Sijavuliwa uanachama wa CHADEMA, Mimi ni mwanachama halali!

Status
Not open for further replies.
Acha Usalia nenda tu, CDM ina hazina kubwa ya viongozi.

Mwanamke kama hataki basi mwache aendezake.CDM hutakiwi.

Nashangaa hawamkubali Heche, hawamkubali Dr. Slaa lakini hawataki kuhama chama, kama hamtaki tiini hiyo mamlaka iliyo juu yenu kwa manufaa ya taasisi mnayodai mnaipenda chadema, hadi hapo watakapo acha uongozi, bila hivyo mtabakia kuoneka watu wa ajabu tu ndani ya chadema, na mtaisihia kutimuliwa kwa aibu!
 
HABARI.

UFAFANUZI WA UPOTOSHAJI.

kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipigiwa simu na kutumiwa MESEJI kuulizwa juu ya habari za kuvuliwa kwangu uanachama wa BAVICHA na CHADEMA.

jimboni kwangu KIBAHA wamefikia hatua ya kuzusha kuwa NIMEHAMIA CCM na sasa kuna vikundi mbali mbali vya wananchi wanajadili kwa mitazamo tofauti tofauti.

naomba niwaambie leo hapa:
SIJAFUKUZWA CHAMA, mimi ni MWANACHAMA HALALI WA CHADEMA. na wala sijawahi kuitwa wala kuhojiwa na mamlaka yoyote ya chama iliyopewa haki na katiba ya chama kuweza kumvua mwanachama uanachama.

kikubwa kuelewa taarifa hizi zinazosambazwa kwa kasi ya ajabu ni za kipotoshaji zenye lengo la kunichafua kisiasa.

hakuna tangazo lolote so far lililotolewa na CHAMA mpaka sasa linalosema nimefukuzwa uanachama.
ni kweli jana nilialikwa kwenye kikao cha kamati tendaji ya BAVICHA, lakini sijaandikiwa kwenye barua yangu ya mwaliko kuwa nimekwenda kuhojiwa ili nifukuzwe chama.

yawezekana waliokuwa kwenye hicho kikao wanasambaza habari hizo, lakini ukweli ni kwamba.

BAVICHA hawajawahi kupewa mamlaka na katiba ya chama chetu kuweza kumfukuza mwanachama uanachama. cha kuzingatia tu kujua ni kuwa mamlaka pekee za chama zenye kuweza kunivua uanachama ni TAWI LANGU ama KAMATI KUU YA CHAMA.

na ili vyombo hivyo viwili vinivue uanachama ni lazima taratibu za kisheria zilizowekwa kwenye jatiba ya chama chetu zifuatwe. taratibu hizo ni pamoja na kuandaa mashtaka, kunipatia hati ya mashtaka kwa maandishi katika kipindi kisichopungua wiki mbili na kuyajibu kisha kuitwa kwenye kikao cha mahojiano.

nasisitiza BAVICHA hawajawahi kunipatia hati yoyote ya mashitaka na sijawahi kuhojiwa. hizi tuhuma zinazowekwa humu mitandaoni tena kwa lugha za kejeli ni za kuzipuuza.

BAVICHA wangeweza kuwa na uwezo wa kunivua uanachama wa BAVICHA na sio uanachama wa CHADEMA, bahati mbaya sana mpaka leo hii hakuna hata mtu mmoja ambaye ni mwanachama wa BAVICHA wote waliokuwepo humo ni sehemu tu ya wanajumuhiya ya wanachadema wenye rika la umri unaolingana.

kwa hiyo taarifa zozote za kuwa mimi nimevuliwa uanachma na BAVICHA chini ya ndugu HECHE ni za kipotoshaji na hazipo.

