Sifa za mwanamke/mwanaume wa kuishi nae

Sifa za mwanamke/mwanaume wa kuishi nae

Evvy jr

Senior Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
140
Reaction score
191
Habari zenu wakuu...
Kuna jambo limekua likinitatiza sana kichwani kwangu. Huwa nakaa nafikiria nadharia mbalimbali za watu juu ya sifa za mwanamke wa kuoa au mwanaume wa kuolewa nae lkn huwa sipati jibu.
Huwa nafurahishwa sana na mzee wangu ambae kiutumishi ni mchungaji, yy huwa ananisisitiza zaidi nizingatie sifa mbili pekee napotafuta binti wa kuoa. Sifa ya kwanza anasisitiza awe ni binti mcha Mungu na sifa ya pili awe ni msichana mzuri wa sura na umbo (anapenda kusema hata wana wa Israel walikua wazuri wa sura na umbo). Cjaelewa kwa nn husisitiza uzuri wa sura na umbo.
Narudi kwako mwana jamvi mwenzangu, Je ni sifa zipi unazingatia kwenye suala la kutafuta mchumba? Na kwa ww ulieolewa/oa ni sifa zipi ulizingatia kwa mwenza wako? Na pia unahisi mzee wangu ni kwa nn anapenda kusisitiza sifa moja wapo iwe ni uzuri wa sura na umbo (kuna siri gani imejificha kwenye uzuri)?
 
Kaka angalia uzuri wa ndani , ndiyo kila kitu, tabia njema.
Alafu fuatilia historia yake ya makuzi pamoja na malezi.
Alafu ndiyo uangalie muonekano wa nje!
Muhimu kumshirikisha MUNGU katika suala la mke/ mume.
 
Huo uzuri akipata madhira ndoani utamuacha uende ukatafute mme au mke mwingine?

Mwambie mchungaji wako aache uzuzu.
 
Hizo Ndio sifa zinazohitajika mkuu, lakini hakikisha awe mcha Mungu kwelikweli
 
Kweli mishahara imetoka hadi Ndoa zimeanza kuzungumziwa hata vyuma vimeanza kulegea nimeamini
 
Itakuwa umepata bint ambaye kimtazamo wako niwakaida sana ila sasa unachohofia mdingi wako atakushangaa kwanini ujachagua mwanamke mzuri wasura naumbo kama alichokwambia?
 
Sifa pekee itakayokufanya ufurahi daima ni uliyenae awe muelewa na usisahau asikufuatilie ovyo ovyo. Na cjui ata kama huyu mtu yupoo
 
Habari zenu wakuu...
Kuna jambo limekua likinitatiza sana kichwani kwangu. Huwa nakaa nafikiria nadharia mbalimbali za watu juu ya sifa za mwanamke wa kuoa au mwanaume wa kuolewa nae lkn huwa sipati jibu.
Huwa nafurahishwa sana na mzee wangu ambae kiutumishi ni mchungaji, yy huwa ananisisitiza zaidi nizingatie sifa mbili pekee napotafuta binti wa kuoa. Sifa ya kwanza anasisitiza awe ni binti mcha Mungu na sifa ya pili awe ni msichana mzuri wa sura na umbo (anapenda kusema hata wana wa Israel walikua wazuri wa sura na umbo). Cjaelewa kwa nn husisitiza uzuri wa sura na umbo.
Narudi kwako mwana jamvi mwenzangu, Je ni sifa zipi unazingatia kwenye suala la kutafuta mchumba? Na kwa ww ulieolewa/oa ni sifa zipi ulizingatia kwa mwenza wako? Na pia unahisi mzee wangu ni kwa nn anapenda kusisitiza sifa moja wapo iwe ni uzuri wa sura na umbo (kuna siri gani imejificha kwenye uzuri)?
Unajua kila mwanamme ana vigezo vyake vya kuchagua mwanamke wa kuishi nae, natumai ww binafsi una vigezo vyako ispokua unahitaji nyongeza kutoka kwetu. Uchamungu ndio kitu cha kwanza kuangalia kwa mwanamke. Pili heshima na jinsi gn anajumuika na familia yake pia na za wenzake. Pesa na uwezo wake wa kiuchumi, mwisho ukoo wake pia unaweza kukufanya ukafunga nae ndoa
 
Nimekupata vzr
 
Back
Top Bottom