Sifa za kiongozi bora

Evari77

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
769
Reaction score
800
Katika jamii yeyote kiongozi bora ni yule anayewapa watu wake matumaini mapya, kuwa tiba ya shida zao na suluhisho la hatima zao na popote alipo utokea amani na si machafuko.

Katika Hali isiyo ya kawaida tumaini linafifia, wanachuo wanafifia kutokana na hali za mkopo wa Elimu ya juu wakati wafanyakazi nao wakifa moyo,

Naunga mkono jitihada za ondoa hewa popote ilipo na sio leta hewa,lkiongozi bora utafuta njia bora kutatua tatizo kubwa bila kuleta sintofahamu

Naomba nizumgumzie vyeti fake hekima ni TUNU kwa kiongozi je n huu mda mwafaka? Na kama lisip[oshughurikiwa sasa litaleta hasara ipi , je njia ngani sahihi inapaswa kutumika haya ni majibu mhimu kabla ya zoezi

Nilipoanza kusikia vyeti feki nilifikili ni mambo ya mtandao,kwa ufahamu wangu nilijua hili jambo kwa wakati huu sio mda mhafaka kwani ipo fomula tu nyepesi ya uongozi uwezi kila siku kuongelea matatizo kana kwamba hakuna jema fomula hii utumiwa na wazazi baba au mama kwa familia yake kama kila siku baba na mama au wazazi uzungumzia motto huyu kafanya lile nalile ubomoa badala ya kujenga kwa ufahamu huu mdogo nilifiliki baada ya wafanyakazi hewa , baaadaye wanafunzi hewa basi nkungekuwa na utulivu ajabu tena nasikia tea tena kwa mshangao waqnatafutwa wanafunzi wasio na sifa ambao wako chuoni ni jambo jema ila sio mda mhafaka kuleta ,mambo mengi makubwa mfululuzo hii si hekima

Hekima utambua mda gani wa kusema na wakujibu swali kwa swali,au kujibu kwa kunyamaza

Katika dunia hii ya sayansi waandae data base iwe openi ambapo mwajili anaweza ku cross check cheti kwa huyo anayeomba kazi au aliopo kazini kama ni fake au la zipo njia nyingi za kutatua tatizo nawasilisha
 
Sijasoma post yako but yaweza kua ni muendelezo wa lawama kwa JPM......!!
 
Nilikuwa naongea na wenzangu nikagundua kila mmoja ana mawazo tofauti, kuna wengine hawa kujua nchi yetu ni socialist au ni capitalist, wengine walikuwa wanasema unampima rais bora kwa msimamo wake na wengine kwa kupambana na rushwa wengine kwa kuangalia GDP per capital, nataka nijue wewe unatumia kigezo kipi kumpima rais bora?
 
Waziri mkuu wa singapore wa kwanza Lee Kuan Yew ni kiongozi bora kwa sababu aliwatoa watu kutoka dunia ya tatu hadi ya kwanza gdp per capital 480 hadi 60000,kwao huyu ni kiongozi bora,kwetu sisi tunapimaje?
 
Anapimwa kwa Uwezo wa kufanya rasilimali zote za nchi kuwa msaada kwa wamiliki ambao ni wananchi wenyewe. Na hapa ndio atapata uhalali wa kusema nchi hii ni tajiri.
 
Kwangu mimi kiongongozi bora ni yule atakaye ongoza watu wake kuwatoa kwenye umaskini.
 
Kipimo ni ustawi wa nchi na hali za wananchi wake. Ni hivi, pale ambapo anapoweza kuitoa nchi kutoka kwenye hali iliyopo kwenda kwenye hali bora zaidi. Kama nchi ilikua masikini basi iende kuwa nchi ya kipato cha kati hadi kuwa nchi tajiri. Utajiri wa nchi unapimwa na mambo mbali mbali, urahisi wa upatikanaji na ubora wa huduma za jamii, miundombinu bora na kipato cha mwananchi wa kawaida. Hivyo basi lazima kiongozi huyo awe na mipango mizuri na rafiki ya kuchumi yenye lengo linaloonekana wazi la kutoa nchi kutoka sehemu iliyopo kwenda sehemu bora zaidi. La khasha, mapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu si mipango ya kiuchumi bali ni sehemu tu ya kuzuia mianya ya upotevu wa mali, kama hakuna mipango ya kimaendeleao ata ukizuia rushwa na ubadhirifu hatuwezi kuendelea, tutabaki kwenye aina ile ile ya uchumi au kuporomoka kabisa, TUNATAKA MAGEUZI YA KIUCHUMI
 
Kiongozi bora ni yule anae kuwa na mipango endelevu, maono,kuto bagua au kupendelea upande mmoja, anaejali demokrasia, mzalendo na maslai ya taifa, apende/kusema kweli sio kigeugeu, self confidence na uwezo wa kusolve tatizo la umaskini sio kama mkulu aliingia kwa mbwembwe nakuonyesha dharau kwa mwenzake kumbe naye ni wa hovyo..
 
Ni yule anayekomesha wananchi wake waishi kama mashetani.
 