Mimi ni MWANACHADEMA halali na nitaendelea kukitumikia changu mpaka hapo itakapokuwa vinginevyo.

sijawahi kuwa na KADI YA UANACHAMA WA BAVICHA hivyo siwezi vuliwa uanachama wangu wa chama kwa kuzingatia umri wangu.

nimeshaandaa malalamiko kwa viongozi wangu wakuu wa chama juu ya upotoshwaji huu unaofanywa na kwa makusudi na baadhi ya viongozi wa BAVICHA katika kile wanachokiita kujihami na uchaguzi ujao wa chama.

Nafikiri sasa ni kilio na kusaga meno.......sio zaidi ya hapo! Hao masalia inabidi wajifunze kuwa kilichofanyika juu yao kiko inline na snowball philosophy......which goes......'Don't let a small snowball become a big snowball, once you see a snowball you just melt it'
 
Mkuu Mwita Maranya,Nimependa signature yako. Ni yako au umeipata sehemu?Kama kuna msaliti hapo chadema na yuko hapo kimaslahi aanze kuchapa mwendo as Mungu yu pamoja nasi.
 
angalia SURA YA TANO ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006,ktk subtitle inasema KUKOMA UANACHAMA
labda nikuwekee nini kipengele hicho kinasema
5.4 Kukoma kwa UanaChama
5.4.1 Kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.
5.4.2 Kutokana na kufariki.
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa
katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo
usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama.
Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na
adhabu hiyo.
5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama
kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.
5.4.5 Kukosa sifa za uanachama.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa
nidhamu.
Hivi watu mnajifanya hamuamini hivyo vifungu hapo juu ama? tangu jana vimewekwa hapa lakini watu bado mnauliza

Kama kuna mtu aliwalisha matangopoli kwamba Bavicha haina uwezo wa kufanya maamuzi kama hayo ndo mjue imekula kwenu
 
Waku nadhani ni wazima na mnaendelea vizuri na ujenzi wa taifa letu! Wana jf nimeona leo tujadiliane ili tuweze kuujua ukweli,maana suala la kufukuzana uanachama kwa vyama vya siasa imekuwa ni changamoto sio kwa vyama vya upinzani pekee,hata chama tawala.naomba kwa kuanza tuanzie kuitazama katiba ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA, naomba wana jf tujadiliane kwa uwazi na ukweli ili tuweze jua nani/chombo gani chenye mamlaka ya kumvua uanachama wa cdm ndani ya chama hicho?. Hoja hii haimlengi yeyote lengo ni kujua ukweli ili wale waliopo chadema ama nje ya cdm waweze kuondoa hiyo sintofahamu vichwani mwao! Karibuni:

Nani walikuchagua si hao BAVICHA sasa kama wamekuona umekuwa kimeta kwa nini wasikuvue na kukuondoa usije ukaua wengi unashangaa nini?
 
Unajua ukijaribu kuangalia kiburi cha hawa vijana utamkumbuka mtu alikuwa anaitwa Kafulila.
Kuna jamaa alimfanya Kafulila akawa na kiburi sana ndani ya CDM kwa ahadi ya kumsaidia lolote likitokea. Kweli Kafulila akawa demoted kwa hasira akaachia chama akasaidiwa na ZZK kuwa Mbunge. Ninawasiwasi kama kiburi cha hawa kina Mchange hakijengwi na ZZK kuwa yeye anaubavu wa kuwasaidia hata wakitoswa.

Matatizo haya sasa yanakuwa na fedha chafu tayari zinazunguka. Kama chama sidhani kama kuna muda wa kuendelea kulea viongozi wenye kutengeneza dhahama badala ya kazi. Maendeleo hayajawahi kuja kwa kumbembeleza mtu yeyote. Na mabadiliko ya uchumi hayawezi kuja kwa kufumbiana macho zaidi ya kuelezena ukweli.

ZZK lazima aache kuwashawishi hawa vijana ili wafanye kazi nao waje kuwa na mafanikio kama yake, ni dhambi sana kuwatenga vijana na yale wanayoyapenda na ukatumia udhaifu wao na njaa zao kuharibu future zao. Ninaamini kabisa kama sio kufuata wale waliokuwa wanawaamini wasingejikuta kwenye hili shimo leo.

