kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,818
Wandugu habari, naona vijana wengi wanauliza sifa za kujiunga na kozi za afya, mimi nitajikita kwenye ngazi ya cheti na sitashahada. Ili uweze kusoma kozi yoyote ya afya ngazi ya cheti lazima uwe umefaulu kuanzia daraja D kwa masomo ya Physics,Chemistry na Biology. Ukitaka kusoma sitashahada yoyote ya afya uwe na ufaulu ufuatao, Phys kuanzia D na kuendelea,Chem kuanzia C na kuendelea na Bios kuanzia C na kuendelea. Kama una sifa njoo PM tusaidiane maana kuna chuo kitachukua wanafunzi wa kozi ya maabara mwezi huu. (Pia kuna kozi imeanzishwa hii mpya ya community health ambapo vigezo vyake ni D moja ya somo lolote la sayansi na D tatu kutoka kwenye masomo mengine)