Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,945
- 4,511
Hapana si wote! mi ninachojua wanawake wengi katika ndoa ni chachu ya mafanikio, sasa iweje wewe ufiche chako halafu cha mwanaume kiwe cha wote! hiyo ni tabia tu ya mtu kuwa mbinafsi! au ndiyo wale wanaokaa mguu mmoja nje mwingine ndani!
Lakini kwa mwanamke yeyote ambaye miguu yote iko ndani hawezi kuwa hivyo; Japo kiukweli mwanaume ndo anayetakiwa kuwa kinara wa kumudu familia mwanamke anachangia tu!
Japo kusema kweli mwanamke asilimia kubwa la pato lake linaingia katika mahitaji ya kifamilia kwani mwanamke ndo mwangalizi mambo mengi ili maisha yaende inawezekana akawa hamwonyeshi mwanaume kipato chote lakini kinaishia kwenye mambo kama mavazi ya familia(baba na watoto), vyombo, mapambo, n.k
Kikubwa kunapokuwa mapenzi ya kweli/dhati huwezi kuona kipi cha nani bali wote mtaungana ili muweze kufikia malengo mliojipangia! tofauti zinakuja kama hakuna upendo au kuna kaubinafsi mmojawapo kaonyesha, au kuna ufujaji wa pesa kwa mmojawenu.
Asilimia kubwa ya wanawake hapa wamethibisha kuwa chake ni chake na cha mwanaume ni cha familia yaani kipato, kwa hiyo mwanaume atahangaika kulipia karo, bill za maji na umeme, kuhakikisha watoto hawafi njaa, mavazi kwa mama na mtoto wakati huo kipato cha mwanamke hakiguswi kamwe.