Sifa za mwenza ambaye kwako anakuja kama mzigo badala ya msaidizi

Sifa za mwenza ambaye kwako anakuja kama mzigo badala ya msaidizi

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,147
Reaction score
43,079
Mwenza ambaye anakuja kwako kama mzigo kisha anakuwa anataka kukutumia kwa maslahi binafsi kisha arudiane na ex wake,au atakuacha ghafla bila sababu zozote za msingi huwa mwenye sifa zifuatazo.

1.ANAKUWA ANAPITIA KIPINDI KIGUMU SANA KIFEDHA HIVYO ANAHITAJI MSAADA WAKO TU
Kumchagua mwenza ambaye anakuja kwako kwa ajili ya kupata msaada wa kifedha ni kujichimbia kaburi kwa mikono yako wewe mwenyewe.

Haina maana mwanaume au mwanamke ambaye anapitia kipindi kigumu sana kiuchumi hafai kuwa mwenza Lah bali kuna madhara makubwa kwa kumchagua mwenza ambaye anakuja kwako kutaka MSAADA wa kifedha na faraja.

Angalia mfano hapa chini

Unakutana na mwanaume au mwanamke ambaye amekonda sana, amepauka sana,ananuka jasho,amefubaa, hana dira yoyote ya maisha,analala chini, haogi, hapigi mswaki,anakula mlo mmoja,hana ndugu wala rafiki wa karibu, ametelekezwa na ujauzito au watoto kisha kwa sababu ya huruma yako unaamua kumtendea wema kwa kumpa chakula, kumpa hifadhi ya kulala,kumpa faraja, kumliwaza,kumtia moyo, kumnunulia simu, kumfungulia biashara, kumchukulia mkopo, kumsomesha, kuwasomesha watoto zake ambao ametelekezwa nao,unawasaidia wazazi wake n.k kisha baada ya maisha ya mwenza wako kuanza kuwa mazuri,akianza kupendeza,akianza kusifiwa kazini au masomoni,akianza kupata umaarufu,kupanda vyeo,kusafiri mara kwa mara.

Ghafla anabadilika tabia.Anakuwa mkali kupitiliza kwa vitu vidogo vidogo,anakuona tabaka la chini, anakuona hauna HADHI ya kuzungumza naye,anakutazama kama kinyesi.

Anaanza kubadilisha wanawake au wanaume mfululizo,au anarudiana na ex wake tena kwa kuonyesha dharau, kiburi, jeuri, majivuno,ujuaji,anakuporomoshea matusi ya nguoni.

Ukijaribu kumkumbusha wapi ametoka atasema "SIJAKULAZIMISHA UNIFANYIE YOTE HAYA "
Kisha anaondoka zake.

Kuliko uanze kuwaita wanawake au wanaume wote ulimwenguni kote kuwa ni "mbwa" kwa sababu ya kusalitiwa na mwenza wako ambaye umeteseka sana kumtengeneza aje kuheshimiwa ni bora ufanye uwekezaji mkubwa sana kwako ili umpate mwanaume au mwanamke ambaye hatakuja kwako kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi.

Bora ubebe majukumu yako tu ya kuhudumia lakini sio kubadilisha maisha ya mwenza wako ili aje kuwa mwenza wa ndoto zako.

2.ANAKUWA NA HUZUNI, HASIRA KUPITILIZA,MAJONZI KISHA ANAKUWA ANATAKA FARAJA YAKO TU SAA 24
Mwenza mwingine ambaye katika hatua za awali hafai ni yule ambaye unamkuta hana furaha hata chembe,anakuwa analia sana,anahuzunika,anaomboleza mahusiano kuvunjika au kifo cha ex wake.
Mwenza wa aina hii hafai kwa sababu kwanza utalazimika kumuomba msamaha mara kwa mara hata kama amefanya makosa lengo usije kumtonesha kidonda cha maumivu ya ex wake.

Vilevile mwenza wa aina hii hafai kwa sababu anakuja kwako ili ufanye kazi ya kumfariji, kumliwaza, kumbembeleza ili aweze kumsahau ex wake hivyo kwako anakuwa hana faida yoyote isipokuwa anakuwa anakutumia kama daraja la kurudiana na ex wake,au kumsahau ex wake.

Mwenza wa aina hii hafai kwa sababu muda wote utakuwa unafanya kazi ya kumfariji, kumliwaza, kumbembeleza,kuogopa kukwazana naye,muda wote uwe malaika ili asije kumkumbuka ex wake.

Madhara yake haki zako za unyumba hakupi,muda mwingi anakuwa anautumia kujali hisia zake lakini yeye hawezi kujali hisia zako hata ukiwa mgonjwa mahututi bado atakuwa anahitaji faraja yako.
Hata ukiwa mgonjwa mahututi yeye atakuwa anataka uendelee kumbembeleza, kumliwaza, kumsikiliza,kumpa faraja.

Wanaume na wanawake ambao huwa na simanzi, huzuni, hasira kupitiliza,upweke kupitiliza,hisia za kisasi au chuki dhidi ya wenza wao wa zamani huwa wanasumbua sana.
Wengi baada ya wewe kujitoa mhanga sana,kumpa hifadhi,kumpa faraja, kumliwaza, kumtia moyo akiona ameanza kupendeza,akiwa na hali nzuri kiuchumi zile hisia kwa ex wake zinakuja kwa kasi sana hivyo anaweza kukuacha ghafla arudiane na ex wake bila kujali umehatarisha maisha yako kwa ajili yake.
Wengi utasikia "NATAKA KUMUACHA BILA KUMUUMIZA KWA SABABU SINA HISIA NAYE HATA KIDOGO"

Chagua mwenza ambaye anakuja kwako akiwa na "QUALIFICATIONS" za mume/mke bora wa maisha yako sio mwenza ambaye kwako anakuja kama project kwa maana uanze kumbadilisha tabia ili akupende kama shukurani ya wema wako kwake.

Kabla haujaanza kumfariji , kumliwaza, kumbembeleza,kutaka amsahau ex wake jiulize ye wewe ukiwa na maumivu makali sana ya kuachwa na ex wako je huyo mwanamke au mwanaume ataweza kujitoa mhanga kwako kukufariji ukiona hawezi tambua kwamba hilo ni bomu.

3.ANAKUWA NA TABIA SUGU AMBAZO WATU WENGINE WANAKUWA WAMEMCHOKA
Unaweza kukutana na mwenza ambaye kwako anakuja kwako kama mzigo kwa sababu watu wengine hawamtaki hata kidogo hivyo anakuja kwako kama kimbilio la mwisho.Kwa maana kama akiondoka kwako hana pa kwenda mwenza wa aina hii hafai.
Mwenza mwenye tabia sugu kama wizi,ulevi kupindukia ,uvivu,uzembe,mwenza mwenye hasira kupitiliza,mbabe,jeuri, mwenye dharau, kiburi, majivuno,utemi,mwenza mbishi sana halafu mchoyo sana,mwenza akipata fedha anatumia zote ghafla zinaisha,mwenza anakuwa na ukaribu uliopotiliza na ex wake,(mwanamke) anakuwa na ukaribu uliopotiliza na marafiki wa kiume tu,mwenza haambiliki,hashauriki,mwenza mwenye misimamo mikali sana.

Madhara ya mwenza wa aina hii akifanya makosa hataki uongee chochote,ukifanya makosa ataongea kutwa nzima,au anasusa haongei mwezi mzima.
Utashindwa kuachana na mwenza wa aina hii,utashindwa kukemea tabia zake mbaya,utavumilia makosa yake miaka yote,utaomba msamaha hata kama haujafanya makosa.

Mwenza wa aina hii anaweza kukutukana,kukudhalilisha,, kugombana na majirani pamoja na wazazi wako, anaweza kukugombeza hadharani, anaweza kukushambulia kwa maneno makali sana lakini utashindwa kuachana naye kwa sababu utakuwa umefanya uwekezaji mkubwa sana kwake ili kumbadilisha tabia.

