Wakuu,nalazimika kujibu,ingawa ni kwa ufupi,mwanaJF mwenzetu
Troll JF aliyenituhumu kuwaunga mkono na kuwatetea mafisadi.
Kwenye Jukwaa hili la Siasa,mwanaJF huyo amenituhumu mimi pamoja na Mkuu
barafu kumtetea na kumuonea huruma Mzee Rugemalila wa Escrow.
Pamoja na kwamba nimemjibu kwenye uzi wake huo,niwieni radhi ili nami nimjibu na kumtaka alete ushahidi wa anachokidai hapa. Nasema, with confidence,sijawahi wala sitawahi kuunga mkono au kushiriki kwenye ufisadi. Siivi na mafisadi,waropokaji,matapeli na wapotoshaji.
With due respect, Mkuu
Troll JF huwa hana uwezo wa kusoma na kupambanua hoja tuziletazo. Kwakuwa amejaa uchama na kujianika kama kada mtiifu wa CCM,hukurupuka na kupotosha mada.
Binafsi,nimezungumzia suala la Escrow mara moja tu. Tena,ni juzi tu ambapo Mbunge Ngeleja alirejesha mgawo wake wa milioni arobaini toka kwa Mzee Ruge. Hoja yangu ilikosoa timing na sehemu alipozirudisha pesa hizo na athari kwenye kesi iliyo mahakamani. Sikutetea wala kumuonea huruma fisadi.
Tangu utoto wangu,na aina ya maisha niliyokulia,nachukia na kujitenga na wizi,ufisadi na jinai yoyote. Lakini,napenda mno kusema ukweli na kuwa huru kimtazamo. Dhana hiyo ya kuwa huru imenizuia kuwa na chama cha siasa kama mwanachama wake hadi sasa.
Namuomba na kumshauri
Troll JF alete hapa ushahidi wa alichokidai. Pia,namshauri awe anasoma hata kwa kusaidiwa mada niziletazo zenye uhuru na ukweli. Tena,asiwe analeta siasa kwa kila jambo. Mwisho,namsihi kuepuka kulazimisha uadui au urafiki.