Kiongozi bora ni yule anayetanguliza maslahi ya nchi kwanza na sio maslahi binafsi
 
Tatizo letu kubwa wana wa Afrika ni kutokujua tafsiri sahihi kwa mazingra halisi. Dhana ya maendeleo ni pana sana, hata kurudi nyuma ni kuendelea pia kukifanyika kwa awamu nyingine. Mfano, kwa kizazi hiki tafsiri yetu ya maendeleo ni nyumba yenye muonekano wa kimagharibi, gari hata usipokuwa na ulazima nalo, akaunti iliyonona, mke mrembo mwenye kuvutia nk, kwa ngazi ya mtu mmojamoja, kitaifa kuwe na mabarabara ya juu hata kama kungekuwa na njia mbadala, lazima tuwe na ma malls hata kama mahitaji yake hayapo. Kwa kifupi, maendeleo ya kweli ni ya watu ktk hali, mazingira na tamaduni zao. Mchina ataendelea ktk uchinachina wake, vivyo hivyo kwa wa waarabu, wazungu nk...kwangu mi maendeleo ni ktk mbinu mpya za kukabiliana na mazingira mapya, huwa najiuliza ktk ngazi ya mtu mmojammoja, mfano kijana wa maisha ya kawaida tu, akafadhiliwa bilioni 2. Akajenga nyumba ya kisasa yenye kutamanika, akanunua gari nzuri, akaweka akiba kubwa benki, je nae atakuwa ni kijana ALIYEENDELEA ? Vivyo hivyo, mabilionea wakija Tz wakawekeza biashara zao kubwa, nchi ikatamanika machoni mwa watazamaji, nayo tutaiita ni nchi iliyoendelea ? Kuna mambo manne hayapingiki ktk swala zima la maendeleo ktk levo ya kitaifa: ardhi, watu, uongozi bora na siasa safi, Kwahyo kiongozi bora ni yule atakayeweza kuitumia ardhi ya nchi yake kupitia nguvu kazi ya watu wake, na taaluma zao kwa maslahi ya watu wake wote.
 
Habari za mda huu wakuu, kiongozi bora anatakiwa awe na sifa zipi? Je, ni uchapakazi au vyeti? Karibuni tujadili.
 
Uongozi ni Taaluma na kipaji! Uongozi ni kuonyesha njia! Uongozi si vyeti ila pia si kutumia cheti fake! Uongozi ni kuwa na wafuasi wa hiari! Ukifika wasimame kwa hiari si kwa amri!
Mwisho uongozi ni dhamana!
 
Kasome civicz form three sio unasumbua humu ndani
 
SIFA KUU ZA KIONGOZI:
1.Hofu ya Mungu (Uchamungu)
2.Hekima
3.Busara
4.Usikivu
5.Kukubali Kushauliwa/kukosolewa
6.Unyenyekevu.

Ikiwa wewe ni kiongozi na una sifa hizo hakika unaowaongoza watafurahia utumishi wako.

NOTE:
Kwa Bahati mbaya sana Siku hizi sifa hizo Sita MUHIMU kwa watu tunaowapa dhamana ya uongozi hatuzizingatii, tunachokiangalia sasa hivi ni Elimu tu!

Hivi nani aliyeturoga mpaka kuamini kua mwenye elimu sana ndio kiongozi mzuri....!!!??
Siku hizi tumesahau kua Uongozi si taaluma Bali ni kujua namna nzuri ya kutekeleza majukumu yako kwa waliokupa dhamana ya uongozi.

Unaweza ukawa Mhandisi mzuri tena kumzidi hata kaka Yangu Ephraim Tirumanywa Kanyambo au Mwalimu mzuri kumzidi hata ndugu Yangu Mashuve Aron lakini hiyo itabaki kua taaluma yako tu!

Tunapokuja katika maswala ya uongozi ni lazima uwe na sifa hizo ndipo utaweza kufanikiwa katika kuwatumikia unaowaongoza.
[HASHTAG]#IjumaaKareem[/HASHTAG]

Mfua Suleiman Lwahupa
(Mshamba Wa Rufiji)
 
Wakuu Salam.

Baada ya salam napenda kwa ufupi tuangalie sifa za kiongozi ni zipi na ili ufanikiwe zaidi kwa ufupi unatakiwa uwe nazo.

1.ujiheshimu, uwaheshimu na wengine ili nao wakuheshimu.
2.onesha utofauti wenye tija kwa jamii unayoiongoza mfano kama unaongoza jamii yenye njaa jitahidi kufanya uwezalo chakula kipatikane, kama kodi ziko juu jitahidi uwezavyo ushushe kodi ili biashara iwe rahisi.
3.Tumia muda wako mwingi kuunganisha makundi tofauti ili yapatane na kua kitu kimoja na wasigawanyike.
4. Uchukue mazuri ya watu wanaotajwa kua mashujaa katika dunia.
5.jifunze kwa watu wote yani unaowashinda cheo na watu wa ngazi zote.
6.kua mnyenyekevu.
7.kua na msimamo wenye maslahi kwa jamii yako au wale unaowaongoza.
8.jaribu kutafakari kabla haujasema kitu chochote kinachogusa hisia zako na za unaowaongoza.
9.uwe tayari kuyalinda maslahi hata ya wale wanaokupinga.
10.jitahidi uache alama njema za kukumbukwa hata utakapomaliza uongozi au utapokufa mfano. Legacy ya Nelson mandela, muamar gadafi, martin luther king jr, na kadhalika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…