4.MWENZA HATAKI KAZI,HATAKI MAJUKUMU YOYOTE LAKINI ANATAKA KUISHI KIFALME
Mwenza ambaye kwako anakuja kama project anakuwa hataki kazi,hataki majukumu yoyote kazi yake kulala mpaka saa 4 akitoka kitandani anataka akute chai lakini hachangii hata senti tano ya fedha za familia,anakaa akitazama TV muda wote akiwa nyumbani lakini usafi wa chumbani anapolala hafanyi,kutwa kucha kuomba fedha lakini anazipeleka kunywa pombe,kufanya starehe.
Akipewa mtaji anakula,akitafutiwa kazi anatafuta kisingizio cha kuacha kazi,akifunguliwa biashara anakwenda kazini siku mbili biashara imekufa,akiwa na fedha nyingi sana zinaisha haraka bila kufanya kitu chochote cha maendeleo.

(Mwanamke) Hataki kufua,hataki kupika, hafanyi usafi wa nyumba,hataki kuandaa watoto waende shule asubuhi,hataki kutoa unyumba,anakuwa na safari za mara kwa mara kwenda nyumbani kwao kisha anakaa muda mrefu sana kinyume na makubaliano.

Mwenza wa aina hii hafai kwa sababu kama utabeba majukumu yote pekeako yeye atakaa na kufanya starehe tu hajali chochote,ukiongea kuhusu tabia zake anakuja juu kwa jazba anaporomosha matusi ya nguoni,au anafunga mabegi anarudi nyumbani kwao.

UFUMBUZI WAKE
Muweke mwenza wako mahali anapostahili.Epuka kuwa na huruma kupitiliza kwa sababu atakupanda kichwani,wengine ndugu zao huwa wanawaendekeza kwa kuweka visingizio kuwa watabadilika ukiwa mvumilivu sana epuka jambo hilo.

Mwenza wako akiwa jeuri mwambie ajitegemee kwa kila kitu.Akiwa hana HESHIMA mwambie akusanye kila kitu chake aondoke.

Chukua mwenza ambaye mnaheshimiana sio mwenza mzigo.Chukua mwenza ambaye anajua wajibu wake na anajituma kubeba majukumu yake ipasavyo.
Epuka mwanaume au mwanamke ambaye utalazimika kumbadilisha tabia ili akupende kama shukurani ya wema wako kwake.

Mwanaume au mwanamke ambaye hana cha kupoteza kwenye mahusiano huwa anakuwa na kiburi, majivuno, ujuaji, anakuporomoshea matusi ya nguoni,atakuwa mbishi sana,atakuwa haambiliki, hashauriki,atakuwa anakusumbua sana.

Epuka kuvumilia makosa ambayo watu wengine ukiwafanyia watakuchukulia hatua kali sana za kisheria.
-Epuka kusamehe makosa ambayo ukifanya kwa watu wengine watakuchukulia hatua kali sana
-Epuka kuvumilia mapungufu ya watu wengine ambayo endapo ukiwa nayo watakukimbia.
-Epuka kumjali mtu ambaye wewe hata ukiwa mgonjwa mahututi hawezi kujali chochote juu yako.
-Epuka kujitoa mhanga kwa mtu ambaye hawezi kujitoa mhanga kwako endapo utakuwa katika hali mbaya

Jiulize kama ukiwa umekonda, unanuka jasho, umepauka,hauna kazi,hauna biashara,unalala chini,unakula mlo mmoja,unavaa nguo zimepauka je huyo mwenza wako anaweza kujitoa mhanga kwako kukufariji,kukuliwaza,kukuinua kiuchumi kama huyo mwenza wako hawezi kwanini wewe uyaweke maisha yako hatarini kumjali wakati yeye hawezi kufanya hivyo kwako.
 
Nikajua ni kwenye jukwaa letu tu kule la wana-Liverpool fc kumbe na huku. Ubarikiwe kwa somo lililoshiba.
 
Nikajua ni kwenye jukwaa letu tu kule la wana-Liverpool fc kumbe na huku. Ubarikiwe kwa somo lililoshiba.
 
Back
Top Bottom