Hakuna mtu ameweza kushindana na chama chake akapona labda kama chama chenyewe kinakufa. Misimamo na maadili ya chama si ya kuchezea. Hata kwenye nchi zilizokomaa kidemokrasia hawachezi. nakumbuka Leberman wa kule Connectcut alitoswa na Democrat baada ya kusaliti maamuzi.

Wasio, binadamu fanya kazi kwa bidii heshimu viongozi wako hata kama hamkubalia jengeni hoja onyesheni mnaowatumikia kuwa ninyi ni bora zaidi ya hao mnaohisi hawafai wananchi ni waamuzi wazuri sana. Na huko mnakokwenda msimwige Kafulila kwani mnaweza kujikuta mnafukuzwa kila mahali ikawa kama mikosi. Msisikilize tena aliyewafikisha hapo mlipo kwani hiyo tabia ya usaliti kuna watu wamezaliwa nazo. Jifunzeni kutumia akili zenu badala ya kutumika. Kazi tu ndio kipimo cha utu majungu hayajengi, ghiliba hazifai, wivu usio na tija hauna maana, wala kufuata wenye tamaa mbaya hakufai.

Poleni kwa yaliyowasibu, msilie mmevuna mlichopanda. Sasa kuweni waungwa tutajieni vinara wenu wote na wale waliokuwa wanawapa fedha, matumaini na mbinu chafu. Tuelezeni nia yenu ilikuwa nini na mipango yenu.

Viongozi mnaopata madaraka msiwe wamimi na kuwatumia vijana kama tissue.
 
Vipi kuhusu wao kutetewa na wewe adui wa CHADEMA?

sina haja ya kuwa na credibility kwa maadui.It's worthless...!

You keep talking about non-issues like personal "credibility" because you cannot engage in logical discussion.

What would you say about your own credibility? I recall you were one of the loudest making the claims and hurling Rhetoric hogwash against CHADEMA.Your previous posts and history on JF speaks louder ......

Keep to the topic, defend your arguments (if you've got some) and forget about credibility, you will not do very well on that scale.

Wabongo bana,
Kwani mpaka uongee kiingereza ndiyo akuelewe.

Si uongee tu kiswahili ambacho ni lugha ya taifa hata wazee wetu ambao hawakubahatika kupata elimu ya mkoloni au kutembea kama sisi kwenye nchi ya wenye lugha wapate kukuelewa.

Ni ushauri tu.
 
Leo mbona wapole? Tukaneni basi ili tuone jeuri yenu! Kumbe na nyie mna hadabu kidogo! Sijui ni nani kawafundisha adabu
Hata Kafulila aliijiwa na adabu ghafla tu baada ya kuambiwa anafukuzwa, na alilia kama kitoto cha chekechea. Kwa hiyo hapo sio adabu actually, ni baada ya kuona kuna dalili ya kupigwa chini. Chezeya opportunity wewe!
 
Hivi watu mnajifanya hamuamini hivyo vifungu hapo juu ama? tangu jana vimewekwa hapa lakini watu bado mnauliza

Kama kuna mtu aliwalisha matangopoli kwamba Bavicha haina uwezo wa kufanya maamuzi kama hayo ndo mjue imekula kwenu
kiongozi
BAVICHA inauwezo wa kumfukuza uanachama mwanachama wake kama kifungu hiki kinavyosema "5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa
nidhamu."
na BAVICHA haina mamlaka ya kumfukuza uanachama mtu ambaye ni mwanachama wa CHADEMA.

