Siishanglii Taifa Stars ili nione kwa sababu ya unafiki wa wanasiasa

kajunju

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
999
315
taifa sttars ilifuzu miaka 39 baada ya kukaa nje ya uringo wa kimataifa. Baada tu ya kufuzu ndipo tumeona miamba ya siasa chafu za nchi hii wanajitokeza kuikumbatia timu. hapa kuna bashite & co, Ndugai na Nkamia.
nikianza na bashite, yeye ameozi timu kama ya mkoa wa dar (mzizima united) na ndiye alfa & omega. anachokifanya ni kujaribu kutumia nguvu kwa yule anayembeba. hapa naona mbwebwe nyingi, sifa kuwa ndizo zinaweza kuivuusha taifa stars. Napenda nimwambie bashite kuwa mpira ni ssayansi na si siasa kama anavyofikiria. Kuhusu Ndugai nilimsikia akilalamika kuwa kijana bashite hana adabu. najiuliza mwaka huu ndugai ndipo hamejua kuwa serikali kwenye bajeti haiweki ata sh. 100 kwa ajili ya maendeleo ya timu? hapa kila mmoja ndugai na bashite wanatafuta umaarufu. timu ikishinda bashite atasema mimi nimeweka mkakati wa ushindi na ndugai ataonekana alienda na group lake kung'alisha sharubu tu.
kati ya wanafiki wabaya wa nchi hii kwenye michezo no. 1 huwa ni nkamia. nkamia aache habari za vijiweni kuwa zinaenda kuendeleza soka la tz. amemponda kocha lakini nani ameifikisha hiii timu apa ilipo. misri alipelekwa umbea wa kuchunguza kocha kupitia chama cha soka naigeria. kama hawaelewani alitegemea wangemsema vizuri?maneno kama haya aliyosema nkamia kwa kocha Amunike je yamemfurahisha? mtu akiteuliwa baada ya interview siyo watu wote watapenda na mkiti wa naigeria anajua sasa CV ya Amunike imepanda anaweza kutaka kufundisha nigeria au kugombea kiti chake. kuhusu wachezaji wetu, lazzima tukubali kikosi chetu ni dhaifu, watu hawajiamini na hii ni sehemu zote. angalia mawaziri, rais anawateuua baadae analalamika kuwa hawawe kudeliver, angalia wafanyakazi wanaofanya international organisation walinganishe na wenzetu wakenya...Hawujiamini kabisa. haya yote ni mfumo wa elimu pamoja na mtu kutompa nguvu kuwa anaweza. haya ata kwenye michezo angalia mwili wa watz hatujikakamui bali hata tukikutana na wachina, korea ambao ni sidico watatusukuma jitu linaanguka lakini si kwamba halina nguvu bali uoga. Kwa kumaliizia siasa chafu za nchii hii zimeingia kila idara/sekta na hazitatuacha salama. kwenye ushabiki tayari wananchi wameggawanyika kwani wanaona ni timu ya watu furani au mtu furani ndiye mwenye timu na wengine hawafai kabisa. lazima tuje na mpango mkakati wa kutengeneza timu za vijana academies angalau 6 kila kanda zinazoweza kutoa wachezaji wazuri. senegal mwaka 1992 walianda afcon wakatolewa robo fainali. wakati huo walikuwa na wachezaji hakina jelous bokande. baada ya kutolewa walijiandaa miaka 10 na mwaka 2002 walikuwa na vijana wengi wadogo diof, fadiga, cisse & co waliokuwa wadogo wanasaidia na wakongwe wachache. Lazima kama taifa tutoke hapa kimkakati na si hizi mbwembwe za ndugai, bashite na Nkamia
asante
 
Utakuwa umemkomoa nani mkuu
IMG-20190627-WA0005.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom