ccm ni chama dola. hiki bila vyombo vya dola hakiwezi ishi....
CCM ni muunganiko wa:
1. Polisi
2. Tume ya taifa ya uchaguzi
3. Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
4. Bakwata
Umesahau Mzee pengo na RC yake japo nami nasali humo.
ROMAN CATHOLIC NA BAKWATA NI MATAWI YA CCM TANGU ENZI ZILEEEE
Salaam
Siasa za vyama vingi zilirejea Tanzania mwaka1992.Kabla ya hapo ilikuwa ni chama kimoja.Wanajeshi walikuwa makada wa chama. (Wah.Kikwete,Kinana,Moses Nnauye nk. Wakati tupo jeshini, ilikuwa mtu akiona muda wa ruhusa umeisha anakimbilia kwa mkuu wa wilaya kuongeza kibali. Akirudi kambini haguswi kwa kuwa 'afande' ameongeza kibali
Siasa za vyama vingi ziliondoa siasa jeshini lakini ni kwa nadharia tu. Katika awamu hii kuna wakuu wa wilaya na mikoa ambao ni wanajeshi na wana magwanda. Wako pia makatibu wakuu. Walikuwa 'wamehifadhi'kadi zao. Ni watiifu kwa chama.
CCM wanaweza kumpa cheo chochote ofisa wa jeshi na asiwakatalie ingawa ni kinyume cha taratibu. Majeshi bado ni jumuiya za Chama Cha Mapinduzi.
CCM imepiga marufuku vyama vya upinzani visifanye siasa, yenyewe inafanya mikutano ipendavyo, tena kwa rasilimali,miundombinu na muda wa serikali.
CCM na Magufuli hawawezi kufanya siasa za ushindani. Wanategemea jeshi la polisi kuwasaidia. Ukiondoa dola, CCM ni chama dhaifu sana.
Opposition wanasakwa na polisi na kufunguliwa mashtaka. Zamani waliambiwa ni vyama vya msimu,ha wana anuani,wanafanya siasa wakati wa uchaguzi. Sasa hivi wakifanya siasa wanaambiwa wanamzuia Rais kuleta maendeleo. Wakifanya CCM hawazuii maendeleo.
Siku mbili zilizopita Rais alifanya kikao na wakuu wa majeshi wastaafu. Alisema anabadilishana nao uzoefu. Nadhani ni zaidi ya hapo. Alitaka wa-plead allegiance. Si angewaita kina Mkapa, Kikwete na wengine wa kisiasa?
Kutumia majeshi yakusaidie kwenye siasa ni woga. Woga unazaa maamuzi yenye utata. Hii ni tabia halisi ya madikteta. CCM haiwezi kukamilika bila majeshi.
Ukiondoa majeshi/dola inakiua.
Hiki si chama cha siasa kwa kuwa hakikubaliki kwa kuuza sera na kujenga hoja, kinatumia, vitisho na ulaghai.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hawasomi katiba wataijulia wapi? Na kama wanaisom basi ni wanafiki.Bila kamanda Sirrrro hakuna kitu
Naye sirrrrrro kakomaa kunyanyapa wapinzani utazani magaidi kumbe katiba inaruhusu vyama vingi.
Jibu ni rahisi hata usiumize kichwa.Mimi pia ni RC lakini nimejiuliza swali moja juzi. Kwamba jaji mkuu wa Kenya David Maraga siyo kiongozi wa dini. Lakini ametenda haki. Je kama ile kesi ingekuwa ni CDM vs CCM na kama CDM ingekuwa ndo NASA na ikaleta ushahidi ule wote kama ilivyofanya NASA, na kama maaskofu wetu kanisa katoliki wange preside hiyo kesi chini ya Pengo, je CDM wangepata haki yao?
Hii nondo.Na pia ndio waliomtuma Lowassa aende cdm kuangalia wanafanyaje?
Opposition washajiharibia sana, unayoyasema utaamini katika kushindwa tu...ila CCM huwa nasema iliishakufa kitambo sana. Tatizo ni upinzani sasa kwa akili yako kuzuiwa siasa unaona ni sababu!???? unazuiwa unakaa kimya kisha unailaumu CCM???..
mi naona upinzani wanataka kuingia ikulu bila hata kupata shida!! will never happen
ndio maana unakuta akili za kushindwashindwa, execuse nyingiii kama hizi
Kwanza ulishawahi kushuhudia Rais DIKTETA!Kwa taarifa yako JPM angekuwa DIKTETA hata hiyo thread usingeiandika!
Mimi pia ni RC lakini nimejiuliza swali moja juzi. Kwamba jaji mkuu wa Kenya David Maraga siyo kiongozi wa dini. Lakini ametenda haki. Je kama ile kesi ingekuwa ni CDM vs CCM na kama CDM ingekuwa ndo NASA na ikaleta ushahidi ule wote kama ilivyofanya NASA, na kama maaskofu wetu kanisa katoliki wange preside hiyo kesi chini ya Pengo, je CDM wangepata haki yao?