuu
 
Hakuna mapenzi mabaya kama yakumouonea huruma mtu kwasababu unakuwa unajitesa na pia kuna muda utamtesa huyo unayemuonea huruma
Inawezekana ulikuwa unamchukulia kama crush but she took it serious.Mwambie ukweli dada wa watu kuna watu wanadeserve upendo wake and they will treat her better
 
Nimekusoma ndugu..hii issue iko complicated kidogo..nina experience na kitu kama hicho ingawa in reverse..kuna msichana mmoja mwenye asili ya ki-asia aliwahi kunitamkia bayana kuwa ananipenda na mimi sikumkatalia maana by that time nilikuwa single..tuliendelea na baada ya miaka kama mitatu kasoro kidogo alinifuata na kuniambia bayana "look love, we've been together all these years and you never did put a foot wrong..lakini nemo, to tell you the truth I have grown out of love for you..hujafanya kitu kibaya but that is the way I feel, cant force my hert and please try to understand that there is no other man"

Unajua nini nilifanya? nilimuelewa, that day tuli-do kwa mara ya mwisho then tukabaki casual friends till now.

Ushauri wangu ni kuwa mwambie kabla hujaondoka asijedhani umekutana na rihanna huko..mwambie ukweli na jitahidi kumplease awe mwelewa..may be atakuelewa..asipokuelewa thats her loss...always ukifanya kitu katika misingi ya ukweli utabaki kuwa na amani ya moyo no matter the repercussions.

mtoa mada angetumia huu ushauri.
 
Nmekuelewa sana mkuu
 
Huyo umemtumia muda wote huo unategemea aolewe na nani,wewe ni mchafuzi na nakuombea na wewe uoe changudoa,mnaleta vitamaa vyenu vya mapenzi vikiisha mnajifanya upendo umekwisha,hivi baba yako angemfanyia hivyo mama yako wewe leo hii ungekuwepo? Umefanya kosa kubwa sana be responceble
 
Interejensia yangu inaniambia kuwa pamoja na umri wako kuonyesha kuwa ni mtu mzima...lakini bado una akili za kitoto....bado una mawazo ya kivulana....akili yako haijakomaa hadi kufikia hadhi ya kuitwa mwanaume katika kundi la wanaume.....ni dhahiri kuwa maamuzi yako ya kimapenzi yanaamuliwa na msisimko wa viungo vyako vya uzazi na sio utashi wa moyo wako.....hujui maana ya penzi na huna dira kwenye mapenzi na kibaya zaidi hujali wengine...mithiri ya mtu aliyewasha moto huku asijue aufanyie nini ili kuni au mkaa unateketea..hili sio jepesi kama unavyofikiria....linaweza likakuletea laana katika kipindi chote cha maisha yako kwa sononeko la huyo dada....kwa kuendekeza tamaa zako za viungo vyako vya uzazi ndio maana mpaka leo upo nae hali ya kuwa umekiri kuwa humtaki na huna mapenzi nae wala moyoni mwako hayupo...huo ni unafki...na unafiki ni dhambi na muumba atakulipa kwa dhambi hiyo......wakati mwingine si kila hitaji la mwili linatakiwa litimizwe.....wakati mwingine tunapaswa kuyashinda majaribu hasa yale yanayohusu ngono......kwani ni hatari sana kuuwasha moto wa mapenzi katika hali ya masihara....ni hatari kwa kuwa kwenye penzi ndio kwenye furaha na faraja ya kweli....kwenye penzi mtu yuko radhi hata kujitenga na nduguze....ilimradi tu apate kuwa karibu na anayeugusa moyo wake......sasa inakuwaje kwa huyu ambaye amejitoa kwa kila kitu na hata kugombana na wapendwa wake katika harakati za kutetea penzi lako la kinafiki alafu aje ajue kuwa ulikuwa unamuongopea.......ulikuwa unamfanya kama kikaragosi kwenye luninga....ulikuwa unamuangalia kwa jicho la
dharau.....juhudi zote alizo zionyesha juu yako zimekuwa bure kabisa.....bila shaka ni jambo lenye kutia uchungu na

hudhuni ndani yake....ni jambo ambalo litapelekea mtu kuchukua hatua mbaya na kuyaharibu maisha yake kabisa

kwa sababu ya uongo wako wewe.......kwanini uuwashe moto wa mapenzi pasipo na maandalizi ya
kuumudu...??......SHINDA MOYO........
nmekupenda bure
 
Umenikumbusha wimbo wa mwana mama Celline Dion; "When the wrong someone love you right"
Kiukweli itamuuma ila,remember when you say i love you,you're making a promise with someone's heart,usimpotezee muda mwambie ukweli atulie atampata anayempenda.
 
Back
Top Bottom