Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
🔹Neno la Mungu halikutengenezei hofu, bali linaondoa hofu na kuleta ujasiri ndani ya mwamini.
🔹Neno la Mungu halikufanyi uwe mnafiki na muongo muongo, linakuonya na kukutahadharisha madhara ya kufanya hayo.
🔹Neno la Mungu halikufundishi kukata tamaa mapema, linakufundisha kujaa matumaini na imani mbele za Mungu, tena katikati ya jangwa.
🔹Neno la Mungu halikufundishi kukalia kimya uovu, linakutuma useme na ukemee dhambi waziwazi bila kumumunya maneno.
🔹Neno la Mungu linakuonya kuhusu rushwa, linakueleza wazi madhara ya rushwa, na kupenda fedha, linaenda mbali zaidi juu ya hilo.
🔹Neno linakutaka kuchukua hatua ya maombi kuomba msaada wa ki-Mungu pale ikiwa shwari na pale hali imekuwa ngumu.
🔹Neno la Mungu linakukumbusha ukiwa upande wa haki uwe na uhakika Mungu hatakuacha uibike katika maisha yako yote.
🔹 Neno la Mungu linakulazimisha kusema hata kama unayosema hayapendwi na waovu, moto unaowaka ndani yako unakufanya useme.
Ninachotaka uelewe ni kwamba usichukulie poa neno la Mungu, usilisome kama gazeti la miji kumi, neno la Mungu ni viwango vingine kabisa vya kukutengeneza uwe vile Mungu anataka.
Kumbatia biblia yako ukijua imebeba ujumbe mzito wa ki-Mungu unaohusu maisha yako ya kiroho na kimwili.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana