Asalaam Aleikum!
Bwana Yesu asifiwe!
Nilimpenda sana kaka mmoja aliyekuwa mwalimu wangu, kumbe na yeye kwa wakati huo alikuwa ananipenda ila hakutaka kuniambia. Tuliheshimiana sana pia tulikuwa marafiki sana. Baada ya kumaliza chuo niliondoka mkoan hapo lakini nawasiliano yaliendelea, hapo ndipo alipoanza kusema lake la moyoni.
Woooh, nilifurahi sana na kujisemea moyoni ulikuwa wapi? mawasiliano yaliendelea kuwa mazuri zaidi na zaidi, baada ya mwaka nilikwenda kumtembelea ila sikufika anapoishi kwani nilihisi kwa jinsi ninavyomfeel na yeye anavyonifeel tunawezajikuta tumeishia kubanjuja. Nilifanya hivyo kila mwaka nilipopata likizo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Tulizungumza mambo mengi hasa kuhusu kuanzisha familia na alionekana kukubali,mwaka wa nne tulianza mapenzi rasmi nikiamini kuwa tunaelekea kuanzisha familia kwani ni muda tosha wa kusomana tabia (hayo ndio yalikuwa mawazo yangu) baada ya miezi minne ya mapenzi motomoto alianza kubadilika, mara hapatikani siku nzima ukimuuliza anadai simu haikuwa na charge, mara line iliblock na sababu chungu nzima.
Kwa vile sikuwahi kufika kwake niliamua kufunga safari na kwenda mpaka ofisini kwake, nilichoambiwa ni kwamba kasafiri kwenda mkoani anakaribia wiki, kabla ya hapo alikuwa na wiki nzima hapokei wala kujibu sms zangu na hatukuwa tumegombana. Nilichukia na kumuandikia sms kali ya kusitisha uhusiano. Nahisi alishukuru sana kwani hakujibu kabisa. Na uhusiano tulikuokuwa tumeudumisha kwa muda wa miaka minne ukaishia hapo....
Ilikuwa ni mwezi wa tano tangu nimeachana na huyo kaka. Ilipofika mwezi wa nane nilipigiwa simu na kaka mwingine niliyesoma nae course flani miaka ya nyuma, wakati tunasoma alinidatilia sana ila sikumkubalii. Alinikaribisha kwake nikamuhaidi ningeenda wiki iliyofata, kweli nilienda tuliongea mambo mengi hatimaye tukaanza uhusiano, baada ya mwezi tukapeana maraha. Kiukweli ndani ya mwezi kabla ya ku-do alinicare sana. Outing kibao, shopping za kufa mtu n.k.
Ila baada ya ku-do tu mapenzi yalipungua hatimaye nilimchukia sana na mapenzi yakaisha. Huyu wa mwisho sasa yeye nilimzungusha kwa muda wa miezi sita baadaye nikaamua kujilipua nikampa tundi... Weee yan yeye alikuwa akijisikia ndio ananitafuta "wewe uko wapi nikufate" akinifata ni direct kwake ku-do tu. Baada ya hapo anaweza asipokee simu au asijibu sms. Na ikitokea kajibu jua kuwa anahitaji. Ukisema basi tutoke tukazungumze kuhusu mahusiano yetu anadai yupo busy.
Je nifanyeje, mapenzi kwangu yamekuwa shubiri, ni miezi miwili sasa mawasiliano yamekatika baina yangu na boyfriend wangu wa mwisho. Je nimekuwa rahisi sana? Lakini mbona nachukua muda mrefu kukubali kutoa tundi labda ungesema ni Easy Going? Msaada wenu ni muhimu kwangu. Samahani kwa maneno mengi. Ahsanteni.
sorry to say this!
ukiamua kukubali mtu kubali kwa moyo tu!ukiamua kukataa kataa mwanzo mwisho!
bahati mbya wanaume unaowavulia pichu unawavulia baada ya kuwaweka muda mreeeefu matokeo yake wakija kukupata tayari wana hasira za kuzungushswa hivo pengine muda ulioamua wewe kurudi yeye tayari ana mtu wake na since unakirudhisha mwenyewe wao wanamega wanasepa!
its like wanakutia kukukomoa sio kwamba wanahisia kweli!
WAY FORWARD
1.hebu jikubali kwanza na utambue mwanaume kwako ni wa aina gani!(vigezo vyako vya kudate mtu mpaka mpeane maraha huwa ni vipi)......................hii itakusaidia kuwa na maamuzi at hand huyu ananifaa fine hanifai tupa kule(for good)
2.jipe muda wa kujitambua wewe ni mwanamke wa aina gani................hii itakusaida kujjifahamu kike hasa na kuset ur principles if not boundaries
3.tambua na ukubali si wakati wote mwanaume akikwambia anakupenda anamaanisha wengine neno anakupenda wanamaanisha "kichupa kimejaa unaweza kunisaidia kipungue" .....................hii itakusaidia kutokulazimika kuvua pichu iwe ni mapema au baadae sababu tu mwanaume amekwambia anakupenda
4.fanya wengine watambue haiba yako,si kila mtu akuone anaweza akawa na wewe!wajichuje wenye huko huko kabla ya kuja kwako!......................hii itakusaidia kupunguza risk za kuanguka kwa mtu ambaye hudhani kuwa perfect kwako
5.JIKUBALI kuwa wewe ni wa pekee na upekee wako haubebwi na utambuzi wa mtu mwingine UPO NDANI YAKO!
UMEANGUKA,SIMAMA,FUTA VUMBI,TAZAMA MBELE,ISHI!
all the best!
...samahani,(km ni mkristo)naomba ukaombewe....
ahsante!Hapa umemsaidia kila atakayesoma ulichoandika, hata kama bado hayajamkuta.
Nahisi kuna mtu unataka kumrithi, maana dalili zote naziona, ngoja nkachukue ushauri kwa Kongosho!
Dada yangu pole sana. Nimesoma maelezo yako na kugundua jambo fulani, yawezeka ikawa ngumu wewe kulitambua. Wako wengi walioumizwa kama wewe, na wengi wanaona haibu kujilipua kwa sababu nafsi inawasuta. Lamuhimu ni kujipanga upya, kwani tayari umeisha gongwa na nyoka, tena mwenye sumu kali, kwa sasa UKIGUSWA NA JANI TU...
Mungu pekee anayetuwazia mema anajua ni lini atakupatia mwenza wako so ishi inavyompendeza Mungu jaribu kushika neno lake na kulitii! Yeye peke yake ndio msaada wako! Atakufundisha ni wapi umekosea na ufanye nn ili ujirekebishe! Kuw na imani na usonge mbele.Jaribu kuhudhuria kwenye seminar za vijana kwenye makanisa utajifunza maisha ya ujana na Changamoto zake. Kingine kama unasoma soma kwa bidii au ni kazi fanya kazi kwa bidii usiangalie wapi ulipoangukia mtazame Yesu kristo mshauri mkuu anajua Mawazo yako na atakusaidia, you are so beautiful you deserve much better!
...samahani,(km ni mkristo)naomba ukaombewe....
Mapenzi hayana formula jamani. Cha msingi kwa sasa usifanye maamuzi yoyote ya mausiano tulia kwanza cse stress zinachangia kufanya maamuzi yasiyo sahihi.
Na tunapo anzisha mausiano kila mtu anakua na mtazamo tofauti possibly ukawaza ndoa lkn mwenzako akawa ki ngono zaidi. Usikate tamaa cse ujaumbwa kwa bahati mbaya package yako ipo.