landa huelewi nikueleweshe nikitumia katiba hii ya mwaka 2006 kama kuna nyingine sijui
ni kwamba,nikiwa mwanachama wa BAVICHA na wakati huo ni mwanacha wa CHADEMA,uanachama wangu unaweza kukoma kama mwanachama wa BAVICHA lakini bado nikawa mwanachama wa chadema
lakini pia kifungu hiki "5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa
katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo
usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama.
Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na
adhabu hiyo."
hakitaji BACHICHA kuwa na uwezo wa kumvua mwanachama uanachama wa CHADEMA,maana imetajwa kuwa TAWI ama NGAZI NYINGINE YA CHAMA na sio ngazi nyingine ya BAVICHA.
NAHITIMISHA
BAVICHA inaweza kumvua mwanacahama wake uanachama wa BAVICHA na sio CHADEMA(hii ni kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006)
 
Komaa mwanangu Mchange, Pigania matumbo ya familia yako, CDM mali ya wote. banana humo humo. Siasa ndiyo zilivyo. penye riziki hapakosi fitina
 
angalia SURA YA TANO ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006,ktk subtitle inasema KUKOMA UANACHAMA
labda nikuwekee nini kipengele hicho kinasema
5.4 Kukoma kwa UanaChama
5.4.1 Kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.
5.4.2 Kutokana na kufariki.
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa
katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo
usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama.
Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na
adhabu hiyo.
5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama
kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.
5.4.5 Kukosa sifa za uanachama.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa
nidhamu.

Hii ya mwisho nimeipenda,wale vijana wachumia tumbo wataondoka na hii!
 
Wabongo bana,
Kwani mpaka uongee kiingereza ndiyo akuelewe.

Si uongee tu kiswahili ambacho ni lugha ya taifa hata wazee wetu ambao hawakubahatika kupata elimu ya mkoloni au kutembea kama sisi kwenye nchi ya wenye lugha wapate kukuelewa.

Ni ushauri tu.

Nikutafsirie?
 
kiongozi
BAVICHA inauwezo wa kumfukuza uanachama mwanachama wake kama kifungu hiki kinavyosema "5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa
nidhamu."
na BAVICHA haina mamlaka ya kumfukuza uanachama mtu ambaye ni mwanachama wa CHADEMA.

landa huelewi nikueleweshe nikitumia katiba hii ya mwaka 2006 kama kuna nyingine sijui
ni kwamba,nikiwa mwanachama wa BAVICHA na wakati huo ni mwanacha wa CHADEMA,uanachama wangu unaweza kukoma kama mwanachama wa BAVICHA lakini bado nikawa mwanachama wa chadema
lakini pia kifungu hiki "5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa
katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo
usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama.
Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na
adhabu hiyo."
hakitaji BACHICHA kuwa na uwezo wa kumvua mwanachama uanachama wa CHADEMA,maana imetajwa kuwa TAWI ama NGAZI NYINGINE YA CHAMA na sio ngazi nyingine ya BAVICHA.
NAHITIMISHA
BAVICHA inaweza kumvua mwanacahama wake uanachama wa BAVICHA na sio CHADEMA(hii ni kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006)

Kiongozi
japo si mwanasheria but nnaufahamu kidogo kuhusu sheria
naomaba ujue kwamba vifungu vidogo vya 5.4 Kukoma kwa UanaChama kama ilivyonyeshwa kwenye katiba vina uzito sawa hivyo basi kifungu
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa
katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo
usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama.
Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na
adhabu hiyo.

na

5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa
nidhamu.

pia kumbuka kifungu namaba
5.4.6 sio kifungu kidogo cha kifungu 5.4.4. Hivi vifungu vyote vina nguvu sawa vyote vinamfukuzisha uanachama mtu
 
Tutamsindikiza Saed Kubenea kwa nderemo kuchukua jimbo la kibaha.
Hivi huyu kilaza yupo?kile ki toilet paper chake{mwanahalisi}wanakifungulia lini jamani?njaa itamuua huyu mpaka anatamani kuingia kwenye siasa na elimu yake ya darasa la pili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom