Siielewi serikali ya Magufuli: Inajali wanyonge, je, wale wasio wanyonge haitawajali?

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,466
Niseme ukweli, nampongeza sana magufuli kwa utendaji wake, ameonyesha mfano wa kuigwa. lakini watendaji wake naona kama siwaelewi fulani hivi. ni kama wametangaza vita dhidi ya wafanyakazi wa serikali vile, kwasababu kwenye hotuba zao zote kwa wananchi wanasema serikali hii inajali wanyonge, je, wale wasio wanyonge haitawajali?,

Pia, kila unakopita ni kwamba vitisho dhidi ya wafanyakazi wa serikali vinafanyika. madaktari wametishwa, manesi wametishwa, sasa kila mtu sasahivi anafanya kazi kwa hofu tu na si kwa adabu, hadi imefika kipindi raia anao ujasiri wa kumpiga daktari ngumi kwasababu amempa rufaa kwenda muhimbili, bila kujua kiutaalamu ni kwanini rufaa hiyo imetolewa. ninapenda kuishauri hii serikali mambo yafuatayo.

1. Serikali isiwagawe wafanyakazi wa serikali na wasio wa serikali.

2. Serikali isiwagawe wanyonge na wasio wanyonge. isionekana inawahudumia tu wanyonge, iwe serikali ya watu wote. hatari ya hapa ni kwamba utatokea uadui kati ya wanyonge na wenye nacho, na wasio nacho watapata hadi ujasiri kuwapiga wenye nacho. siku hizi ukienda maofisi ya umma hasa hospitali ni kawaida kuona raia wanamwambia mfanyakazi "tutakusemea kwa magufuli", wafanyakazi nao wakipata mwanya wanawaambia nendeni mkamwambie magufuli wenu (tumeshuhudia haya). imefika kipindi sasa wafanyakazi hawafanyi kazi kwa utu toka moyoni bali wanatimiza wajibu wakati kazi nyingi zinahitaji utu toka moyoni. daktari au nesi pamoja na mwalimu mfano wanatakiwa kufanya kazi kwa utu sio kwa kulazimishwa au kutishwa kwasababu wakitishwa watafanya kazi kutimiza wajibu tu.

3. Serikali ijue kuwa wafanyakazi ndio wanalipa kodi kuliko watu wote bila kukwepa hivyo isiwachukulie kama wote ni waovu na wavivu.

4. Serikali isifikiri kubana matumizi yooote ndio jibu la umasikini wa tz. inaweza kubana matumizi lakini ikapandisha mishahara na kutoa marupurupu. duniani kote kuko hivyo. wao mishahara hawapandishi, na semina, safari na membo mengine mengi wamebana, hivi kwa mshahara wa serikali nani ataishi hapa mjini?

5. Magufuli ni rais anayetakiwa kuendelea kutawala walau miaka yote 10, lakini wakati akifanya hivyo awe makini. kubana sana matumizi kunawaumiza baadhi ya wafanyakazi, ajue wapiga kura ambayo ni ya siri sio wanyonge tu, hata wafanyakazi ni wapiga kura, na zaidi ya yote, hao wanyonge wengi wanawategemea wafanyakazi katika mambo mengi sana.

MWISHO: Hii nchi sio ya wanyonge/walalahoi tu, ni nchi ya watanzania wote na serikali inatakiwa kujali makundi yote kila mtu kwa nafasi yake, kinyume na hapo unagawa wananchi na serikali inakuwa haieleweki na inaweza isipite baada ya miaka 5.

ALIENDA KIGALI RWANDA: Alipoenda kigali rwanda, kuna maendeleo mazuri, je? kagame amebana sana kila kitu kupita kiasi namna hii au kuna kiasi? kuna vitu vingine ni reasonable kama vile promotion nk watu kupandishwa madaraka kwa wakati, watu kuongezewa posho ili wafanya kazi kwa moyo, watu kupewa marupurupu n.k,
 
Ngoja kwanza magufuli arudishe nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma wakati wakiendelea kuboresha mifumo ya kiutendaji
 
Ngoja kwanza magufuli arudishe nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma wakati wakiendelea kuboresha mifumo ya kiutendaji
mimi simpingi magufuli, kusema kweli anaonekana kufanya kazi kwa moyo wote na ndiye rais wa aina yake tulikuwa tunamhitaji na ninamuombea kwa Mungu. lakini ninampa ushauri tu awe makini, hata baba wa familia ukiwa mkali kama simba tu ndani ya nyumba, watoto watakupenda kinafiki, watakusapoti kinafiki, siku ukipata tatizo wakaona unaweza usisimame tena vizuri wanaambatana na yule wanayefikiri anawasaidia. hii imeleta mgogoro sana. nimeshuhudia wafanyakazi wa serikali wakidharauliwa sana sana mbele ya macho yangu, raia anaenda ofisini halafu anafikiri yupo nyumbani kwake sebuleni anataka ahudumiwa kama mfalme....raia wana majibu mabovu sana kwa kiburi cha magufuli na waziri mkuu.

kutia adabu kwa wafanyakazi wa serikali ingesaidia kama ingekuwa kwa njia ya kuwapeleka mahakamani, sio kuwarukia kwa vitisho mtaani tu kwa tuhuma ambazo hazijathibitishwa. ndio maana raia wanapata hata ujasiri wa kumpiga daktari ngumi sasahivi. hivi unafikiri tanzania nzima kwenye kazi ya wito kama udaktari, kuna daktari anayehudumia kwa moyo/wito? watu wanawaona kila mgonjwa anayekuja kwake hawamuamini wanaona kama either ametumwa au anaweza kuwachoma kwa tuhuma za uongo, hawajiamini na wanahudumia wagonjwa bila kujiamini. maisha gani haya? hivi tukienda jino kwa jino, tutafika?

nilitegemea serikali iwaadibishe wafanyakazi wabovu, lakini wakati huohuo, iwaambie wananchi kwamba wanatakiwa kuheshimu ofisi za serikali, wakienda kule waende kwa heshima, wawaheshimu wanaowahudumia na kama hawatafanya hivyo wataadibishwa.

kilichopo sasahivi kuna uadui mkubwa sana kati ya WAFANYAKAZI WA SERIKALI dhidi ya WANANCHI. upo mkubwa sana sana na tunakoelekea sio kuzuri.na atakayeumia hapa sio mfanyakazi wa serikali bali mwananchi kwasababu mfanyakazi wa serikali ana maeneo mengi ya kutokea, raia bado ana heso hana pa kutokea pingi.
 
Back
Top Bottom